Pages

KAPIPI TV

Friday, December 21, 2012

MAHABUSU AFIA POLISI KATIKA MAZINGIRA TATA.


Na Anthony Mayunga-Mara
Desemba 21,2012.

MAHABUSU mmoja katika kituo kidogo cha polisi cha Gibaso kata ya
Nyarukoba wilayani Tarime Ryoba Marwa Mngoreme(70) mkazi wa kijiji cha
Murito amekufa katika mazingira tata huku polisi wakidai alijinyonga
kwa kutumia kamba ya jaketi lake.

Tukio hilo linadaiwa kutokea desemba 21 majira ya kati ya saa 4 na 5
asubuhi mwaka huu katika kituo hicho limethibitishwa na kamanda wa
mkoa wa kipolisi Tarime na Rorya Justus Kamugisha.

Kamanda huyo amesema mahabusu huyu amekufa wakati anapelekwa hospitali
kwa matibabu”amefia njiani wakati anapelekwa hospitalini…amejinyonga
kwa kutumia kamba ya jaketi lake …nafuatilia tukio hili vizuri nitatoa
taarifa”alisema.

Alipotakiwa kueleza mahabusu huyo ameshikiliwa kwa muda gani hadi
anakutwa na mkasa huo ,alidai hajui na kuwa anaendelea na ufuatiliaji
wa tukio zima.

Ndugu waeleza.

Chacha Marwa Rhobi(46) mtoto wa marehemu huyo akiongea na Mwananchi
kwa njia ya simu amesema kuwa baba yake alikamatwa desemba 19 ,mwaka
huu na askari watatu wa kituo hicho kwa tuhuma za migogoro ya ardhi.

“Baba yangu amepigwa si kwamba amejinyonga…mama amekuja jana akamletea
chakula akiwa vizuri wakiwa wanakataa kutoa dhamana kwa misingi ya
rushwa …hii taarifa sikubaliani nazo”alisema.

Alisema kuwa yeye amefika kituoni hapo kupeleka chakula kama kawaida
amefika na kuambiwa kuwa anaumwa amepelekwa hospitalini Tarime kwa
ajili ya matibabu,bila kumweleza ameugua nini.

“Pia nilikuwa nakuja kumdhamini pia ingawa walikuwa wanazuia sana kwa
misingi ya rushwa …nadhani walimpiga sana wakiwa katika misingi ya
kudai rushwa …na amekufa sasa wanawaya waya kwa maneno ambayo
hayaeleweki”amesema.

Alisema alipofika ofisi ya diwani wa kata hiyo ndipo akapata ukweli wa
mambo kuwa baba yake ameuawa kwa kupigwa na gari la polisi limefika
haraka na kuchukua mwili kwa madai kuwa ni mgonjwa.

Diwani.
Diwani wa kata ya Nyarukoba Mstapha Masiani ameliambia gazeti hili
kuwa taarifa alizonazo ni kuwa amekufa kwa kipigo ,na kuwa tabia hiyo
imezoeleka na kumegeuka kituo cha mateso kwa wananchi.

“Hakujinyonga amepigwa walipoona amekufa sasa wanadai
kajinyonga…taarifa za ndani kutoka kituoni hapo zimenifikia maana si
kila mmoja anafurahishwa na mauaji ya raia”alisema.

Alidai kuwa mara baada ya mauaji hayo wamebadilisha hadi askari polisi
waliokuwa hapo na kuleta wengine”gari la polisi limefika na askari
wengine na kuwatoa hao,malalamiko ya ukatili wanaoufanya yako ngazi
zote”alisema.

Polisi wahofia kituo kuchomwa.
Kubadilishwa haraka kwa polisi kituoni hapo habari zinadai kuwa
ilikuwa ni hofu ya polisi hao kuwa huenda matukio kama ya Ngara
yakajirudia ya wananchi kuvamia kituo cha polisi na kukichoma.

Wananchi waomba uchunguzi wa kina.
Baadhi ya wananchi kijijini hapo waliowasiliana na mwandishi wa habari
hizi walisema kuwa uchunguzi wa kina wa mwili wa marehemu huyo
ufanyike kwa uwazi na taarifa iwekwe hadharani ili kuondoa utata huo.

No comments: