Pages

KAPIPI TV

Monday, December 10, 2012

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU WAADHIMISHA SIKU YA HAKI ZA BINADAMU DUNIANI

Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na haki za binadam LHRC Dr.Helen Kijobisimba akiongoza maandamano ya amani wakati wa Maadhimisho ya Siku ya haki za binadamu duniani ambayo yalipita mitaa kadhaa ya jiji la Dar-es-salaam na kuhitimishwa katika Viwanja vya TTCL. 
Mkurugenzi wa LHRC Dr.Helen akisoma ripoti ya miaka 10 ya hali ya haki za binadam nchini ambapo alieleza bado kuna changamoto kubwa kukabiliana na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini.
Burudani ya vijana wa Makirikiri ya Dar-es-salaam nao walikuwa ni sehemu ya maadhimisho hayo ya siku ya haki za binadamu duniani ambayo yanaadhimishwa kwa mwaka wa 64 tangu kuanzishwa kwake.
Rais wa Chama cha wanasheria Tanganyika  wakili Francis Stola akizungumza katika maadhimisho hayo.
Wafanyakazi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi ya juu wa kituo hicho.





No comments: