Pages

KAPIPI TV

Sunday, December 23, 2012

"KITUMBO USIWE KAMA RAGE TUNAKUAMINI"-WADAU WA SOKA TABORA

Na mwandishi wetu maalum.

Muda mfupi tu baada ya kuchaguliwa kukiongoza chama cha soka mkoa wa Tabora Tarefa,baadhi ya wadau wa soka mkoani hapa wamemtaka mwenyekiti wa chama hicho Yusuph Kitumbo kukiongoza chama hicho na kuhakikisha kunakuwepo mabadiliko yatakayoleta maendeleo ya kweli.

Wadau hao ambao hawakutaka kutajwa majina yao wamemtahadharisha Kitumbo kutokuwa kama mwenyekiti aliyemaliza muda wake Aden Rage kwa madai kwamba tangu achaguliwe kukiongoza chama hicho hakuleta maendeleo yoyote zaidi ya kuwepo kwa migogoro na viongozi wenzake hali iliyosababisha chama hicho kukosa muelekeo.

"kila siku marumbano,Rage ameshindwa kuweka ofisi ya Tarefa licha ya kuwa amekuwa na nafasi nzuri ukiachilia mbali ya Mwenyekiti wa Simba,hata kutumia nafasi ya Ubunge wake pia kukiimarisha Tarefa nayo imemshinda!!"alisema mmoja wa wadau wa soka Tabora.

Sambamba na hilo mwingine amediriki kuweka wazi kuwa"Rage kwa wastani kipindi chote alichodai kuwa anaiongoza Tarefa alikuwa haongei na katibu wake Albert Sitta hata salaam tu ilikuwa ni ngumu,sasa hapa mpira ungeendelea vipi ndugu mwandishi"

"Eti mimi nashangaa wakati fulani Rage alitangaza kuvunja uongozi wote wa Tarefa lakini tukashangaa amerudi kimya kimya,hili jambo lilitufanya tuone kuwa huyu kiongozi hatufai tumeingia mkenge afadhali abaki huko kwenye CCM yake ndio wanakubali mambo ya aina hiyo,kwakweli Rage aliturudisha nyuma sana hapa Tabora kwa soka"mdau mwingine alisema

"Kwakweli kwasasa tunamuomba sana Kitumbo kama kweli ameamua kuleta mabadiliko basi afanye kweli aepuke ubabaishaji uliokuwa unafanywa na viongozi waliopita"     

Hata hivyo Safu mpya ya viongozi hawa wa Tarefa wameonesha matumaini makubwa na huenda kukawa na mafanikio endapo kama watatekeleza mipango na maazimio yao na kubwa zaidi wakiondoa ubinafsi.  

   

No comments: