CHAMA
soka mkoa wa Tabora,(TAREFA),kimefanya mkutano wake mkuu na
kuchagua viongozi ambao watakaa madarakani kwa kipindi cha miaka
minne.
Uchaguzi huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka ya maji safi na maji taka,mjini Tabora,TUWASA.
Akitangaza
matokeo ya uchaguzi huo mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi Bwire
Mkama,alisema nafasi ya mwenyekiti ilikuwa na wagombea watatu ambapo
Yusuph Kitumbo alishinda kwa kura (16), akifuatiwa na Mussa Ntimizi kura
(8), huku meneja wa TRA Tabora akipata kura (0) ambapo kura halali zilizopigwa ni 24 na hakukuwa na kura hata moja iliyoharibika.
Mkama
aliongeza kuwa nafasi ya katibu wa TAREFA ilikuwa na wagombea wawili
ambapo Fath Remtullah Dewij alishinda kwa kura (17), na kumshinda katibu wa
TAREFA zamani Albert Sitta aliyepata kuwa (7) kura zilizopigwa 24.
Mwenyekiti
huyo wa kamati ya uchaguzi alitangaza nafasi mwakilishi wa vilabu
ilikwenda kwa Lazack Ilumba akishinda kwa kura (13),huku nafasi mjumbe
wa mkutano mkuu TFF ikienda kwa Dick Mlimuka aliyepata kuwa (14).
Mkama
alimtangaza mshindi wa nafasi ya mwakilishi wa soka la wanawake ambaye
alikuwa mgombea pekee Janeth Michael aliyepata kura (22),huku nafasi ya
mjumbe kamati ya utendaji ikienda kwa Stanlaus Shija aliyeshinda kwa
kura (22).
Aidha
mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi alitamka kuwa nafasi kadhaa bado ziko wazi
kwa kukosa wagombea huku nafasi moja mgombea akijitoa kwa kutingwa na
majukumu mengi.
Mkama
alitaja nafasi zilizowazi kuwa ni nafasi ya makamu mwenyekiti,katibu
msaidizi,mjumbe wa kamati ya utendaji na mweka hazina msaidizi huku
nafasi ya mweka hazina Musa Msananga akijitoa kwa kuandika barua akidai kutingwa na majukumu ya kikazi.
Mwenyekiti
mpya wa TAREFA aliyeshinda uchaguzi huo Yusuph Kitumbo katika nasaha
zake alisema anavunja makundi yote ili kujenga uongozi imara wenye
kutaka kuleta maendeleo ya soka mkoa wa Tabora.
Kitumbo aliongeza moja kazi zake atakazoanza nazo ni pamoja na kuhakikisha chama kinakuwa na ofisi ya kisasa inayotambulika.
Aidha
aliongeza kuwa kazi nyingine ni kuhakikisha uongozi wa wilaya nao
unatimiza majukumu yao ipasavyo na sanjari na kuwa na ofisi
zinazoeleweka.
Alisema
atahakikisha vikao vyote vya kikatiba vinafuata taratibu na kalenda
kamwe hatakuwa mtu wa makundi daima atahakikisha upendo mshikamano na
utulivu vinakuwepo miongoni mwa viongozi walioshinda na wagombea wote
walioanguka kwenye uchaguzi huo atashirikiana nao pia.
Hata hivyo baadhi ya wadau wa soka mkoani Tabora macho na masikio yao kwasasa wamemuangazia Yusuph Kitumbo ili kuona kama atakuwa na uwezo wa kuleta mabadiliko ya kweli kwa Chama hicho.
No comments:
Post a Comment