KESI ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael (Lulu), dhidi ya aliyekuwa msanii mwenzake, Steven Kanumba, inaendelea kupigwa kalenda kwa madai kwamba upelelezi haujakamilika.
Kesi hiyo iliahirishwa juzi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi, Augustino Mbando. “Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii haujakamilika, tunaomba tarehe nyingine ya kutajwa,” alidai Wakili wa Serikali, Kenneth Sekwao.
Hakimu Mbando alikubali kuahirisha kesi
hiyo hadi Desemba 17 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa. Mtuhumiwa
Elizabeth Michael anatetewa na mawakili, Kennedy Fungamtama, Peter Kibatara na Fulgence
Masawe.
Lulu yuko rumande kwa miezi nane sasa kutokana na tuhuma za makosa ya
mauaji na kukosa dhamana, inadaiwa kwamba mnamo Aprili 7 mwaka huu maeneo ya
Vatican, Sinza, alimuua Steven Kanumba.
Kuchelewa kukamilika kwa
upelelezi kumeanza kuzua mjadala kwa watu mbalimbali wanaofika
kusikiliza kesi hiyo, wakidai kwamba hawajui matukio gani nchini ambayo
upelelezi wake unaweza kufanywa kwa haraka.
“Nashindwa kuelewa, kila
siku upelelezi bado, kuna upelelezi gani katika kesi hii wa kumaliza
mwaka mzima, kila kesi ina mazingira yake ya kuchelewesha upelelezi
lakini hii…” alihoji msikilizaji huku akitoka katika chumba cha
mahakama.
No comments:
Post a Comment