Imedaiwa kuwa matapeli hao wamekuwa
wakitumia jina la mbunge huyo Deo Haule Filikunjombe kwa kupigia watu
simu na kuomba kutumiwa fedha jambo ambalo ni sawa na utapeli wa
kutupwa .
Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao
huu wa www.francisgodwin.blogspot.com unaonyesha kuwa baadhi ya watu
tayari wamekwisha lizwa na utapeli huo ambapo matapeli hao wamekuwa
wakijitambulisha kuwa wao ni Deo Haule Filikunjombe japo si kweli.
Hadi sasa tayari watu kadhaa wamelizwa
kupitia jina la mbunge huyo na kuwa wapo waliosajili namba zao kama
Deo Haule kumbe ni matepeli na mmoja kati ya walionusurika kutapeliwa
ni pamoja na mkurugenzi wa kituo cha radio Njombe ambae alionyesha
kushitukia utapeli huo .
Kwa upande wake mbunge Filikunjombe
amewataka wananchi kuwa makini na utapeli huo na kuwa hana kawaida ya
kutumia mtu kuazima pesa na kuwataka wananchi wasikubali kuamini
mazungmzo ya kwenye simu ambayo hutumiwa na matapeli hao .
Filikunjombe pia amewapa pole wale wote waliotapeliwa na matapeli hao na kuwataka kuwa makini na utapeli huo .
No comments:
Post a Comment