Na Anthony Mayunga-Serengeti
WAKATI wanaharakati wanazindua siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ,wazee wa baadhi wa mila baadhi ya maeneo wilaya ya Serengeti wamepanga kuanza
ukeketaji na tohara kwa vijana wa kiume
kuanza desemba 15 mwaka huu.
Uamzi wa wazee wa mila kwa baadhi ya maeneo ambao unafanywa kisirisiri imebainika kuwa itakuwa ni siku moja baada ya kufungwa kwa shule za msingi desemba 14,2012.
Habari za uhakika ambazo zimethibitishwa na baadhi ya wazee wa mila zinadai kuwa muda huo umepangwa ukizingatia tarehe ambazo ngariba wa vijana wa kiume atakuwa amemaliza kazi nchini Kenya.
“Ngariba wa kiume anatokea nchini Kenya ambako kwa sasa wanaendelea na kazi ya kutahili…kuanzia tarehe hizo atakuwa amemaliza na ndiyo maana wamepanga tarehe hizo…”alisema mmoja wa wazee wa mila jina limehifadhiwa.
Aliliambia Mwananchi kuwa ngariba wa kike wapo vijijini lakini kwa mila na desturi watoto wa kike hawawatangulii vijana wa kiume,hivyo kazi hiyo itafanyika kwa wakati mmoja hasa maeneo ya kata ya Kebancha bancha.
Akizungumzia tishio la serikali la kuwakamata watakaohusika na kukeketa watoto wa kike ,alisema kuwa kuacha itakuwa kazi ngumu kwa kuwa mila na desturi itakuwa imepotea.
“Ili kutopoteza mila wanakata kidogo sana ili damu ionekane imevuja,kuacha kabisa ni vigumu haya mambo yatakwenda taratibu yaishe yenyewe kama ilivyokuwa kwa kutoga masikio”alibainisha.
Hata hivyo baadhi ya maeneo wazee wa mila wakiulizwa msimamo wao kuhusu kuacha ukeketaji wamekuwa wakisukumia wanawake kuwa ndio wanashawishi watoto wa kike ,huku akina mama wakisema wenye sauti ni wazee wa mila kwa kuwa ndio wanaoheshimiwa na jamii.
“Kuna kusukumiana kwa wazee wa mila na akina mama … wazee wa mila wanasema akina mama wanachangia kuendelea kwa ukeketaji kwa kuwa huwadanganya watoto kuwa wanaenda kusalimia bibi zao …huko hukeketwa kwa aibu yao kwa jamii ni kubwa kuliko wanaume,”alisema.
Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa wanawake wananyanyapaliana sana kama kuliko wanaume hasa mabinti zao wanapokuwa hawajakeketwa,hali ambayo pia huwaathiri watoto wa kike
kutengwa na wenzao na wengine hutoroka kwenda kukeketwa.
Baadhi ya mashirika yanayotoa elimu ya kupinga vitendo vya ukeketaji kwa wilaya za Serengeti na Tarime hasa Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT)wamesema kuwa wana uhakika wa kupokea watoto wengi
watakao kimbia kukeketwa.

No comments:
Post a Comment