MWANAMKE anayetuhumiwa kumnyanyasa
mtoto wa dada yake kwa kumfungia ndani na kumchoma kwa maji ya moto, hatimaye
amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Mbeya kujibu shitaka
linalomkabili.
Mwendesha mashtaka wa Serikali,
Achiles Mulisa ameiambia Mahakama kuwa
Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth.
Mtuhumiwa Wilvina Mkandala (24) alitenda kosa la kusababisha majeraha akiwa na nia ovu ambayo imemsababishia ulemavu mtoto Aneth.
Mulisa akisoma mashtaka hayo mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo Gilbert Ndeuruo amesema kosa hilo ni
kinyume cha kanuni ya adhabu kifungu cha 222(a) sura ya 16 kama
ilivyorejewa mwaka 2002.
Kutokana na kosa hilo mshtakiwa
amekana shitaka hilo ambapo amerudishwa mahabusu hadi Novemba 22, Mwaka huu
kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mwendesha mashtaka huyo alisema
Mshakiwa amenyimwa dhamana kutokana na hali ya mhanga ambaye ni mtoto Aneth
kutokuwa ya kuridhisha na kuongeza kuwa sababu nyingine ni kwa ajili ya usalama
wake.
Alisema upande wa Jamhuri
una mashahidi wanne ambao wataanza kutoa ushahidi wake mahakamani hapo Novemba
22, Mwaka huu kutokana na upelezi kukamilika.
Aliwataja mashahidi hao kuwa ni
Mwenyekiti wa Mtaa wa Majengo Shukuru Mwakanyamale, Daktari anayemtibu mhanga
katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya Dr. Paul.
Wengine ni Askari Polisi
aliyepeleleza kesi hiyo WP Pudensia na Habiba Mwakanyamale ambao wako tayari
kufika mahakamani na kutoa ushahidi wao mbele ya mahakama.
Awali mshatakiwa huyo aliieleza
mahakama kuwa na uhusiano na mtoto huyo ambapo pia alikiri kuwa na
taarifa za kile kinachoendelea juu ya matibabu ya mtoto huyo na kuhusu kukatwa
kwa mkono wake wa kushoto na kufungwa bandeji ngumu(POP) kwenye mkono uliobaki.
No comments:
Post a Comment