Baadhi ya waombolezaji wakisawazisha kaburi la marehemu Sinjembele Julius(62) aliyeuawa kwa kupigwa na mwanae Ndele Julius(25)
Baadhi
ya waombolezaji wakishiriki mazishi ya Sinjembele yaliyofanyika nyumbani kwake katika kitongoji cha Igawilo kata ya Swaya Mbeya
Kaburi baada ya kuzikwa marehemu
Mkazi
wa Swaya jijini Mbeya Ndugu Ndele Julius amemuua mama yake mzazi kwa
kumpiga mateke na ngumi kisha kutoroka kuelekea pasipo julikana Novemba
25 mwaka huu. Tukio
hilo limetokea majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa mama huyo mara baada
ya kutokea kwa ugomvi kati ya mtoto wake na kijana mwingine hali
iliyopelekea mama huyo kuingilia ndipo alipo kutwa na mauti huo.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoani humo Ndugu Diwani Athumani amesema
kuwa Chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliokuwepo kati ya mtoto wake na
kijana mwenzake kitendo ambacho kilipelekea mama huyo kuingilia ugomvi
huo.
Amesema
wakati mama huyo akijaribu kuamulia ugomvu huo mtoto wake alicha
kupigana na mwenzake na kuanza kumshambulia mama yake kwa kumpiga
ngumi na mateke mwilini.
Amesema
mama huyo alifariki muda mchache kutokana na kupigwa sehemu mbalimbali
za mwili wake na kusababishiwa majeraha makuibwa yaliyopeleka kupoteza
uhai wake.
Awali
akizungumzia tukio hilo Mtoto wa Kwanza wa mama huyo Ndugu Razaro
Mbwiga amesema kuwa mdogo wake alikuwa na tabia ya kugombana na mama
yake marakwamara.
Hata
hivyo teyari mwili huo umekwisha chukuliwa hospitali na kuzikwa ambapo
katika maziko hayo Chama cha Muungano wa kijamii (Mujata) umewataka
vijana kujiepusha na vitendo viovu kama uvutaji bangi na pombe za
kienyeji kwani ndio chanzo cha kutokea kwa vurugu nyingi.
Na E .Madafa picha kwa hisani ya Joachim Nyambo
No comments:
Post a Comment