Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo.
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa na msako unaendelea kuwatafuta wengine waliohusika katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment