Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam Suleiman Kova akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya
na Taasisi za kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda ambapo amefafanua
kuwa pamoja na mambo mengine Sheikh huyo anahusishwa na kundi
lililovaamia kiwanja No. 311/3/4 BLOCK “T” eneo la Chang’ombe katika
Manispaa ya Temeke mali ya Kampuni ya AGRITANZA.
Jeshi
la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtia mbaroni Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda.
Akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya
Polisi ya Dar es Salaam Sulemain Kova amesema Jeshi hilo
limechukua hatua hiyo kutokana na Sheikh Ponda kutuhumiwa kwa makosa
mbalimbali ya kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani.
Hata
hivyo leo katika jiji la Dar es Salaam kumekuwa na patashika kati ya Polisi wa kutuliza ghasia baina ya waandamanaji waliokuwa wakitaka
Sheikh huyo kuachiwa pamoja waumini wengine wanaoshikiliwa.
No comments:
Post a Comment