Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wa U.W.T Tabora wakiwa wamepanga foleni eneo ambalo limekuwa likitiliwa shaka kuwa linatumika kupokelea rushwa kwa wajumbe hao wakati wa uchaguzi mkuu wa Viongozi wa ngazi ya mkoa.
Afisa wa Takukuru Bi.Julieth Mtui akijaribu kuwatahadharisha wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi unaofanyika katika ukumbi wa Frankmann Hotel mjini Tabora.
RUSHWA CHOONI
Katika hali ambayo imeendelea kutiliwa shaka ndani ya eneo la uchaguzi mkuu wa U.W.T mkoa wa Tabora ukumbi wa Frankmann Hotel ambapo vitendo vya rushwa viliendelea kutawala licha ya kuwa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru ikichukua hatua kadhaa katika kukabiliana na vitendo hivyo.
Baadhi ya watu wanaodaiwa kutumiwa na wagombea katika uchaguzi huo wamekuwa wakijaribu kutoa fedha kwa lengo la kutaka mgombea fulani aweze kuchaguliwa katika kinyang'anyiro hicho.
Kwaupande mwingine Takukuru baada ya kubainika kuwa wameendelea kuwabana wapambe wanaodaiwa kuwa na mafungu ya fedha walizopatiwa na wagombea kwa lengo la kugawa,utaratibu wa utoaji wa rushwa ulibadilika na kuanza kutolewa chooni hali ambayo kwa mara ya pili maafisa wa Takukuru walibaini hilo na kuanza kulifuatilia na kutoa tahadhari kwa wajumbe waliohudhuria katika mkuutano huo.
"Jamani kinamama mliosimama na kupanga foleni huko chooni tumebaini mchezo unaoendelea huko,tunawaombeni muondoke haraka"mmoja kati ya maafisa wa Takukuru alishika kipaza sauti na kutoa tamko hilo.
Hata hivyo licha ya tamko hilo kuonekana kuwa na nguvu,mchezo huo mchafu ukahamia nje ya ukumbi huo wa mkutano wa uchaguzi na hapo sasa baadhi ya wajumbe walikuwa wakijipatia fedha zilizokuwa zimekunjwakunjwa kama karatasi ambayo isiyokuwa na thamani.
Jambo hilo limeendelea kutilia shaka na kuonekana kuwa vitendo hivyo vya rushwa bado vitaendelea kutia dosari kwa Chama cha Mapinduzi kutokana na ukweli kwamba mtu asiye na fedha hana nafasi ya kupata uongozi katika Chama hicho.
Habari ambazo hazijathibitishwa hadi sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya milioni Sitini na sita tayari zimekwisha teketea katika uchaguzi huo kama sehemu ya rushwa.
No comments:
Post a Comment