Habari zilizotufikia muda si mrefu ni kwamba kiongozi wa jumuiya ya Uamsho, Ustaadh Farid amepatikana akiwa katika hali nzuri na kwa sasa yupo kwao kwa mzazi wake akipumzika. |
Vipeperushi vinavyotishia uhai wa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar vimepeperushwa mjini hapa
kufuatia ghasia zinazoendelea kwa siku ya tatu mfululizo.
Kipeperushi kimojawapo kinasema: “CCM
kosa letu kuwatia mbwa msikitini. Sasa tunasema kuwa basi tena
litakalokuwa na liwe kwa sisi CCM basi tena umoja na CUF.
Nyie CUF/Muamsho Abubakari Khamis Bakar (Waziri wa Katiba), Mussa
(Kamishna wa Polisi) na Azizi (Kamanda wa Polisi Mkoa) mmeshazoea fujo
na sisi sera yetu CCM sera yetu amani sasa mujiuzulu mumpishe Rais
afanye kazi zake, Tumechoka na nyinyi juu ya mauaji ya askari wetu.
Ondokeni murudi kwenu.
Wewe Abubakar hukuanza leo na jana ufisadi kazi ya ufisadi umeizoweya hadi ulifungwa jela na mafisadi wenzako, mwishowe huku SMZ kumekuokoa.”
Wakati huo huo kuna waraka umesambazwa ambao umewatisha khofu waumini wa
dini ya kikristo nchini ukisema wote watakatwa vichwa waraka huo ambao
unasemekana umetolewa na watu wenye kujiita jumuiya ya Uamsho umeandikwa
na kusambazwa katika maeneo mbali mbali huku wenyewe wakristo
wakipelekewa maofisini kwao.
Akizungumza na masikitiko Askofu wa Kanisa la Anglikan Mkunazini
Emmanuel Masoud amesema ni waraka ambao umewastusha wakristo kutokana na
maneno mazito yalioandikwa humo ambapo ndani ya waraka huo.
“Maneno yaliandikwa humu yametushitua sana sisi waumini wa dini ya
kikristo hapa Zanzibar kwa kweli sio jambo la kupuuzia ikiwa
wanasema watatukata vichwa ni jambo la hatari kabisa” alisema Masoud.
Wakizungumzia ukweli juu ya suala hilo Sheikh Azzan amesema jumuiya yake
haihusiki na waraka wa aina hiyo na wao kama waislamu hawana sababu ya
kuwatisha watu kwa kuwa wanaamini uislamu sio dini ya kuwabagua watu
wala kuwatisha watu.
Azzan alisema wapo baadhi ya watu ambao
wanatumia propaganda mbaya za kutaka kuwagawa wazanzibar katika kipindi
hiki na ndio wanatumia kila sababu za kuwagawanya lakini
aliwatahadharisha wananchi kuepukana na propaganda kama hizo kwani
zinaweza kuitia nchi katika pahala pabaya na kutoweka kwa amani.
“Sisi hatuhusiki na waraka huo aliyetoa waraka huo ni watu ambao
wanapingana na amani iliyopo lakini pia ni watu wenye kueneza propaganda
mbaya za kutaka kuwagawa wazanzibari jambo ambalo sisi tunaamini hatuna
ugomvi na wazanzibari wote sisi ni dugu hatubagui awe ni mkristo au
muislamu awe mweupe au mweusi hatuwezi kubaguana kwa kuwa misingi ya
dini yetu imekataza kubaguana” alisema Azzan
No comments:
Post a Comment