Pages

KAPIPI TV

Monday, October 8, 2012

SEIF GHULAMALI NDIYE MWENYEKITI MPYA UVCCM MKOA WA TABORA

 Mwenyekiti mpya wa UVCCM Sief Hamisi Ghulamali muda mfupi mara baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi mkuu mkoani Tabora,Ghulamali atashika wadhifa huo kwa muda wa miaka mitano.
 Wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi wa UVCCM mkoani Tabora wakishangilia ushindi wa mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya umoja wa vijana Seif Ghulamali.
 Baadhi ya wajumbe wakiwa wanasubiri kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo baada ya kupiga kura katika ukumbi wa chuo cha utumishi wa umma Uhazili mjini Tabora.
 Mjumbe mmoja akiwa ametoka kuchukua chakula wakati akisubiria kwa hamu kubwa matokeo ya uchaguzi huo.
 Mgombea wa nafasi ya uenyekiti UVCCM, Sunday Kabaye akitoa neno la shukrani katika uchaguzi huo baada ya kushindwa na kukubali matokeo.
 Mwenyekiti wa UVCCM Seif Ghulamali mara baada ya kutajwa kuwa mshindi katika kinyang'anyiro hicho ambapo ukumbi mzima ulizizima kwa vifijo na ndelemo.

Na  Hastin Liumba,Tabora

Jumuiya ya umoja wa vijana  chama cha mapinduzi,(UVCCM),mkoa wa Tabora imekamilisha uchaguzi wake jana huku vitendo vya rushwa vikiwa nje nje hali iliyopelekea diwani wa kata ya Kitete,(CCM),kuchapwa makofi na afisa wa TAKUKURU.

Katika uchaguzi  huo ambao ulifanyika kwenye ukumbi wa chuo cha utumishi wa umma,kampasi ya Tabora,ulianza majira ya saa sita mchana.

Aidha wagombea wa  nafasi ya mwenyekiti katika jumuiya hiyo walikuwa ni Sunday Kabaye,Seif Ghulamali na Janeth Masika.

Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi huo,Idd Ame alimtangaza Seif Ghulamali kuwa mshindi baada ya kujizolea kura 336,Sunday Kabaye kura 156 na janeth Masika kura 6 na kura halali ziliopigwa ni 499.

Baada ya uchaguzi huo kutangazwa matokeo yake,baadhi ya wajumbe kutoka wilaya ya Kaliua,waliteta na gazeti hili kuwa walipewa maelekezo na “Profesa” bila kutaja jina wamchague Ghulamali.

“Tulitakiwa kumchagua Ghulamali huku mweznetu mmoja akisema maelekezo hayo ni kutoka kwa profesa……tukawa hatuna jinsi na chai tulishapewa.” Alisema mjumbe huyo huyo akigida bia yake ya Balimi.

Chanzo kingine cha habari kilisema kuwa kuna kundi moja ambalo mgombea wao alishindwa kwenye kiti cha jumuiya ya UWT,hivi karibuni lilijiapiza kuwa baada ua kushindwa UWT wataonyeshana ubabe kwenye uchaguzi wa UVCCM.

Aidha kundi hilo baada ya jana matokeo kutangazwa lililipuka kwa shangwe huku likicheza muziki wa taarabu na kumkejeli mgombea aliyeshindwa Sunday Kabaye,kwa kuimba Sunday!Sunday!Sunday!.
Chanzo kimoja cha taarifa kilibainisha kuwa kundi hilo tayari limeanza kujipanga na kudai kiti cha WAZAZI, mkoa watakibeba ili heshima iwepo.

Wakati hayo yakiendelea nje ya ukumbi,baadhi ya wajumbe walisema endapo ujinga huo utaendelea watahama chama bila kueleza watahamia chama gani.

Walisema jumuiya ya UVCCM imeletewa kiongozi wa kuongozwa na rimoti kwa maslahi ya kundi la watu wachache.

Aidha tukio la kupigwa makofi na kufukuzwa kwa diwani wa kata Kitete na maafisa wa TAKUKURU kuliashiria kuwa uchaguzi huo uliashiria ulikuwa na vitendo vya rushwa.

Chanzo kimoja cha taarifa kilisema ndani ya ukumbi rushwa ilikuwa ya wazi wazi kwa wajumbe kushinikiza mgombea mmoja achaguliwe.

No comments: