Pages

KAPIPI TV

Thursday, October 11, 2012

NYOTA YA MEYA WA MANISPAA YA TABORA GHULAM DEWIJ YAZIDI KUNG'AA NDANI NA NJE YA CCM

 Kutoka maktaba ya KAPIPIJhabari.COM:-Bw.Ghulam Dewij akiwa anapokea taji la maua kutoka kwa binti yake kama pongezi ya kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa ya Tabora.
Kutoka maktaba ya KAPIPIJhabari.COM:-Bw.Ghulam wakikumbatiana na diwani wa kata ya Gongoni ambaye pia ni mkurugenzi wa Kampuni la Usafirishaji la NBS LTD mara baada ya kuteuliwa na CCM kuwania nafasi ya Meya wa manispaa wakati huo.


LICHA ya kuwepo kwa vijimambo vilivyodumu kwa siku kadhaa ambavyo naweza kusema visivyo na miguu wala kichwa,Mbele wala nyuma,Chini wala juu ambavyo havikuwa na mashiko ya aina yoyote na wala haviingii akilini kwa mtu mwenye akili iliyosalama,Sana sana vilizidi kuwatia Presha waliovianzisha na baadaye kupatikana wengine kuvikumbatia licha ya kuwa mara kadhaa akili zilipowarudia walijikuta wakifikiria huenda wakawa na mapungufu makubwa kichwani.  

Niliendelea kujiuliza wakati wote nilipokuwa nikiyasikia hayo waliyokuwa wakimzushia Bw.Ghulam,na nilipojaribu kuyafuatialia kwa karibu zaidi nikagundua ni chuki zisizo kuwa na maana yoyote ile kwani pamoja na kuwasikiliza hao waliokuwa wakipita wakiyasema  ndio walikuwa  vinara wakubwa wa majungu hayo, na karibu wakati wote hawakuwa na ushahidi kwa yale wanayoropoka

Sina nia mbaya lakini itabidi mnifikirie wenyewe kunisamehe hata kama sijawaomba msamaha kwani sina muda wa kufanya hivyo pale ninapogundua kuwa kuna ukweli kwa yale ambayo mnayazusha halafu mkitakiwa kutoa ushahidi mnakosa majibu,kwakweli nathubutu kusema ACHENI UNAFIKI,mwacheni kijana wa watu afanye kazi aliyotumwa na wananchi msiendekeze maslahi yenu binafsi. 

Ghulam Dewij nakubali kuwa ni kiongozi ambaye bado nyota yake inazidi kung'ara ndani na nje ya CCM,....Hebu jaribu kufanya mahesabu wewe mwenyewe, Ghulam mbali na kushika nafasi mbalimbali katika Chama chake ambazo alionekana kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kile kinachodaiwa kukisaidia chama katika kuimarisha masuala kadhaa ya kimsingi lakini pia amekuwa mstari wa mbele na kuwa karibu zaidi na wanachama wenzake pasipo kubagua kiongozi au mpiga debe wa chama,kwake yeye wote walikuwa ni muhimu.

Hili ndio linadhihirisha kuwa Ghulam ni kiongozi aliyekuwa akikubalika na wadau wote wa ndani ya chama nikiachilia mbali hao walioko nje ya chama ambao Ghulam ameonekana mara kadhaa akishiriki shughuli za kijamii huko mitaani kama shida za maafa na furaha za harusi na mengineyo.

Alipochaguliwa kama diwani wa Kanyenye hii ilikuwa ni mara ya pili kwa wadhifa wa aina hiyo kwa kata tofauti,nikimaanisha kote huko alikuwa anakubalika Kata ya Mbugani na Kanyenye.

Sasa akachaguliwa kuwa Meya wa manispaa ya Tabora na kuanza kuonesha uwezo wake katika kuyatekeleza yale aliyotumwa na wananchi na hatimaye hata heshima na hadhi ya manispaa yetu imeanza kurudi,....Hili likawa mwiba kwa wale waliotaka kumuendesha vile wanavyotaka wao na tena ni kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo Ghulam Dewij aliliona si haki kwa kufanya hivyo kwa wajanja wachache ambao sasa walimgeuka na kuanza kutengeneza hayo ambayo yaliwaingia vichwani mwao na kumzushia kila aina ya ubaya....na mbaya zaidi eti wakadiriki hata kuandaa mpango wa kumuondoa katika wadhifa wa Meya wa Manispaa.

Ni mengi niliyonayo ukiachilia mbali na lile la  kutaka kumchonganisha na mkuu wa mkoa wa Tabora ilimradi aonekane kuwa hafai.....Jamani Jamani!!!!hivi kama hafai ni nani ambaye angefaa....Acheni UZUSHI.

Hivi kama angekuwa Ghulam ni mbaya kiasi hicho mnacho mzushia angeweza kuaminiwa na wengine kama ilivyo sasa hata kufikia hatua jina lake limekwenda Dodoma na kurudi Tabora kisha wajumbe wenye akili timamu wa Jumuiya ya Wazazi wakamchagua kwa wingi wa kura hizo alizopangiwa na Mwenyezi Mungu kuzipata kuwa Mwenyekiti wao!....AMA KWA HAKIKA ALIYEANDIKIWA YES NI YES TU HAKUNA KINGINE.............Ndugu zangu hebu Tabora mjini tubadilike anayeonesha uwezo wake katika kutenda jambo zuri kwa manufaa yetu sote tujaribu kumsapoti tutaona manufaa yake kwa muda mfupi na sio kumtafutia dhahama na kumpaka matope bure,sio uungwana huo.              

   

No comments: