Na Juma Kapipi,Tabora.
Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili mkazi wa kata ya Kiloleni mjini Tabora aliyefahamika kwa jina la Ashura Salumu amefariki dunia baada ya kuungua moto wakati akiwa amelala kitandani majira ya saa tano usiku .
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambao ni majirani katika kata hiyo ya Kiloleni eneo jirani na Soko la Ghana wameuambia mtandao huu kuwa,majira ya usiku huo walisikia kelele za mayowe yaliyokuwa yakipigwa na mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Amina Juma(29)ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo ambaye ni kwa sasa ni marehemu.
"Sisi tukiwa hapa mtaani kwetu tulianza kusikia kelele za mama huyo akidai kutaka kusadiwa kuwa mtoto wake anaungua moto ndani ya nyumba aliyokuwa akiishi,ndio tukatoka na kwenda kujaribu kusaidia"alisema mmoja wa mashuhuda hao Tabu Ramadhani.
Wakiwa katika harakati za kutaka kuokoa maisha ya mtoto huyo,mmoja kati ya wasamalia wema ambao waliamua kuvunja dirisha baada ya kuona hakuna uwezekano wa kupitia mlangoni,..''Niliamua kujitosa ndani na kumkuta mtoto huyo akiwa ameanguka kutoka kitandani ambapo godoro na chandarua vilikuwa vimeshika moto,nikamchukua mtoto akiwa mahututi mpaka nje"alisema mmoja wa vijana walioingia ndani kujaribu kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Hata hivyo walimkimbiza hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete ambako mara baada ya kumfikisha mtoto huyo kwa kutumia usafiri wa pikipiki alipoteza maisha kabla ya kuanza kupata huduma.
Mama wa marehemu amekaririwa na mtandao huu akidai kuwa alimwacha mtoto wake huyo(Ashura Salum)akiwa amelala kitandani na alikuwa amemfunika kwa chandarua ikiwa ni hatua ya kumkinga na malaria,...Chandarua na godoro viliangukiwa na kibatari kilichokuwa kikisaidia kutoa mwanga ndani ya chumba hicho,ambapo inadaiwa kuwa ndio chanzo cha tukio hilo lililosababisha mauaji ya mtoto huyo.

No comments:
Post a Comment