Pages

KAPIPI TV

Saturday, October 13, 2012

MTOTO ALIYEUNGUA MOTO ANAHITAJI MSAADA WA MATIBABU - 0752 635 504

Mtoto Jackson Festo (miezi 4)akiwa na mama yake mzazi Anna Charles.


Mtoto Jackson Festo mwenye umri wa miezi minne anahitaji msaada wa matibabu kufuatia majeraha aliyoyapata kutokana na ajali ya moto.

Akizungumza na mtandao huu mama mzazi wa mtoto huyo Anna Charles alisema mtoto wake alipatikana na masahibu hayo ya moto uliozuka ndani ya chumba alichokuwa amelala majira ya usiku wa saa mbili nyumbani kwao huko katika kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.

Hata hivyo alipotakiwa kuelezea chanzo cha moto huo Anna hakuweza kuweka bayana kutokana na kuwa yeye alikuwa katika mihangaiko ya maisha yaani kibaruani kwake.

"JAMANI NAWAOMBENI WASAMALIA WEMA MNISAIDIE NIKAMTIBU MWANANGU,SINA UWEZO WA KUKABILIANA NA HALI HII"Alisema Anna huku akitokwa na machozi kuashilia uchungu alionao kutokana na masahibu ya mwanae.

Kwa mujibu wa maelezo ya Anna,mtoto huyo baada ya kupata matibabu katika hospitali ya mkoa wa Tabora Kitete inahitajika apelekwe katika hospitali nyingine zenye wataalamu waliobobea ili aendelee na matibabu ya kina baada ya kushindwa kwa madaktari wa hospitali ya Kitete.

Kwakuwa kila kimfaacho mtu ni chake Anna tayari amemaliza vitu mbalimbali vya nyumbani zikiwemo nguo zake za kuvaa kwa kuuza ili apate angalau  fedha za matibabu na za kujikimu kimaisha. 

IKIWA UTAGUSWA NA KUTAKA KUMSAIDIA MTOTO HUYU WASILIANA NA MAMA MZAZI ANNA CHARLES KWA NAMBA HII...0752 635 504

No comments: