Dkt.
Parseko Kone akizungumza na wananchi wa kata ya Nkonko jimbo la Manyoni
Mashariki wakati akihimiza utunzaji wa barabara pamoja na kuongeza
uzalishaji wa mazao ili waweze kutumia barabara kuyafikisha mazao hayo
kwenye masoko ya uhakika.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone (wa kwanza kushoto) akielekeza
jambo wakati akikagua barabara ya Chikuyu hadi kijiji cha Sanza wilayani
Manyoni.Wa kwanza kulia ni Meneja wa TANROADS mkoa wa Singida Mhandisi
Yustaki Kangole akimsikiliza kwa makini mkuu wa mkoa. Wa pili kushoto ni
mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki John Chiligati.
Meneja
wa TANROADS mkoa wa Singida Yustaki Kangole (wa kwanza kulia), akitoa
maelezo kwa mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone (wa pili kulia)
wakati mkuu huyo wa mkoa akikagua barabara ya Chikuyu hadi kijiji cha
Sanza inayojengwa kwa kiwango cha changarawe.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone ( wa pili kulia aliyenyoosha
mkono) akielezea jambo wakati akikagua barabara ya Chikuyu hadi kijiji
cha Sanza inayojengwa kwa kiwango cha changarawe. Wa kwanza kulia ni
meneja wa TANROADS mkoa wa Singida mhandisi Yustaki Kangole.
Sehemu
ya barabara ya kutoka kijiji cha Chikuyu hadi kijiji cha Sanza jimbo la
Manyoni Mashariki inayojengwa kwa kiwango cha changarawe.
(Picha zote
na Nathaniel Limu).
No comments:
Post a Comment