Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini LHRC Dr.Helen Kijo-Bisimba akizungumza katika mdahalo wa kupinga adhabu ya kifo duniani uliofanyika leo jijini Dar-es-Salaam.
Mwalusanya
Choir: Kwaya ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ilikuwa na wimbo
maalumu wa kuhimiza kufutwa kwa Adhabu ya Kifo Tanzania
Na Rodrick Maro,Dar-es-Salaam
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini LHRC leo kimeungana na wanaharakati mbalimbali kupinga adhabu ya kifo duniani katika kuadhimisha siku hiyo jijini Dar-es-Salaam.
Katika Maadhimisho hayo yalifanyika kwa kuwa na mdahalo wa kusisimua na kutolewa kwa ushuhuda wa
mmoja wa waathirika wa adhabu ya kifo, aliyeponea tundu la sindano
kunyongwa huku akiwa amekaa gerezani kwa zaidi ya miaka 18 kwa kosa ambalo linalodaiwa kuwa
hakulitenda!
Baadhi ya wadau wengine waliohudhuria maadhimisho hayo ni pamoja na Ubalozi wa Uingereza, mashirika rafiki, wanavyuo wa vyuo vya elimu
ya juu, wanafunzi wa sekondari (Kibasila), wanahabari na wananchi wa jiji la Dar-es-salaam.
No comments:
Post a Comment