Kwa mujibu wa waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia matamko yaliyokuwa yakitolewa na baadhi ya waislam kuhusu dhamira ya kufanya maandamano kuelekea Ikulu kushinikiza kuachiwa huru kwa mmoja wa viongozi wa dini ya kiislam Sheikh Ponda aliyekamatwa kwa makosa ya uchochezi, watu hao walifika mmoja mmoja kabla ya kudhibitiwa na Askari wa
Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati.
Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es
Salaam kutoa amri ya kuzuia maandamano hayo yanayodaiwa kuwa si halali kwa madai ya kutokuwa na kibali cha kufanya hivyo.
Hata hivyo licha ya baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu kuwataka waumini wao kuwa na subira katika suala hilo lakini bado baadhi yao wamepingana na amri za viongozi wao na kuanza kuafanya maandamano hayo yasiyo halali
No comments:
Post a Comment