Pages

KAPIPI TV

Friday, September 21, 2012

UVCCM URAMBO WATISHIA KUHAMA CHAMA"Wamtuhumu Mbunge Sitta kwa kuwagawa"

Baadhi ya viongozi wa ngazi za kata jumuiya ya umoja wa vijana CCM wilayani Urambo wakiwa wamevamia Ofisi za CCM Mkoa wa Tabora kwa madai ya kukithiri kwa vitendo vya rushwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa nafasi za uongozi ngazi ya wilaya  katika jumuiya hiyo,ambapo imedaiwa kuwa baadhi ya vigogo wanatumia fedha na nafasi walizonazo kupanga safu za uongozi katika jumuiya hiyo ya Umoja wa vijana.

Vijana hao ambao wametinga katika ofisi za CCM Mkoa wamesema kwa dhuruma zinazoendelea kufanywa na vigogo hao wilayani Urambo ni vema Uongozi ngazi za juu za Chama hicho uingilie kati vinginevyo wapo tayari kurudisha kadi za CCM.

"Haiwezekani Chama kiwe ni cha mtu mmoja au cha familia fulani ni bora turudishe kadi kuliko kuwa na Chama kilichogubikwa na watu wenye kulenga maslahi yao binafsi"alisema mmoja wa kiongozi katika kundi la vijana hao.  

No comments: