Pages

KAPIPI TV

Thursday, September 6, 2012

UTPC YATOA TAMKO MAUAJI YA DAUDI MWANGOSI

Wajumbe wa Mkutano Mkuu UTPC wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumuombea Marehemu Daudi Mwangosi aliefariki katika Vurugu za Chadema na Polisi mkoani Iringa

UMOJA wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umesema kuwakufuatia mauaji ya  mwandishi wa habari wa Wa kituo cha Channel Ten Mkoani Iringa Bw. Daudi Mwangosi kimeitaka serikali kuwasimamisha kazi askari waliohusika katika tukio la mauaji ya kinyama ya mwandishi huyo. Umoja huo umesema kuwa askari walioshiriki katika oparesheni hiyo ambayo ni haramu kusimamishwa mara moja ili kupisha uchunguzi kufanyika.

Hayo yalisemwa jana Jijini Dar Es Salaam na Rais wa UTPC Bw.Keneth Simbaya wakati alipokuwa akitoa tamko Kwa Viongozi wa Vilabu Mikoani kuhusiana na mauaji dhidi ya mwandishi wa habari Huyo aliyeuwawa akiwa mikononi mwa polisi katika kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi. “Hapa tunataka uchunguzi huu ukikamilika tunaitaka serikali kuutangazia umma na kupisha sheria kwa wale watakaobainika kuhusikakwa uzembe huo kwa namna moja au nyingine wachukuliwe hatua dhidi ya mauaji hayo ya mwandishi wa habari Bw. Daudi Mwangosi”alisema.
Hata hivyo Bw. Simbaya alisema wakati uchunguzi ukiwa unaendelea serikali iridhie na kurasimisha malipo kwa ajili ya Mjane wa mwandishi huyo na watoto walioachwa na marehemu ili waweze kujikimu.

Aidha alisema licha ya kutoa tamko hilo wanaendelea kulitazamia jeshi la polisi kama mdau mwenye shaka kwa namna wanavyotenda kazi zao na waandishi wa habari mikoani na kwamba watataarifu umma kuhusu
mwenendo wao hapo baadae. “Lakini pia katika mkutano huu tumeridhia kushirikiana na taasisi zingine za haki za binadamu ,uwakili na Utetezi ili kubaini namna bora ya kuishitaki serikali kama mwenendo wa suala hili hautakuwa unaleta tija Kutokana na vithibitisho hivyo tunakaribisha mashirika ya haki za binadamu ,asasi zisizokuwa za kiserikali ili kuweza kufanikisha azma hii”alisema Bw. Simbaya.
Akizungumzia kuhusu usalama kwa waandishi wa habari Bw. Simbaya alisema katika kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi yao kwa usalama amelitaka jeshi la polisi kutoa utaratibu ambao utawezesha wanahabari nchini kufanya kazi kwa usalama bila hofu wala dharau,kutoa elimu kwa jeshi la polisi kuhusu umuhimu wa wanahabari na jukumu lao katika Taifa.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa Vyama vya waandishi wa habari Tanzania ambao wanahudhulio mkutano mkuu wa UTPC walisema tamko hilo halijapewa uzito kutokana na tukio la mauaji lenyewe na jinsi lilivyo huku wakitaka Tamko hilo kupewa uzito wa kina. “Hili Tamko lilitakiwa kupewa uzito sana kwani sisi tuliokuwepo katika msiba huo kwa ujumla inasikitisha sana hivyo tamko ni muhimu lipewe uzito zaidi kulingana na mauaji yenyewe yanavyotisha hivyo tufuate maamuzi ya viongozi wa clabu waliotoa matamko ya kususia habari za polisi mpaka pale watakapokuwa wameridhia kukaa meza moja na wanahabari juu ya mauaji hayo”alisema mmoja wa viongozi wa clabu za waandishi wa habari Tanzania Bw. Christopher Nyenyembe.

                 Habari na Esther Macha Na Mwajabu Kigaza

No comments: