Mkuu
wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi akizungumza na wananchi wa
kata ya Utemini manispaa ya Singida ahamasisha maadili mema kwa
watoto.
(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu
Baadhi
ya ya wakazi wa manispaa ya Singida wamelalamikia mavazi yanayovaliwa
na wanafunzi wa vyuo vya uhazili na uhasibu, kwa madai kwamba
yanachangia kuharibu maadili ya watoto wao.
Malalamiko
hayo yametolewa na wakazi hao kwenye viwanja vya shule ya sekondari ya
Utemini mjini Singida katika mkutano ulioitishwa kwa ajili ya mkuu wa
wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi kuhamasisha ujenzi wa maabara
katika shule za sekondari za kata.
Wakifafanua,
wamesema wanafunzi wa vyuo hivyo na hsasa wa kike, wanavaa nguo ambazo
ni kinyume na maadili ya kitanzania na zinachochea vitendo vya ngono
zembe.
“Mheshimiwa
mkuu wa wilaya, nguo zinazovaliwa na hawa wanafunzi wa kike, zinaacha
nusu ya mwili ubaki kama alivyozaliwa na mbaya zaidi zinawabana
kupindukia, na Kwa upande wa wanafunzi wa kiume, wao suruali zao
wanazivaa chini kabisa ya makalio” almeema Ntandu Jumbe.
Wamesema
uvaaji wa nguo unaofanywa na wanafunzi wa vyuo hivyo, unachochea kasi
ya mmomonyoko wa maadili kwa vijana na atoto wao kuongezeka mara dufu.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya Queen Mlozi amesema tatizo hilo na yeye
amelibaini lakini hata hivyo, akadai kuwa hayo ni matunda ya utandawazi.
Amesema
tatizo la kuharibika kwa watoto kwa maana ya kutokuwa na maadili mema
ni la karibu kila familia na hivi sasa ni kubwa mno.
Queen
Mlozi amesema kwa kweli dawa pekee hivi sasa ya kupambana na janga hili
la watoto kuharibika, ni sisi sote wazazi, walezi, viongozi wa serikali
na wa madhehebu ya dini, kuunganisha nguvu zetu pamoja na kuimba wimbo
mmoja, nao ni wa malezi bora kwa watoto wetu.
Aidha,
mkuu huyo wa wilaya ameagiza kwamba kuanzia sasa kila vikao vya maamuzi
vya ngazi mbalimbali, ajenda yao kuu iwe ni mkakati wa kudhibiti kasi
ya mmomonyoko wa maadili kwa watoto.
No comments:
Post a Comment