Mkuu
wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, akizungumza na wananchi wa
kata ya Utemini manispaa ya Singida akihamasisha ujenzi wa maabara
katika shule za sekondari za kata na kujitambulisha.
Diwani
wa kata ya Utemini CCM jimbo la Singida mjini Baltazar Kimario,
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya
shule ya sekondari kata ta Utemini. Mkutano huo ulitumika kwa Mkuu wa
Wilaya Mlozi kuhamasisha ujenzi wa maabara.
Baadhi
wa wakazi wa Utemini mjini Singida waliohudhuria mkutano wa hadhara
ulioitishwa kwa ajili ya mkuu wa wilaya ya Singida Queen Mlozi, kuhimiza
ujenzi wa maabara.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi (wa kwanza kushoto) akishiriki
kutoa burudani na kikundi cha uhamasishaji cha nyota njema cha Utemini,
kwenye mkutano wa hadhara.(Picha na Nathaniel Limu).
Serikali
ya wilaya ya Singida imewaagiza wakazi wa manispaa ya Singida,
kuunganisha nguvu zao pamoja kuchangia ujenzi wa maabara katika shule
zote za sekondari za kata.
Kasi
na nguvu zilizotumika kujenga shule za sekondari za kata, zimetakiwa
ziongezeke zaidi ili ifikapo oktoba 20 mwaka huu, majengo ya maabara
yawe yamefikia katika hatua nzuri ya kupauliwa.
Agizo
hilo limetolewa na mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi,
wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Utemini jimbo la Singida mjini.
Amesema suala la ujenzi wa maabara ni muhimu mno katika wakati huu wa dunia ya sayansi na teknolojia.
Mlozi
amesema wazazi na walezi ni lazima watambue hilo, ili waweze kushiriki
kikamilifu katika ujenzi wa maabara mahali watoto wao, watajifunza kwa
vitendo masuala ya sayansi.






No comments:
Post a Comment