Afisa Mawasiliano wa
Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa mmoja wa
wananchi walio telea Banda hilo leo.
Maonesho ya kimataifa
ya biashara Dar es Salaam (DITF) maarufu kama Saba saba yameanza Juni
28, 2012 katika viwanja vya Maonesho vya JK Nyerere barabara ya Kilwa
jijini Dar es Salaam.
Wafanyabiashara wa ndani
na nje ya Tanzania wanashiriki maonesho hayo makubwa Tanzania, huku
serikali na taasisi zake nyingi zikiwa moja ya washiri katika maonesho
hayo yanayoratibiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzanaia.
Pia
taasisi za Kimataifa na mashirika makubwa duniani yanashiriki maonesho
hayo, miongoni mwa mashirika hayo ni Umoja wa Mataifa ambao upon a
taasisi zake zote zaidi ya 21. UN Tanzania wapo katika Banda la
Ali Hassan Mwinyi na elimu mbalimbali juu ya Umoja huo wa Mataifa ambao
Tanzania ni mwanachama wake unapatikana.
Afisa habari wa Shirika
la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Austin Makani akiwa
na Afisa Habari wa Umoja wa Umoja wa Mataifa (UN) Hoyce Temu.
Mjasiriamali, Bi
Magreth Msuya kutoka Kikundi cha MATA Woman Group cha Tabata jijini Dar
es salaam ni moja ya watu wanaofaidika na UN, na hapa anashiriki
maonesayo ndani ya Banda la UN. Kulia ni mteja anaeangalia bidhaa zake
na kto ni Afisa Habari wa UN Tanzania, Hoyce Temu.
Afisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu akitoa maelezo kwa wananchi walio telea Banda hilo leo.
Banda la umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment