Pages

KAPIPI TV

Tuesday, July 24, 2012

TANESCO TABORA WAANZA OPERESHENI YA KUWASAKA WANAOIBA UMEME"Wanusurika kipigo,Wakamata watano hadi sasa,Wapata hasara ya zaidi ya shilingi mil.1"

 Baadhi ya maafisa wa shirika la umeme Tanesco Tabora wakiendelea na ukaguzi wa wizi wa umeme unaofanywa na baadhi ya wateja wa shirika hilo,hapa ni moja ya nyumba iliyoko maeneo ya Bachu Ground mjini humo ambayo inadaiwa kuwa hujuma dhidi ya Tanesco inafanywa.
 Mmoja kati ya wateja wa Tanesco katika nyumba hiyo anayedaiwa kukutwa akifanya hujuma dhidi ya Tanesco,lakini mteja huyo ambaye ametambulika kwa jina la Mansoor alikana kuhusika na uharifu huo.
 Hili ni eneo la Mita ya umeme wa Luku ambayo imefanyiwa hujuma hizo kwa kuunganisha njia ya moja kwa moja ambayo mita haiwezi kusoma matumizi sahihi ya nyumba hiyo.
 Baadhi ya Askari Polisi walilazimika kufika eneo hilo la Bachu kuzuia vurugu ambayo ingeweza kutokea baada ya maafisa wa Tanesco kutaka kuondoa kabisa huduma ya umeme katika nyumba hiyo huku mwenye nyumba akiwa hataki kuondolewa kwa huduma hiyo.
 Hatimaye kwa kutumia dhana ya Polisi jamii ili kutekeleza Utii wa Sheria bila Shuruti,Maafisa hao wa Polisi walifanikiwa kumchukua Bw.Mansoor na kumpeleka kituo kikkubwa cha Polisi Tabora.
 Baadaye mafundi wa umeme Tanesco walipata mwanya wa kukata huduma ya umeme kwa Bw.Masoor baada ya kuzuia kwa muda mrefu huku akiwatishia kupigana endapo wataondoa huduma hiyo.
Askari Polisi walilazimika kusimamia zoezi la ukataji umeme wakati Bw.Mansoor akiwa tayari amewekwa ndani.

No comments: