NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS wa Liberia,
Ellen John-son Sirleaf amewataka
viongozi wa nchi za Afrika kufanya
jitihada za kuhakikisha wanatenga rasilimali za kutosha za kuweza kupambana na ugonjwa wa Malaria ili ifikapo
mwaka 2015 Bara la Afrika lifanikiwe kutokomeza ugonjwa huo kwa asilimia sifuri.
Kauli hiyo
ilitolewa leo na Rais huyo
wakati wa sherehe za uzinduzi wa Ofisi
za Umoja wa Viongozi wa Afrika wa Kudhibiti Malaria(ALMA) iliyopo katika
Kituo cha Mkakati wa Kupambana na Malaria(Ceemi), jijini Dares Salaam.
Alisema lengo
kubwa la ALMA ni kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2015 Bara la Afrika
linaondokana na ugonjwa huo ikiwemo vifo vinavyosababishwa na Malaria .
“Tunaweza kufanya hivyo ili tuweza kufanya tunatakiwa kuchukua hatua za kuwa na rasilimali za kutosha na kuzitawanya katika vituo vya afya kama ilivyo katika azimio letu la Abuja.” Alisema Rais Hellen.
Aliongeza kuwa jitihada hizo zitafanikiwa kwa kuboresha usimamizi
bora wa mfumo wa fedha ili kuweza kukabiliana na tatizo la
uhaba wa fedha kiasi cha dola za
Marekani bilioni 3.2 .
“ Tunatakiwa kuboresha mifumo yetu ya fedha ili kuwezesha upatikanaji wa
vifaa vya kupambana na ugonjwa wa Malaria mfano dawa na utoaji wa vyandarua bure, utafiti na kuwa
wabunifu wa kutafuta njia za kukabiliana na uhaba wa fedha ili tuweze kutimiza
lengo la kuwa na asilimia zero ya Malaria ifikapo mwaka 2015. ” alisisitiza.
Rais huyo,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa ALMA alisema baadhi ya nchi zimefanikiwa kutimiza
lengo hilo la Abuja, ambazo ni Msumbiji, Togo na Rwanda.
Aliongeza kuwa
bara hilo limefanikiwa kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo kwa
asilimia 33 katika kipindi cha miaka 10 iliyopita alisema.
Kwa upande
wake Rais Jakaya Kikwete alisema bara hilo, linaongoza kwa vifo
vinavyotokana na ugonjwa huo kwa asilimia
89 na kuwa na wagonjwa kwa asilimia 83.
“Tukikusanya
nguvu za pamoja naamini tunaweza
kufanikiwa. Tumeaanza vizuri nguvu za pamoja zitatuwezesha kufatuta vifaa
pamoja ili kila nchi viweze kupelekwa.
Alisema kupitia
ALMA wamefanikiwa kutoa vyandarua bure
milioni 400.
Wakati huo
huo Rais Kikwete alisema Tanzania itaendelea kutoa ushirikiano na ALMA ili kufikisha
malengo ya kupambana na ugonjwa huo.
Katibu
Mtendaji wa ALMA, Joe Pumaphi alisema dola za Marekani bilioni 12 hutumika kila
mwaka katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Huku akihoji ni kwanini fedha hizo
ziendelee kutumika.
Aidha Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, DK. Hussein Mwinyi alisema nchini Tanzania ugonjwa huo bado unaongoza
kwa kusababisha vifo vya mama wajawazito na watoto. Hivyo kesi zinazoripotiwa ni za watu milioni
12 na vifo watu 60,000 hadi 80,000 kwa mwaka.
Alisema Tanzania
imefanikiwa kutokomeza ugonjwa huo kwa asilimia 50 kwa utoaji wa vyandarua vilivyo na dawa bure kwa watoto
walio na umri wa chini ya miaka mitano milioni tisa na kaya milioni 17.6.
Alisema changamoto
iliyopo ni kuwa na uwezo wa kununua dawa na vyandarua kwa kutumia fedha za
ndani.
No comments:
Post a Comment