Pages

KAPIPI TV

Wednesday, July 25, 2012

MVP YATOA MSAADA WA VITABU KWA SHULE ZA MSINGI VIJIJINI VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI.12

 Kiongozi wa mradi wa vijiji vya Milenia Mbola Dr.Gerson Nyadzi akiwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ilolangulu muda mfupi mara baada ya kukabidhi msaada wa  vitabu vya kiada na ziada.
 Kiongozi wa mradi wa vijiji vya milenia Mbola Dr.Gerson Nyadzi,alivaa suti nyeusi ni Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Uyui Bw.Said Ntahondi akiangalia vitabu vilivyotolewa msaada na mradi Mvp kwa shule za msingi zipatazo 17 zilizoko katika eneo la vijiji vya Milenia Mbola.
 Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Uyui Bw.Ntahondi,pamoja na maafisa wa Mvp na wadau mabalimbali wa elimu wakiwa katika moja ya vyumba vya kompyuta vinavyotumika kufundishia wanafunzi katika shule ya msingi ya Ilolangulu. 
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ilolangulu wakiimba nyimbo wakati wa hafla fupi ya upokeaji wa msaada wa vitabu vilivyotolewa kwa shule 17 zilizopo eneo la mradi wa vijiji vya Milenia mbola.
Picha ya pamoja mara baada ya kupokea msaada wa vitabu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi mil 12 vilivyotolewa na mradi wa Mvp.

Na Juma Kapipi-Tabora
Mradi wa vijiji vya Milenia Mbola Mvp umetoa msaada wa vitabu  vipatavyo 1500 kwa shule za msingi 17 vyenye thamani ya kiasi cha shilingi Mil.12,266,000/=.

Akikabidhi msaada huo kwa Shule ya msingi Ilolangulu iliyopo kata na Tarafa ya Ilolangulu wilayani Uyui mkoani Tabora,Kiongozi na mratibu wa Mradi huo Dr.Gerson Nyadzi alisema lengo la kutoa msaada huo ni kutekeleza moja ya malengo manane ya Milenia katika kuboresha elimu.

Aidha Dr.Nyadzi alisema baada ya kufanikiwa kuboresha maeneo mbalimbali katika kusaidia sekta hiyo ya elimu kwa kujenga miundo mbinu yakiwemo madarasa,kupanua wigo kwa kuanzisha masomo ya kompyuta  na  mpango wa chakula shuleni kwa wanafunzi,hatua iliyofuata ni kutatua changamoto hiyo ya upungufu wa vitabu vya ziada na kiada kwa shule za msingi zilizopo eneo la mradi wa vijiji vya Milenia Mbola.

Akipokea msaada huo diwani wa kata ya Ilolangulu ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya  ya Uyui Bw.Said Ntahondi pamoja na kuwataka walimu katika shule hizo 17 kuvitunza vitabu hivyo ili viweze kutumika na kuleta manufaa kwa wanafunzi waliopo sasa na wa baadaye.

Kwaupande wake mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi Ilolangulu Bw.Salum Kusaye pamoja na kuupongeza mradi kwa kutoa msaada huo lakini pia alizungumzia changamoto ya ukosefu wa vitabu kwa shule yake ambapo aliweka bayana kuwa wastani wa wanafunzi wapatao 35 wanalazimika kutumia kitabu kimoja na hivyo kuifanya kazi ya ufundishaji kuwa ngumu.

"Kwakweli hili limekuwa ni tatizo kubwa na tumelipigia kelele sana lakini hakuna mafanikio,yaani inafikia wakati mwingine tunakosa hata chaki inabidi mimi kama mwalimu mkuu naanza kuingia madeni kwa kukopa madukani ilimradi wanafunzi wasome"alisema mwalimu mkuu huyo huku akidai kuwa hata hiyo fedha anayoitoa kwa ajili ya kununua vifaa vya shule huwa harudishiwi.

Aidha Mradi wa milenia Mbola umekuwa ukitoa misaada mbalimbali kwa shule hizo ambapo mafanikio kwasasa yameanza kuonekana kwa kuwepo kwa ongezeko la ufaulu kwa wanafunzi licha ya kuwepo kwa  changamoto hiyo.   

No comments: