Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
. ZAIDI ya wafuasi 40 wa kikundi cha Jumuiya ya Uamsho
Zanzibr wamekamatwa na Polisi kufuatia vurugu zilizotokea jana kwenye
eneo la Darajani mjini Zanzibar.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa
watuhumiwa hao walikamatwa baada ya kufunga barabara kadhaa kwa mawe,
vyuma, matofari na kuchoma moto matairi ya magari.
Kamanda Aziz amesema
kuwa katika vuurugu hizo hakuna Askari ama watuasi wa kikundi hicho
waliofariki ama kujeruhiwa wakati wa ghasia hizo zilizokuwa nimeendelea
katika mitaa mbalimbali ya mji wa Zanzibar.
Amesema wafuasi hao
walitumia mawe, chupa na vipande vya mbao kuwarushia Polisi lakini
amesema hadi kumalizika kwa zoezi la kuwatawanya wafuasi hao saa nane
usiku wa kuamkia leo,
Hata hivyo Kamanda
Aziz amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwasaka viongozi wa
kikundi hicho ambao wametoroka mara baada ya kuibuka kwa vurugu hizo.
Amesema vurugu hizo
ambazo zilianza jana majira ya saa 11.00 jioni, zilidumu hadi saa 8.00
usiku kufuatia wafuasi wa kikundi hicho kujikusanya katika maeneo
mbalimbali wakifanya vurugu.
“Tunawatafuta
viongozi wa kikundi hicho na tunawataka popote walipo wajitokeze na
kujisalimisha wenyewe Polisi.” Alisema Kamanda Aziz.
Mara baada ya kuanza
kwa ghasia hizo na hadi asubuhi ya leo (jana) barabara za Darajani na
mlandege, mitaa iliyokuwa na mikusanyiko mikubwa ya watu, ilikuwa haia
hata mtu mmoja na hata biashara zilisimama.
Hata hivyo biashara
mbalimbali zimerudia tena katika hali yake ya kawaida huku watumishi wa
Baraza la Manispaa ya mji wakiendelea na kazi ya uongoaji wa mawe,
matofari na mabaki ya majivu ya matairi ya magari.
Ametoa wito kwa
wananchi kutoa taarifa Polisi endapo watawaona ama kubaini mahala
walipojificha viongozi wa kundi hilo la uamsho ili wahojiwe kwa tuhuma
za kuanzisha ghasia.
No comments:
Post a Comment