Kufuatia Tangazo la Chama cha Madaktari
nchini (MAT) la kuanza mgomo siku ya Jumamosi tarehe 23 Juni, 2012,
Mahakama Kuu ya Tanzania,Kitengo cha kazi,Dar es Salaam imetoa amri ya
kusitisha mgomo huo mpaka hapo pande zote mbili yaani Serikali na Chama
cha Madaktari Tanzania (MAT) yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Amri
hiyo ya Mahakama imetolewa kufuatia maombi namba 73 ya 2012
yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).Sababu za msingi
amabazo zimepelekea Mahakama kuu kutoa amri hiyo upande mmoja ni pamoja
na;
Iwapo
mgomo huo utatokea utakuwa na kuwa amri hii isipotolewa madhara yake ni
makubwa isiyoweza kufidiwa kwa namna yoyote ile kama vile kupoteza
maisha n.k
Wajibu maombi,ambao ni MAT, inaundwa na Madaktari ambao wapo katika
Sekta ambayo inatoa huduma mahsusi (essential service sector), Aidha
Chama cha Madaktari Tanzania kimetangaza mgomo bila kufuatia taratibu
zilizoanishwa katika Kifungu cha 76(1 na 2) cha Sheria ya Kazi
(Employment and Labour Relations Act No 6 ya 2004.
Masharti hayo ni
Kuzuia wafanyakazi walio katika Sekta Muhimu kugoma na kama wakigoma,
Kuwepona makubalianao ya pamoja ya kutoa huduma za msingi wakati mgomo ukiendelea.
Kwa misingi hii,Mahakama Kuu ya
Tanzania, kwa Chama cha Madktari Nchini na wanachama wake kusitisha na
kutoshiriki katika mgonmo huo.
No comments:
Post a Comment