Bw.Haruna Msoga mwenyekiti wa Talgwu mkoa wa Tabora. |
Baadhi ya watumishi wa halmashauri wakiwa nje ya ofisi zao za zamani baada ya kusitishwa kwa huduma ya usafiri |
Na Mwandishi wetu.
Watumishi wa halmashauri ya Tabora (UYUI)wamelalamikia hatua ya mwajiri wao kusitisha huduma ya usafiri ya kuwatoa Tabora mjini hadi makao makuu ya wilaya ya Uyui ambayo ipo eneo Isikizya kilometa 45 kutoka Tabora mjini.
Hatua ya watumishi hao kutoa lawama dhidi ya mwajiri ambaye ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo imekuja mara baada ya mkurugenzi huyo kutoa noties ya muda mfupi kusitisha huduma hiyo ya usafiri(Basi) ambayo kwa madai ya watumishi hao amekiuka haki za mtumishi.
Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa(TALGWU)mkoani Tabora Bw.Haruna Msoga amesema Talgwu imepinga vikali uamuzi wa mwajiri huyo na kusisitiza kuwa ni vipi mkurugenzi huyo aliweza kupanga bajeti ya usafiri kwa watumishi hao na iweje kwasasa kusitisha huduma hiyo na kibaya zaidi amefanya hivyo pasipo kufuata utaratibu.
Ingawa madai katika barua hiyo ambayo nakala yake hiyo hapo juu imeleeza sababu za kusitisha huduma ya usafiri huo ni baada ya kutokana na kikao cha baraza la madiwani kuketi na kujadili hali mbaya ya kifedha katika halmashauri hiyo,Bw.Msoga alisema mwajiri alipaswa kuzungumza kwanza na uongozi wa tawi la chama cha wafanyakazi wa halmasahuri hiyo kabla ya kutoa noties hiyo ambayo sasa imetafsirika kuwa ni kuwanyanyasa watumishi hao.
Hata hivyo hali hiyo ambayo imetokana na kuhama kwa ofisi za halmashauri hiyo kutoka Tabora mjini hadi Isikizya zaidi ya km 45 ambapo mtumishi ili aweze kufika kituo chake cha kazi anahitaji kuwa na kiasi cha shilingi elfu kumi na tano kila siku hali ambayo hailingani na mshahara wake kwa mwezi.
Watumishi hao chini ya Talgwu wameamua kwa pamoja hawatakwenda katika kituo chao cha kazi hadi siku ambayo mwajiri huyo atakapotoa huduma ya usafiri.
Kwaupande mwingine waananchi wa wilaya ya Uyui huenda wakakosa huduma kutoka kwenye halmashauri hiyo kwa muda usiojulikana hali ambayo imetokana na mvutano baina ya watumishi na mwajiri.
No comments:
Post a Comment