Pages

KAPIPI TV

Friday, May 4, 2012

WANAHABARI TABORA WASHEHEREKEA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI"Kuanzia tarehe 3 Mei hadi tarehe 19 Mei,watakutana na wadau pia"


LUCAS NDAGA :Mwandishi wa habari mwandamizi,mhariri na Mwanasheria wa kujitegemea akiwafunda waandishi wa habari wa mkoa wa Tabora katika siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani.
Baadhi ya waandishi wa habari wa Tabora katika kongamano la siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani
 JUMA KAPIPI:Mwandishi wa habari wa Channelten,Magic Fm,Wapo Fm,Tabora Television na KAPIPIJhabari.COM

Na Robert Kakwesi

WANAHABARI Mkoani Tabora wameahidi kutekeleza majukumu yao kwa kufuata Maadili ya Taaluma ya habari katika kutimiza wajibu wao.

Ahadi hiyo wameitoa katika mkutano miongoni mwao uliokuwa ukijadili majukumu yao katika Kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari Duniani.

Wakizungumza katika mkutano huo wanahabari hao kutoka Vyombo mbali mbali vya habari,wameeleza wapo baadhi waliokuwa wakitekeleza majukumu yao pasipo kufuata Maadili na hivyo kuitia doa taaluma ya Habari.

Wameeleza wote wasiofuata maadili ni lazima wajirekebishe ili kuipa  heshima Taaluma ya habari ambayo ni muhimu katika kuleta maendeleo Mkoani Tabora na nchini kwa ujumla.

Pia wana Habari habari wameahidi kuwa na ajenda katika habari zao kuwafanya  wananchi wa Mkoa wa Tabora kuelewa majukumu yao na wapi wanapopotoka kwa lengo la kuleta maendeleo Mkoani Tabora

No comments: