Na Habari Maelezo Zanzibar
Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi leo
wameshiriki katika kazi za usafishaji wa mji katika eneo la Forodhani
Mjini Zanzibar.
Utaratibu huo ni uzinduzi wa kazi za Usafi unaoongozwa na Baraza la
Manispaa hapa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya mikakati yake yakushajiisha
Wananchi juu ya Usafi katika sehemu za Mjini na Nyenginezo.
Akielezea juu ya uzinduzi wa Usafi huo, Mkurugenzi wa Baraza la
Manispaa Zanzibar Rashid Ali amesema kuwa Kazi hiyo ya usafi kwa
sehemu za Mjini na nyengineze itakuwa ikifanyika kila mwanzoni mwa
mwezi kwa siku ya Jumaamosi.
Amesema kuwa kazi hiyo itakuwa endelevu na sio ya zima moto na
Jumaamosi ijayo itakuwa kwa kila Nyumba ,Wadi na Shehia kufanya usafi
na wao watakuwa na Wajibu wakukusanya Taka hizo ili wazipeleke
kunakohusika kwa kuzitupa.
Aliendelea kusema kuwa Jumaamosi nyengine kazi hiyo itaendelea tena
hiyo ambapo watalazimika kufunga baadhi ya Nija kuanzia saa12
asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
Nae Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mwinyiussi Abdulla kwa niaba ya Waziri Dkt Mwinyihaji Makame
amesema kuwa Madhumunui ya Ofisi hiyo kuanzisha utaratibu huo
wakufanya usafi kila siku ya Jumaamosi ya wanzoni mwa mwezi ni
kuwashajiisha Wananchi kuona kuwa kazi hiyo si ya Baraza la Manispaa
tu bali ni ya kila mtu.
Alisema kuwa ni wajibu wa kila mtu pale alipo kuungana na Serikali
katika kazi hiyo ya kufanya usafi kwani ni kwa faida ya mtu mwenyewe
na Taifa kwa ujumla,
Katika uzinduzi huo Maofisa mbali mabli katika ofisi hiyo walishiriki
katika kazi za usafi wakiwamo Manaibu Makatibu Wakuu, Wakuu wa Wilaya,
Wakurugenzi, Masheha pamoja na Wafanyakazi kutoka Taasisi mbali mbali
ziliomo katika Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
No comments:
Post a Comment