Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati akizindua
rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, litakaloendelea kwa siku tatu Mkoani Iringa.
Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 8, 2012, katika Ukumbi wa Shule ya Msingi
Mtakatifu Dominic Savio, mkoani Iringa. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wa kumbukumbu katika eneo la
Shule ya Msingi Mtakatifu Dominic Savio, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la
Uchumi wa Kijani, Leo Mei 8, 2012, litakalofanyika kwa Siku tatu mkoani Iringa.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Msanii wa Muziki wa Asili na Mashahiri, Mrisho Mpoto,
akighani maneno yake yenye ujumbe Kuhusu Utunzaji wa Mazingira, mbele ya mgeni
rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib
Bilal, wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi wa Kijani, uliofanyika Mkoani
Iringa leo Mei 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
Taasisi ya Uongozi, baada ya kuzindua rasmi Jukwaa la Uchumi wa Kijani, mkoani
Iringa leo Mei 8, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR






No comments:
Post a Comment