Pages

KAPIPI TV

Thursday, May 10, 2012

AJALI MBAYA TENA TABORA"Ni basi la TRANSMISSION kutoka Kigoma-Tabora"

 Harakati za kuokoa maisha ya wasafiri waliokuwa wamebanwa katika basi hilo ambapo kampuni la Wachina la wajenzi wa barabara ya Ndono-Urambo lililazimika kufanya kazi hiyo ya uokoaji kwa kutumia vifaa mbalimbali.

 Baadhi ya majeruhi katika basi la Transmission  mara baada ya kutolewa kutoka ndani ya basi walipokuwa wamebanwa kwa zaidi ya saa nne.
 Mmoja kati ya majeruhi waliokuwa wakitolewa ndani ya basi hilo la Transmission.

Zaidi ya abiria ishirini na watano wamejeruhiwa kufuatia ajali mbaya ya basi la kampuni ya Transmission lililokuwa likifanya safari zake kutoka Kigoma kuelekea Tabora majira ya saa mbili usiku wa jana eneo la kata ya Ndono wilayani Uyui mkoani Tabora .

Basi hilo lenye nambari za usajili T 150 AHZ ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina moja la Pamba, imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva alishindwa kulimudu gari hilo katika barabara ya Ndono ambayo ipo katika matengenezo makubwa kwasasa.

Hata hivyo pamoja na basi hilo kuanguka vibaya hakuna mtu yeyote aliyepoteza maisha ingawa watu wanane walikuwa wamejehiwa vibaya wawili kati yao walikuwa wamekandamizwa ndani ya basi hilo,ambapo ikalazimika kampuni linalotengeneza barabara hiyo kuanza shughuli ya kuokoa watu hao kwa kushirikiana na Askari Polisi waliongozwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani wilaya ya Tabora Bw.Hamisi Kisandu ambapo walifanikiwa kuwatoa wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini mwao.



 

    






No comments: