Pages

KAPIPI TV

Friday, June 23, 2017

AKINAMAMA WALIMA NYANYA KINYEREZI DAR WAJIFUNZA KILIMO CHA UYOGA

Mafunzo kwa vitendo. Akinamama wa Kinyerezi Green Voices wakiweka udongo kwenye mifuko kama maandalizi ya kilimo cha uyoga.

MRITHI WA DKT. MDEGELA KKKT DAYOSISI YA IRINGA, MCHUNGAJI BLASTON GAVILE, KUWEKWA WAKFU JUMAPILI



Askofu Mteule Mchungaji Blastone Tuluwene Gavile (kushoto) akiwa na Msaidizi wa Askofu Mteule Mchungaji Himid  John Sagga.

IBADA ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gavile, inatarajiwa kufanyika Jumapili Juni 25, 2017 mjini Iringa.

Monday, March 27, 2017

WAZIRI MWIGULU AWAASA ASKARI KUTOWABAMBIKIZIA WATU KESI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Mzee John Samwel Malecela akizungumza wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
 Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
SACP Ramadhani Mungi Msimamizi wa bandari Tanzania na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renata Mzinga wakifatilia kwa makini kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mhe Mwigulu Lameck Nchemba akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi la Polisi mara baada ya kuwasili katika ufunguzi wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu Akisisitiza jambo wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha kazi cha Mwaka 2017 cha Maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi

Na Mathias Canal, Dodoma

Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesisitiza pia Askari na Maafisa wa Polisi kutotumia taarifa za watu wanaohasiana kuwa ndio chanzo pekee cha msingi wa shtaka badala yake kufanya uchunguzi kwa kina na kujiridhisha vyema ili kufikia hukumu yenye tija Na haki kwa mtuhumiwa kwani kufanya hivyo kutaimarisha amani na jeshi la Polisi kupata taarifa nyingi za uhalifu kutoka kwa wananchi endapo watajikita katika haki.

Akizungumzia Vita dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe Nchemba alisema kuwa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukamata na kuziteketeza Dawa za kulevya zilizopo mashambani ambapo ametilia msisitizo zaidi kwa Askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi kuendelea kupambana ili kuzikamata Dawa za kulevya zilizopo katika viwanda.

Amesisitiza pia Jeshi la Polisi kuendelea kupambana na kubaini uhalifu sambamba na kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha lengo mahususi la serikali ambalo ni kuzuia uhalifu linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka 2017 inayosema "ZINGATIA MAADILI TUNAPOPAMBANA NA UADILIFU ILI KUIMARISHA USALAMA KWA MAENDELEO YA TAIFA" endapo kama itatekelezwa kwa vitendo itaijenga nchi na kuzidi kudumisha zaidi amani iliyopo kwa wananchi.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu alisema kuwa kikao hicho cha kazi kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kina dhamira kubwa ya kufanya Tathmini ya utendaji wa mwaka 2016 na kuandaa mikakati mizuri ya mwaka 2017 na kupata fursa ya kubadilika kiutendaji kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hata hivyo amesisitiza zaidi askari wote nchini kutofanya kazi kwa mazoea, Kuacha Urasimu na kujenga uaminifu na weledi katika kazi.

Mangu amesema matendo ya Askari Polisi nchini yanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii hivyo askari Polisi hapaswi kuwa chanzo cha vurugu au kujihusisha na matendo ovu yasiyostahili katika jamii.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaombele kwa kujadiliwa katika Kikao hicho itakuwa ni pamoja na Vita dhidi ya Dawa za Kulevya, Vita dhidi ya Magendo, Vita dhidi ya ujangili na Uvuvi sambamba na Vita dhidi ya Ubambikizaji wa kesi kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha Waziri Mwigulu Nchemba kuzungumza na askari hao amelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi kubwa linayofanya ambapo pia ameeleza mpango wa Mkoa katika kupambana na migogoro ya ardhi kwa kuanzisha kamati maalumu ya wataalamu wa sheria kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Kupitia na kushauri ili kuweza kumaliza haraka migogoro hiyo.

Naye Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela alisema kuwa jambo la msingi ambalo askari Polisi wanapaswa kulifanya ni pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata Uhuru wake na kama jambo hilo likitekelezwa ipasavyo Fikra za Hayati Mwalimu J.K Nyerere zitakuwa zimeenziwa kwa weledi.

AGPAHI YAADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA KIFUA KIKUU – MERERANI, MKOA WA MANYARA


 
Picha ya pamoja katika maadhimisho ya kifua kikuu -  Mererani.

Shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative (AGPAHI) linalojishughulisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limeungana na wadau wote duniani katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani, 24 March 2017.

Maadhimisho hayo yalifanyika katika mji mdogo wa Mererani, wilaya ya Simanjiro katika Mkoa wa Manyara, eneo ambalo Shirika la AGPAHI linatekeleza mradi wa kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI sehemu za migodini kwa hisani ya shirika la ADPP la Msumbiji.

Katika maadhimisho hayo, shirika la AGPAHI kwa kushirikiana na timu ya afya ya wilaya walifanya zoezi la kutoa huduma mbalimbali kwa jamiii inayozonguka mji mdogo wa Marerani kuanzia tarehe 23 – 25 Machi, 2017.

Huduma zilizotolewa ni uchunguzi wa kifua kikuu, kupima Virusi vya Ukimwi na kutoa elimu kwa umma kuhusu kifua kikuu na VVU/UKIMWI.

Zoezi hilo lilisimamiwa na afisa mradi wa kifua kikuu na UKIMWI, kutoka AGPAHI, mratibu wa kifua kikuu na ukoma wa wilaya ya Simanjiro, wataalamu wa maabara, watoa huduma wa Afya kutoka kituo cha Afya Mererani na wahudumu wa afya ngazi ya jamii.

Kauli mbiu ya mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani ni; “TUUNGANE PAMOJA KUTOKOMEZA KIFUA KIKUU”.

Shirika la AGPAHI linafanya kazi katika mikoa sita ambayo ni Mwanza, Geita, Mara, Tanga Shinyanga na Simiyu. Huduma zitolewazo na shirika la AGPAHI ni kusaidia serikali kupitia vituo vya kutolea huduma za afya katika:

   1.Kutoa huduma za tiba na matunzo kwa watu
      wanaoishi na virusi vya UKIMWI;

   2.Kutoa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya
      UKIMWI kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto;

   3.Kutoa huduma ya uchunguzi wa dalili za awali na
      huduma za awali za saratani ya mlango wa kizazi
      na

    4.Kutoa huduma shirikishi za kifua kikuu na UKIMWI
     sehemu za migodini.

Vilevile, shirika linafanya kazi katika mji mdogo wa mererani katika kutekeleza mradi wa kifua kikuu sehemu za migodini.

Matukio katika picha.

Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI kutoka AGPAHI, Bi Alio Hussein akiwaelimisha na kugawa vipeperushi kwa wakazi wa Mererani kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Mhudumu wa afya ngazi ya jamii akiwaelezea wakazi wa Mererani dalili za Kifua Kikuu na namna ya kuweza kujikinga na maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.


Wahudumu wa Afya ngazi ya jamii wakichukua maelezo ya baadhi wakazi wa Mererani waliokua tayari kuchunguzwa kama wana maambukizi ya vijidudu vya Kifua Kikuu.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Kajolii Maasai akitoa burudani na kuendelea kuwahimiza wakazi wa Mererani kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Elimu kwa wachimbaji wa madini ya Tanzanite kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI ikiendelea.


Wachimbaji wa madini ya Tanzanite katika Kitalu D, wakiwa wamekusanyika kwa wingi wakielimishwa kuhusu Kifua kikuu na VVU/UKIMWI.


Bi. Alio Hussein akiwaonesha kwenye picha namna ambavyo vijidudu vya Kifua Kikuu vinaweza kusambaa kama mgonjwa atakohoa bila kuziba mdomo.


Wachimbaji wakielimishwa kuhusu aina za Kifua
Kikuu kwa njia ya bango.




Maswali mbalimbali yakiulizwa kwa wachimbaji juu ya kifua kikuu na UKIMWI.


Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Kajolii Maasai akitoa burudani kwa wachimbaji wa Kitalu D waliokusanyika kwa wingi kuja kupata Elimu kuhusu Kifua Kikuu.


Mchimbaji wa madini ya Tanzanite akijibu swali lililoulizwa ikiwa ni mwendelezo wa kutoa elimu na uhamasishaji kuhusu Kifua kikuu na Ukimwi.


Wa kwanza kushoto ni Kajolii Maasai msanii wa muziki wa kizazi kipya, wa pili kushoto ni mchimbaji wa madini ya Tanzanite ambaye alijishindia Tishirt baada ya kujibu vizuri swali kuhusu Kifua kikuu na watatu kutoka kushoto ni Afisa mradi wa Kifua kikuu na UKIMWI, Bi Alio Hussein, na mwisho ni Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Wilaya ya Simanjairo, Bi Selestina Rosai.


Na Joshua Fanuel wa Kilimanjaro Official blog,

Thursday, March 9, 2017

EfG YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI SOKO LA TEMEKE STERIO JIJINI DAR ES SALAAM


 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Soko la Temeke Sterio Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliandaliwa na shirika hilo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
 Mjumbe wa Bodi ya EfG, akizungumza katika maadhimisho hayo.
 Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris akitoa hutuba 
yake kwenye maadhimisho hayo.
 Mkuu wa Dawati la Jinsia Kituo cha Polisi Chang'ombe, Mkaguzi wa Polisi, Meshack Mpwage, akihutubia kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo. Kushoto ni Mwenyekiti wa muda wa muda wa wanawake wajasiriamali masokoni, Betty Mtewele na Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris.
 Kikundi cha Sanaa cha Machozi kikitoa burudani.
 Waananchi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
 Maadhimisho yakiendelea. wanawake wakiwa na mabango yenye maneno ya nafaa kuwa kiongozi.
 Meza kuu.
 Wafanyabiashara katika soko la Temeke Sterio wakifuatilia maadhimisho hayo.
 Burudani za sarakasi zikiendelea.

 Nifuraha tupu katika maadhimisho hayo.
 Hapa ni kuserebuka kwa kwenda mbele 'kweli ni wanawake na maendeleo'
 Vipeperushi juu.


Wasaidizi wa kisheria katika soko la Tabata Muslim jijini Dar es Salaam, Aisha Juma (kushoto) na Irene Daniel wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.

Na Dotto Mwaibale

TANZANIA ya Viwanda haitawezekana bila ya kuwepo wanawake wachapa kazi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita wakati akizungumza 
na waandisi wa habari kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika viwanja vya Soko la 
Temeke Sterio Dar es Salaam.

Magigita alisema wanawake waliowengi ndio wanaoinua uchumi wa nchi kutokana na kujikita katika ujasiriamali hivyo bila ya 
kuwepo mpango mzima wa Tanzania ya Viwanda hautakuwepo. 

Alisema wanawake wanapaswa kuendelea na sera yao ya kuhamasishana na kuunda vikundi ili iwe rahisi kwao kupata mikopo yenye riba nafuu kutoka katika Taasisi za 
kifedha ili waweze kusonga mbele katika shughuli zao za ujasiriamali.

"Tunaiomba serikali katika bajeti zake itenge fungu maalumu kwa ajili ya wanawake" alisema Magigita.

Alisema kauli mbiu ya siku ya wanawake mwaka huu ni Tanzania ya Viwanda Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko ya Uchumi.


Akizungumza kwa niaba ya Kamnada wa Polisi Mkoa wa Temeke, Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Kituo hicho, Mkaguzi wa Polisi, 
Meshack Mpwage alisema jeshi la polisi litaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kukabiliana na vitendo vya ukati wa kijinsia masokoni na maeneo mengine.

"Jeshi la polisi kupitia dawati la jinsia tutaendelea kutoa ushirikiano na masuala yote yanyohusu ukatili wa kijinsia na hatutasita kumchukua hatua mkosaji" alisma Mpwage.

Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Niall Morris alisema ukatili wa kijinsia upo duniani kote na si Tanzania pekee na umekuwa ukipingwa kwa nguvu zote.

"Matukio ya ukatili wa kijinsia yapo karibu duniani kote na yamekuwa yakipgiwa kelele kutoka na ukubwa wake hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kuwa katika mapambano 

hayo" alisema Morris. 

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Tuesday, March 7, 2017

MAANDALIZI YA TANZANIA DAY 2017 DALLAS TEXAS



Aprili 29, 2016, Mstahiki Meya wa jiji la Dallas, jimbo la Texas aliitangaza rasmi siku hiyo kuwa SIKU YA TANZANIA
Na mwaka huu, Jumuiya ya waTanzania waishio jimboni humo kwa kushirikiana na Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (Diaspora Council of Tanzanians in America) wanaandaa maadhimisho makubwa ya siku hiyo yatakayofanyika katika jiji la Dallas.
Viongozi Ben Kazora wa Jumuiya ya Dallas na Charles Bishota wa DICOTA wamezungumza na Mubelwa Bandio kuhusu maandalizi ya siku hiyo
KARIBU USIKILIZE

KUTOKA VOA SWAHILI:-ZULIA JEKUNDU

Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki kinachotayarishwa na kutangazwa na Mkamiti Kibayasi toka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA)
Kipindi hiki hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo
Juma hili, video mpya ya Ariana Grande, mzozo mkali kati ya Nicki Minaj na Remy Na unavyoendelea, matatizo ya iPhone 7plus, The Weekend alipokutana na Drake Ujerumani, Obamas ndani ya New York, kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake duniani na kadhalika
< br />

ULAJI WA VYAKULA NA KUTOFANYA MAZOEZI WACHANGIA ONGEZEKO LA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZWA

 mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro akichukuliwa vipimo  mara baada ya kuzindua wiki ya wanawake duniani ambayo kwa mkoa wa Arusha imeathimishwa katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid
 Muuandaaji ya wiki ya wanawake duniani kwa mkoa wa Arusha Phidesia Mwakitalima wa kwanza kulia  akishuhudua jinsi mkuu wa wilaya ya Arusha akiwa anachukuliwa vipimo vya afya yake




Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro akiwa anaingia uwanjani tayari kwa  uzinduzi  Rasmi zoezi la kupima Moyo, Cancer, Kisukari, Macho, Magonjwa Sugu ya mfumo wa hewa Bure yanayofanyika Arusha katika Viwanja vya Sheikh Amri Abeid  yaliyoandaliwa na Phide Entertainment kushirikiana na wafadhili mbalimbali ambapo kilele chake ni siku ya wanawake duniani tar 8/3/2017

Habari picha na Woinde Shizza,Arusha
Tatizo la baadhi ya watanzania kula vyakula bila mpangilio na kutofanya mazoezi ili kulinda afya zao limechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la magonjwa ya kisukari ,kansa,na shinikizo la damu.

Hayo yalisemwa na mtaalamu wa magonjwa ya yasiyoambukizwa kutoka hospitali ya mkoa wa Arusha,Mt meru,Dk Beatrice Ngogi wakati wa zoezi la upimaji wa afya bure lililofanyika jana katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.

Akihojiwa na waandishi wa habari mtaalamu huyo alisema asilimia kubwa ya kundi la watu walioathirika na magonjwa yasiyoambukizwa ni kati ya umri wa miaka 45-60 na kudai kuwa  mtindo wa maisha ya watu umechangia kwa kiasi kikubwa  ongezeko la magonjwa hayo.

“mtindo wa maisha umekuwa ni tatizo kubwa kwetu ndio maana tunawasihi watanzania tufanye mazoezi  na kuzingatia mlo wenye utaratibu”alisema mtaalamu huyo

Hatahivyo,mtaalamu wa magonjwa ya kisukari katika hospitali ya rufaa ya KCMC mkoani kilimanajro,DK Valeria Matei alisema kwamba  katika siku za karibuni watoto wadogo wanazaliwa wakiwa na ugonjwa wa kisukari mbali na wazee ambao ilikuwa imezoeleka.


Alisema kwamba elimu ya afya ni muhimu sana itolewe katika jamii ya watanzania kwa kuwa wengi wanakumbwa na ugonjwa huo bila kujijua na wakishajitambua ugonjwa huo unakuwa umeshawathiri kwa kiasi kikubwa.

Doroth Kuziwa, ambaye ni mwathirika wa ugonjwa wa kisukari alisema ya kwamba alikuwa kubaini kuathirika na ugonjwa huo kwa muda mrefu huku akisisitiza kwamba vyakula vya wagonjwa wengi wa kisukari vimekuwa ghali hali ambayo inawafanya washindwe kumudu gharama hizo.

Hatahivyo,Hiza Omary ambaye ni mgonjwa wa macho alisema kwamba aliacha kazi ya udereva kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya macho huku akisema kwamba vyombo vya habari vina jukumu kubwa la kuhabarisha umma kuhusu elimu ya afya katika jamii.

Mkurugenzi wa kampuni ya Phide Entertainment,Phidesia Mwakitalima alisema kwamba kampuni yake imeingia mkataba na hospitali za KCMC  na Mt Meru kwa lengo la kufadhili  zoezi la upimaji wa afya bure kwa wakazi wa mkoa  wa Arusha  katika kuelekea siku ya wanawake duniani.

Alisema kwamba zoezi hilo litahitimishwa siku ya kilele cha siku ya mwanamke duniani  huku akisisitiza kundi la wanawake kuzingatia mfumo wa ulaji wa vyakula mbalimbali ili kuepuka magonjwa yasiyoambukizwa.

 mmoja wa madaktari wanaotoa huduma akiwa anachukuwa damu salama kutoka kwa mwananchi ambaye amejitolea kuchangia damu
 mmoja wa daktari akimpongeza mamaa mara baada ya kupimwa na kukutwa anaugongwa wa presha
Dokta kutoka katika hospiotali ya kcmc akitoa elimu kwa wamama waliouthuria kupata huduma ya kupimwa bure
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mh Gabriel Fabian Daqarro Akisaini Daftari la Wageni la Phide Entertainment baada ya Uzinduzi wa Zoezi la kupima buree wananchi Moyo, Cancer, Kisukari, Macho na Magonjwa sugu ya mfumo wa Hewa .. Pamoja na changizo la Damu kwa ajili ya Ward za Wazazi Mkoani Arusha