Pages

KAPIPI TV

Wednesday, September 21, 2016

WATANZANIA WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA


Na Rabi Hume, MO BLOG

Kutokana na kuwepo na shughuli nyingi za kibinadamu ambazo zinaharibu mazingira, watanzania nchini kote wametakiwa kuwa makini kwa kutunza mazingira yanayowazunguka ili kuepusha matatizo ambayo yanaweza kutokea kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo vya uharibifu mazingira.

Rai hio imetolewa na Balozi Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Geneva, Uswisi, Modest Mero katika warsha ya kujadili kuhusu kilimo na biashara iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Balozi Mero alisema kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa na shughuli nyingi ambazo zinaharibu mazingira hali ambayo inatishia maisha ya vizazi vijavyo na hivyo ni vyema watanzania wakaanza kuchukua hatua kwa kutunza mazingira ili kuepeusha athari ambazo zitajitokeza kwa miaka ijayo.

"Dunia nzima watu wanakata miti, wanachoma majani mashambani lakini hawajui kama kuna vitu vya muhimu wanaua ardhini, na mimi niwambie watanzania wawe makini wasikate miti ambayo inawazunguka huo ni uharibifu wa mazingira," alisema Balozi Mero.
Balozi Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Geneva, Uswisi, Modest Mero akizungumza na washiriki wa warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), ikizungumza kuhusu kilimo na biashara. (Picha zote na Rabi Hume - MO BLOG)

Aidha alisema kuwa kwa sehemu kubwa watu ambao wanachangia vitendo hivyo ni wafanyabiashara na hivyo kuwataka wafanyabiashara kuacha vitendo vya kukata miti ikiwa bado haijafika katika muda sahihi ambao wanaruhusiwa kuikata.

"Wafanyabiashara wanakata sana miti, lakini wajue kuwa wakikata hovyo baadae wataikosa hiyo miti, ili mazingira yanayotuzunguka yawe mazuri inabidi kuyatunza ila tukitumia vibaya hata vyanzo vya maji vitakauka," alisema Mero.
Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Osward Mashindano akizungumzia malengo ya warsha hiyo.

Nae Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Osward Mashindano alisema warsha hiyo ina lengo la kuzungumzia jinsi gani kilimo, biashara, usalama wa chakula na mabadiliko ya hali ya nchi jinsi ambavyo vinaweza kutoa matokeo mazuri au mabaya.

Alisema kuwa pamoja na matokeo hayo, pia wanazungumzia ni hatua gani inafaa kuchukuliwa iwapo matokeo yanakuwa ni mazuri au mabaya ili kumsaidia mkulima mdogo kwa jinsi gani anaweza kufaidika na kilimo chake na kuepuka kupata hasara.

"Bidhaa kwa sasa zinatakiwa kuongezwa thamani, bidhaa kama haijaboreshwa haiwezi kuwa na soko zuri la ndani na hata nje ya nchi, tunataka kujua matokeo yake yanakuwaje maana biashara inavutia kutokana na soko lake lilivyo,

"Watu wanatakiwa kujua matokeo kama ni mazuri wafanyaje kama wengine wanaweza wanachangamkia fursa au kama ni mabaya wajue jinsi gani wanaweza kupunguza athari hizo ... tunatazama hilo maana hata sera zilizopo sasa hazisemi hatua gani ichukuliwe kama matokeo ni mabaya au mazuri," alisema Dkt. Mashindano.

Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakihangia mada zilizokuwa zikijadiliwa.



Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujadili kuhusu kilimo na biashara iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).



Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

WATU 283 WAJITOKEZA KUPIMA VVU/UKIMWI KWENYE MKESHA WA MWENGE WILAYANI IKUNGI

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikimbia na baadhi ya watumishi wa Wilaya yake ishara ya kuukabidhi Mwenge wa uhuru Manispaa ya singida mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Ikungi
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akizungumza wakati wa kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kupima Virusi Vya Ukimwi
Wananchi wa Manispaa ya Singida wakiusubiri Mwenge wa Uhuru kwa shauku kubwa muda mchache kabla ya kuwasili katika eneo lao ukitokea Wilaya ya Ikungi

MBUNGE PETTER MSIGWA AMEKABIDHI MADAWATI 537 KWA AJILI YA JIMBO LA IRINGA MJINI



MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati  537 ambayo ameyatoa kwa ajili ya jimbo la iringa mjini.


 MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati  537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
 MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati  537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
haya ni baadhi ya madawati 537aliyokabidhi MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msingwa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA



MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa amekabidhi madawati hayo 537 ambayo ameyatoa katika jimbo lake yataweza kuwa mkombozi mkubwa kutokana na kuweza kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya kusoma katika mlundikano mkubwa na baadhi yao walikuwa  wanakaa chini ya sakafu.


Aidha Msigwa katika hotuba yake ya kukabidhi madawati hayo amewataka viongozi wa manispaa ya iringa na tabia ya kuhujumu na kuiharibu  miundombinu ya shule na badala yake wahakikishe wanatunza mali zote za serikali kwa lengo la kuweza  kuwasaidia watoto wengine wa vizazi vijavyo waweze kusoma katika mazingira mazuri.


“Sipendi kuona wanafunzi wanaosoma katika shule za jimbo langu wanakaa chini,kitendo hicho huwa kinaniumiza sana ndio maana nimeamua kupambana kutafuta madawati ili kufanikisha adhima yangu ya kukuza elimu kwa wanafunzi wa jimbo la iringa mjini”alisema Msigwa



Naye meya wa halmashauri ya manispaa ya iringa Alex Kimbe amesema kwamba kwa sasa hawana mapungufu yoyote ya madawati hivyo  hakutakuwa na changamoto ya mwanafunzi wake kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu.


MADAWATI hayo 537 ambayo yametolewa na ofisi ya Mbunge wa Iringa Mjini yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 60 yatasambazwa katika kata zote ambapo pia yataweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea adha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto hiyo kwa kipindi cha muda mrefu na hatimaye  kuongeza kiwango cha ufaulu.
 

Lakini tatizo la kupanda na kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika baadhi ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya manispaa ya iringa lilikuwa linasababishwa na wanafunzi wengine  kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu sambamba  na kuwepo katika mazingira ya  miundombinu ambayo sio rafiki kwao hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao.


Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari na shule za msingi katika manispaa ya iringa.


 Wanafunzi hao akiwemo Ayoub Joseph,Paul Kisige pamoja na Riziki Ismail walisema kwamba kitendo cha baadhi yao kujisomea wakiwa sakafuni kimepelekea kupunguza uwezo wa kifikiri na kujikuta wanafanya vibaya katika masamo yao na kushindwa kufaulu, hivyo wamempongeza mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji Petter Msingwa kwa juhudi wanazozifanya za kupambana na adha ya  madawati.



“Hapo mwanzoni kwa kweli hali ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu wanafunzi wengine walikuwa wanasoma wakiwa wanakaa chini ya sakafu na hii kiukweli unamwondolea kabisa uwezo wa kufanya vizuri mwanafunzi, lakini kutokana na agizo hili la Rais tumepata nafuu kubwa na wanafunzi tuna imani tutaweza kufanya vizuri katika masomo yetu, na pia tunampongeza mbunge wetu kwa juhudi zake za kutuletea madawati,”walisema wanafunzi hao.


Pia walisema kwamba pamoja na changamoto ya kuwepo kwa upungufu wa madawati lakini serikali inatakiwa kuhakikisha inatilia mkazo suala linguine la nyumba za walimu pamoja na kuimarisha mambo mengine ya msingi, kama kuongeza madarasa mwengine ili kuweza kuepukana na mlundikano kwa wanafunzi.

JESHI LA POLISI KILIMANJARO LAWATUNUKU ZAWADI ASAKARI WAKE 34

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali waliotekeleza vyema majukumu yao.kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Wilbroad Mutafungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mjini Moshi kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akihitimisha ukaguzi wakati wa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza asakari walitekeleza vyema majukumu yao.
Gwaride likitoka kwa mwendo wa haraka mara baada ya kumalizika kwa ukaguzi.
Ofisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi  mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 wa jeshi hilo waliotekeleza vyema majukumu yao.
Baadhi ya maofisa wa jeshi la Polisi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari 34  waliotekeleza vyema majukumu yao.
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuoneesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq baadhi ya silaha zilizokamatwa hivi karibuni zikidaiwa kutumika katika vitendo vya uharifu.
Mkuu wa Kitengo cha dawa za kulevya cha jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Mkaguzi wa Polisi,Ezekiel Midala akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro sehemu ya dawa za kulevya zilizokamatwa na jeshi hilo.
Baadhi ya askari waliotunukuwa zawadi kwa utendaji kazi mzuri wakisonga mbele kwa ajili ya kutunukiwa zawadi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitunuku zawadi kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa asakari waliofanya vizuri wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Pikipiki mbili aina ya Fekon zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai kusaidia jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akiwa ameketi juu ya pikipiki na kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Mwandamizi Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa askari  34 wa jeshi hilo mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitoa cheti kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akitambua mchango wa wadau kwa jeshi la Polisi. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

Tuesday, August 30, 2016

MKURUGENZI WA FULLSHANGWEBLOG AKABIDHIWA TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU 2015

1
Bw . Mohamed Seif Ofisa kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tume hiyo akikabidhi kwa Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015, Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye mgahawa wa Mokka City Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam.
2
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015 mara baada ya kukabidhiwa rasmi.
3
Bw. John Bukuku Mkurugenzi wa Mtandao wa Fullshangweblog Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani 2015

MAHOJIANO NA PROF.JULIUS NYANG'ORO KATIKA KIPINDI CHA JUKWAA LANGU

Profesa Julius Nyang'oro ni Mwalimu, mtaalam wa sayansi ya siasa na mwanasheria.
Amekuwa mwalimu tangu mwaka 1977 nchini Tanzania na hapa nchini Marekani.

Ni mwandishi wa vitabu zaidi ya 14, vingi vikiigusia Tanzania kwa namna moja ama nyingine. Moja ya vitabu alivyoandika, na ambavyo vilimtambulisha zaidi kwa jamii ya waTanznia, ni kumhusu Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete. Ambapo ameandika vitabu viwili kumhusu.

Prof Nyang'oro alikuwa mkarimu sana kuungana nasi kwenye kipindi cha JUKWAA LANGU Jumatatu ya Agosti 29, 2016 kuzungumzia mambo mbalimbali kuihusu Tanzania akiwa mwandishi, mwalimu, mtaalamu wa mausala ya siasa na mwanasheria
KARIBU

RC SINGIDA AKABIDHI MADAWATI 630 KWA WAKURUGENZI WA WILAYA NA MANISPAA

Na Mathias Canal, Singida


Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Mkoa wa Singida wamekabidhiwa jumla ya madawati 90 kwa kila Halmashauri ili kuondoa adha waliyokuwa wanakumbana nayo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipowaagiza wakuu wa mikoa yote nchini wakati akiwaapisha Ikulu, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.




Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa chini wakiwa darasani.


 Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
Mtigumwe amesema kuwa Hali ya Madawati katika Mkoa ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500 hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika Halmashauri za Singida na Manyoni.

WATANZANIA WARAHISISHIWA UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA TEKNOLOJIA


Pamoja na kuwepo kwa maendeleo ya kasi katika nyanja mbalimbali lakini sekta ya teknolojia inabaki kuwa moja ya njia ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa kupatikana kwa mafanikio hayo kwa kurahisisha kazi nyingi kufanyika kwa haraka.

Kwa kutambua hilo, kampuni inayohusika na utoaji wa huduma zinazohusiana na teknolojia ya EnGenius imeingia katika makubaliano na kampuni ya usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia ya Red Dot ili iweze kusambaziwa vifaa na huduma mbalimbali ambazo zinafanywa na Red Dot katika nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao akizungumzia kazi ambazo wanazifanya na mipango ya kutoa bidhaa bora kwa nchi za Afrika Mashariki.

Kampuni ya EnGenius ambayo inatoa huduma kama za internet wireless, radio frequency (RF) technology na kusambaza bidhaa mbalimbali kama kompyuta imesema kuwa imefanya maamuzi ya kuingi katika makubaliano na Red Dot ikiamini kuwa ni moja ya njia sahihi ambayo itawawezesha kuwafikia wateja kwa karibu zaidi.

Akizungumzia makubaliano hayo, Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao alisema kampuni ao kwa sasa inahitaji kujitanua katika nchi za Afrika Mashariki kama Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Ethiopia hivyo wameungana na Red Dot ili waweze kukuza biashara yao zaidi.

"Tumeingia makubaliano na moja ya wasambazaji wakubwa wa Red Dot na tunaamini watatusaidia EnGenius kufikia malengo yetu ya kuwa wauzaji wakubwa wa bidhaa za kiteknolojia kwa Afrika Mashariki, tunafahamu kuwa ni wasambazaji wakubwa na atatusaidia kukuza biashara yetu," alisema Hsiao.


Na Rabi Hume, modewjiblog.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution akielezea jinsi ambavyo wamejipanga kufanya kazi na EnGenius. (Picha zote na Na Rabi Hume, modewjiblog.com)

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani alisema kuwa ni ushirikiano mzuri ambao wameanza kuufanya na EnGenious na wana mipango mingi kuhakikisha malengo ambayo yamewekwa yanafikiwa.

"Tuna taraji mafanikio makubwa, Red Dot ni kampuni ya kitanzania ambayo inafanya kazi katika nchi za Afrika Mashariki kwahiyo tunatazamia ushirikiano huu utakuwa na faida," alisema Bharwani.
Meneja Mkuu wa Red Dot Distribution Tanzania, Rajesh Adiani akifungua halfa ya uzinduzi wa makubaliano kati ya Red Dot na EnGenius kwa kuelezea shughuli ambazo wanazifanya.
Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa EnGenius, Alishan Zaidi akilelezea huduma ambazo wanazitoa za kiteknolojia na usambazaji wa vifaa vya kiteknolojia kama kompyuta na kamera za usalama.
Mkurugenzi Mtendaji wa Red Dot Distribution, Munir Bharwani na Mkuu wa Kanda wa EnGenius, Van Hsiao wakipongezana baada ya kuingia rasmi katika makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja.

Baadhi ya wageni waalikwa wakiangalia bidhaa ambazo zinatolewa na EnGenius.
Baadhi ya wageni waaliakwa waliohudhuria halfa ya makubaliano ya Red Dot Distribution na EnGenius.