Pages

KAPIPI TV

Wednesday, September 21, 2016

MADEREVA 10 WA TANZANIA WALIOTEKWA NCHINI CONGO WAREJEA NCHINI NA KUSEMA WALIPONEA TUNDU LA SINDANO KUUAWA

 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba (katikati), akizungumza na madereva 10 wa Tanzania waliotekwa na watu wanaodaiwa kuwa ni waasi Jamhuri ya Demokrasia ya Conco (DRC), wakati wa hafla fupi ya kuwapokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam leo jioni. Kulia ni Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba na kushoto ni Mkurugenzi  Idara ya Afrika katika wizara hiyo, Balozi Samweli Shelukindo.
 Balozi wa Congo nchini, Jean Mutamba (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo.
 Mmiliki wa Kampuni ya Simba Logistic ambayo magari yake na madereva walitekwa, Azim Dewj (kushoto), akizungumza katika hafla hiyo ya kuwapokea madereva hao.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakisubiri kuchukua taarifa za kuwapokea madereva hao.
 Madereva hao wakipokelewa uwanjani hapo.
 Madereva hao wakiwa chumba cha mkutano cha uwanja huo wakati wa mapokezi yao.
Dereva  Mbwana Said (kulia), akielezea jinsi walivyotekwa.
 Dereva Kumbuka Seleman (kulia), akisimulia jinsi alivyotoroka na kutoa taarifa ya kutekwa kwao.
Dereva  Athuman Fadhili (kulia), akisimulia walivyookolewa na majeshi ya Congo na jinsi walivyojificha porini na kutembea umbali mrefu kwa kutambaa ambapo ilifika wakati waliomba bora wafe kuliko mateso waliyokuwa wakipata.
 Hapa ni furaha ya kukutana na ndugu jamaa na wafanyakazi wenzao.
 Picha ya pamoja na viongozi waliowapokea.
 Ndugu, Jamaa, marafiki na wafanyakazi wenzao wakiwa nje ya jengo la VIP uwanjani hapo wakisubiri kuwapokea.
 Mapokezi yakiendelea.
Ni furaha ya kukutana na wapendwa wao.
Hapa Dereva Mbwana Said akikumbatia na mjomba wake Kassim Salim katika hafla hiyo kwa Mbwana ilikuwa ni furaha na majonzi. 
Mbwana Said (katikati), aamini macho yake baada ya kukutana na mke wake Mariam pamoja na mtoto wake Kauzari.

Na Dotto Mwaibale

MADEREVA 10 wa Tanzania waliotekwa na watu  wanaodhaniwa ni waasi Jamhuri ya Demokraia ya Congo (DRC) wamesema waliponea tundu la sindano kuuawa.

Kauli hiyo imetolewa na madereva hao katika hafla ya kuwapokelewa iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam leo jioni.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake Mbwana Said alisema analishukuru jeshi la Congo kwa jitihada kubwa walioifanya kwa ajili ya kuokoa maisha yao." 

" Tunaishukuru serikali ya Congo kwa kutuokoa kwani tulikuwa katika wakati mgumu na leo kuungana tena na ndugu zetu" alisema Said.

Alisema walilazimia kutembea kwa muda mrefu huku risasi zikirindima kati ya majeshi ya serikali na waasi hao hadi walipofanikiwa kutuokowa kutoka kwenye mikono ya waasi hao. 

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Suzan Kolimba aliishukuru serikali ya Congo kwa jitihada iliyoifanya na kufanikiwa kuwaokoa madereva hao.

Balozi wa Congo nchini Jean Mutamba aliwataka madereva hao kuacha viza na nyaraka zao ubalozini pindi wanapo safiri na kurudi ili iwe rahisi kuwatambua pale wanapopata matatizo.

"Tukio hilo limetokea kwa bahati mbaya na kutoa wito kuwa waendelee kusafiri kwa kufuata taratibu zilizopo," alisema Mutamba.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712727062)



WATANZANIA WATAKIWA KUTUNZA MAZINGIRA


Na Rabi Hume, MO BLOG

Kutokana na kuwepo na shughuli nyingi za kibinadamu ambazo zinaharibu mazingira, watanzania nchini kote wametakiwa kuwa makini kwa kutunza mazingira yanayowazunguka ili kuepusha matatizo ambayo yanaweza kutokea kutokana na kushindwa kudhibiti vitendo vya uharibifu mazingira.

Rai hio imetolewa na Balozi Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Geneva, Uswisi, Modest Mero katika warsha ya kujadili kuhusu kilimo na biashara iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

Balozi Mero alisema kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa na shughuli nyingi ambazo zinaharibu mazingira hali ambayo inatishia maisha ya vizazi vijavyo na hivyo ni vyema watanzania wakaanza kuchukua hatua kwa kutunza mazingira ili kuepeusha athari ambazo zitajitokeza kwa miaka ijayo.

"Dunia nzima watu wanakata miti, wanachoma majani mashambani lakini hawajui kama kuna vitu vya muhimu wanaua ardhini, na mimi niwambie watanzania wawe makini wasikate miti ambayo inawazunguka huo ni uharibifu wa mazingira," alisema Balozi Mero.
Balozi Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa Geneva, Uswisi, Modest Mero akizungumza na washiriki wa warsha iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), ikizungumza kuhusu kilimo na biashara. (Picha zote na Rabi Hume - MO BLOG)

Aidha alisema kuwa kwa sehemu kubwa watu ambao wanachangia vitendo hivyo ni wafanyabiashara na hivyo kuwataka wafanyabiashara kuacha vitendo vya kukata miti ikiwa bado haijafika katika muda sahihi ambao wanaruhusiwa kuikata.

"Wafanyabiashara wanakata sana miti, lakini wajue kuwa wakikata hovyo baadae wataikosa hiyo miti, ili mazingira yanayotuzunguka yawe mazuri inabidi kuyatunza ila tukitumia vibaya hata vyanzo vya maji vitakauka," alisema Mero.
Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Osward Mashindano akizungumzia malengo ya warsha hiyo.

Nae Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Osward Mashindano alisema warsha hiyo ina lengo la kuzungumzia jinsi gani kilimo, biashara, usalama wa chakula na mabadiliko ya hali ya nchi jinsi ambavyo vinaweza kutoa matokeo mazuri au mabaya.

Alisema kuwa pamoja na matokeo hayo, pia wanazungumzia ni hatua gani inafaa kuchukuliwa iwapo matokeo yanakuwa ni mazuri au mabaya ili kumsaidia mkulima mdogo kwa jinsi gani anaweza kufaidika na kilimo chake na kuepuka kupata hasara.

"Bidhaa kwa sasa zinatakiwa kuongezwa thamani, bidhaa kama haijaboreshwa haiwezi kuwa na soko zuri la ndani na hata nje ya nchi, tunataka kujua matokeo yake yanakuwaje maana biashara inavutia kutokana na soko lake lilivyo,

"Watu wanatakiwa kujua matokeo kama ni mazuri wafanyaje kama wengine wanaweza wanachangamkia fursa au kama ni mabaya wajue jinsi gani wanaweza kupunguza athari hizo ... tunatazama hilo maana hata sera zilizopo sasa hazisemi hatua gani ichukuliwe kama matokeo ni mabaya au mazuri," alisema Dkt. Mashindano.

Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakihangia mada zilizokuwa zikijadiliwa.



Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujadili kuhusu kilimo na biashara iliyoandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).



Washiriki wakiwa katika picha ya pamoja.

WATU 283 WAJITOKEZA KUPIMA VVU/UKIMWI KWENYE MKESHA WA MWENGE WILAYANI IKUNGI

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akikimbia na baadhi ya watumishi wa Wilaya yake ishara ya kuukabidhi Mwenge wa uhuru Manispaa ya singida mara baada ya kumaliza mbio zake Wilayani Ikungi
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akizungumza wakati wa kuwashukuru wananchi kwa kujitokeza kupima Virusi Vya Ukimwi
Wananchi wa Manispaa ya Singida wakiusubiri Mwenge wa Uhuru kwa shauku kubwa muda mchache kabla ya kuwasili katika eneo lao ukitokea Wilaya ya Ikungi

MBUNGE PETTER MSIGWA AMEKABIDHI MADAWATI 537 KWA AJILI YA JIMBO LA IRINGA MJINI



MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati  537 ambayo ameyatoa kwa ajili ya jimbo la iringa mjini.


 MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati  537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
 MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati  537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
haya ni baadhi ya madawati 537aliyokabidhi MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msingwa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA



MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa amekabidhi madawati hayo 537 ambayo ameyatoa katika jimbo lake yataweza kuwa mkombozi mkubwa kutokana na kuweza kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya kusoma katika mlundikano mkubwa na baadhi yao walikuwa  wanakaa chini ya sakafu.


Aidha Msigwa katika hotuba yake ya kukabidhi madawati hayo amewataka viongozi wa manispaa ya iringa na tabia ya kuhujumu na kuiharibu  miundombinu ya shule na badala yake wahakikishe wanatunza mali zote za serikali kwa lengo la kuweza  kuwasaidia watoto wengine wa vizazi vijavyo waweze kusoma katika mazingira mazuri.


“Sipendi kuona wanafunzi wanaosoma katika shule za jimbo langu wanakaa chini,kitendo hicho huwa kinaniumiza sana ndio maana nimeamua kupambana kutafuta madawati ili kufanikisha adhima yangu ya kukuza elimu kwa wanafunzi wa jimbo la iringa mjini”alisema Msigwa



Naye meya wa halmashauri ya manispaa ya iringa Alex Kimbe amesema kwamba kwa sasa hawana mapungufu yoyote ya madawati hivyo  hakutakuwa na changamoto ya mwanafunzi wake kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu.


MADAWATI hayo 537 ambayo yametolewa na ofisi ya Mbunge wa Iringa Mjini yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 60 yatasambazwa katika kata zote ambapo pia yataweza  kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea adha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto hiyo kwa kipindi cha muda mrefu na hatimaye  kuongeza kiwango cha ufaulu.
 

Lakini tatizo la kupanda na kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika baadhi ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya manispaa ya iringa lilikuwa linasababishwa na wanafunzi wengine  kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu sambamba  na kuwepo katika mazingira ya  miundombinu ambayo sio rafiki kwao hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao.


Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari na shule za msingi katika manispaa ya iringa.


 Wanafunzi hao akiwemo Ayoub Joseph,Paul Kisige pamoja na Riziki Ismail walisema kwamba kitendo cha baadhi yao kujisomea wakiwa sakafuni kimepelekea kupunguza uwezo wa kifikiri na kujikuta wanafanya vibaya katika masamo yao na kushindwa kufaulu, hivyo wamempongeza mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji Petter Msingwa kwa juhudi wanazozifanya za kupambana na adha ya  madawati.



“Hapo mwanzoni kwa kweli hali ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu wanafunzi wengine walikuwa wanasoma wakiwa wanakaa chini ya sakafu na hii kiukweli unamwondolea kabisa uwezo wa kufanya vizuri mwanafunzi, lakini kutokana na agizo hili la Rais tumepata nafuu kubwa na wanafunzi tuna imani tutaweza kufanya vizuri katika masomo yetu, na pia tunampongeza mbunge wetu kwa juhudi zake za kutuletea madawati,”walisema wanafunzi hao.


Pia walisema kwamba pamoja na changamoto ya kuwepo kwa upungufu wa madawati lakini serikali inatakiwa kuhakikisha inatilia mkazo suala linguine la nyumba za walimu pamoja na kuimarisha mambo mengine ya msingi, kama kuongeza madarasa mwengine ili kuweza kuepukana na mlundikano kwa wanafunzi.

JESHI LA POLISI KILIMANJARO LAWATUNUKU ZAWADI ASAKARI WAKE 34

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akipokea salamu za heshima kutoka kwa askari wakati wa gwaride maalum lililoandaliwa wakati wa hafla fupi ya kutunuku zawadi kwa askari 34 wa vyeo mbalimbali waliotekeleza vyema majukumu yao.kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro ,Wilbroad Mutafungwa.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akikagua gwaride la heshima baada ya kuwasili katika viwanja vya kikosi cha kutuliza ghasia mjini Moshi kwa ajili ya hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Saidiq akihitimisha ukaguzi wakati wa gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili ya kuwapongeza asakari walitekeleza vyema majukumu yao.
Gwaride likitoka kwa mwendo wa haraka mara baada ya kumalizika kwa ukaguzi.
Ofisa Mnadhimu wa jeshi la Polisi  mkoa wa Kilimanjaro,Koka Moita akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 wa jeshi hilo waliotekeleza vyema majukumu yao.
Baadhi ya maofisa wa jeshi la Polisi wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa askari 34  waliotekeleza vyema majukumu yao.
Baadhi ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Said Mecky Sadiq akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutunuku zawadi kwa asakari 34 waliotekeleza vyema majukumu yao.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Wilbroad Mutafungwa akimuoneesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq baadhi ya silaha zilizokamatwa hivi karibuni zikidaiwa kutumika katika vitendo vya uharifu.
Mkuu wa Kitengo cha dawa za kulevya cha jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Mkaguzi wa Polisi,Ezekiel Midala akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro sehemu ya dawa za kulevya zilizokamatwa na jeshi hilo.
Baadhi ya askari waliotunukuwa zawadi kwa utendaji kazi mzuri wakisonga mbele kwa ajili ya kutunukiwa zawadi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitunuku zawadi kwa baadhi ya askari waliofanya vizuri katika kutekeleza majukumu yao.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai akizungumza wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa asakari waliofanya vizuri wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Pikipiki mbili aina ya Fekon zilizotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Asante Tours ,Cuthbert Swai kusaidia jeshi la Polisi katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akiwa ameketi juu ya pikipiki na kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Mwandamizi Msaidizi wa Polisi,Wilbroad Mutafungwa wakati wa hafla ya kuwapongeza na kutoa zawadi kwa askari  34 wa jeshi hilo mjini Moshi.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Mecky Sadiq akitoa cheti kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Ibraline ,Ibrahim Shayo akitambua mchango wa wadau kwa jeshi la Polisi. 

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.