Pages

KAPIPI TV

Wednesday, August 10, 2016

VIJANA WAENDESHA MDAHALO KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI KUELEKEA SIKU YA KIJANA DUNIANI, KARIMJEE JIJINI DAR

Mwakilishi Mkazi msaidizi kutoka UNFPA Bi. Christine Mwanukuzi akifungua mdahalo huo, kuwashukuru vijana kwa kujumuika pamoja na kuwapongeza kwa kufanikisha mdahalo huo kuelekea katika siku ya vijana duniani siku ya tarehe 12.08.2016
Bw. Badru Juma Rajabu akielezea historia ya siku ya vijana ilipoanzia na kusisitiza kuwa vijana wanatakiwa kutambulika na wasisahau kuchukua fursa pale wanapowezeshwa

Oscar Kimario muwezeshaji kutoka Restless Development akielezea baadhi ya ripoti juu ya vijana na kuwasihi vijana kuwa ndio watakuwa mstari wa mbele katika maendeleo endelevu hivyo wanapaswa kujituma na kufanya kazi kwa bidii

Vijana wakiendelea kufuatilia mdahalo huo kwa makini
Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO Nancy Lazaro akizungumzia ajira zenye staha ,alisema kuwa vijana wengi wameajiriwa lakini katika ajira zisizo na staha na kusisitiza ifike kipindi sasa vijana waajiliwe na kazi zenye Staha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Msichana Initiatives Rebeca Gyumi akijibu maswali mbalimbali ambayo waliuliza vijana waliofika katika kongamano hilo na kusema kwamba sio kweli kwamba wanafunzi waliomaliza elimu ya vyuo ni vilaza
Vijana wakiendelea kufuatilia wajibu maswali wakijibu yale waliyo yauliza

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St.Josephs Veronica Shayo kidato cha tano akisisitiza vijana kuwa na tabia za kuweka akiba kwa kile wanachopata ili kije kuwasaidia pindi watakapo kuwa wakubwa.
Muwezeshaji wakati wa kongamano hilo la vijana ambalo kauli mbiu yake inasema Sepesha Umasikini kwa Michongo Endelevu na yenye tija Bw. Lawrence Ambokile akiendelea kutoa mwongozo 
Noreen Toroka akijibu baadhi ya maswali lakini pamoja na hayo amewasisitiza vijana kuto kutumia kipato wanacho kipata bila tija na wawe na utaratibu wa kuhifadhi kwa ajili ya maendeleo baadae, pia aliongeza kuwa vijana wasilazie damu fursa mbalimbali zinazotolewa kwa ajili yao

Baadhi ya vijana kutoka Restless Development na wanafunzi pamoja na wadau wakendelea kufuatilia mdahalo

Mwanzilishi wa Malkia Investment Bi. Jenipher Shigoli akichangia  jambo katika mdahalo huo

Albert Kutoka ILO akichangia na kujibu maswali ya vijana mbalimbali katika mdahalo huo ambapo alisisitiza vijana kujituma
 Mwanzilishi wa Charity Movement Sophia Mbeyela akitoa ushuhuda wake wa jinsi alivyo anza ujasiliamali tangia akiwa mdogo na kusisitiza kwamba vijana haijalishi ni mzima au ana ulemavu wa viungo vya mwili wake wote wanatakiwa kujumuika pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya Taifa

Kijana Onesmo akiwaeleza vijana wenzake kuwa kama wao walemavu wavioungo wanaweza kufanya mambo makubwa iwaje vijana wazima wasiweze hii ilikuwa ni changamoto

Picha ya pamoja ya Baadhi ya Washiriki wa Mdahalo huo

Picha na Fredy Njeje wa Blogs za Mikoa



YONO YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA UBORA WA KAZI

Mwenyekiti wa  Kampuni ya Udalali ya Yono Auction Mart, Yono Kevela, akionesha tuzo za kimataifa ya ufanisi bora wa kazi baada ya kukabidhiwa.

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Udalali ya Yono Auction Mart, imekabidhiwa tuzo ya Mshindi wa Kimataifa ya Ufanisi na Ubora wa Kazi, baada ya kushindanishwa na kampuni nyingine 49 za nchi tofauti duniani hatua iliyotokana na utendaji wake katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza Jijini Dar es salaam jana, Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Yono Kevela, alisema ushindi huo unatokana na ufanisi wao wa kazi zikiwepo za ukusanyaji madeni ya kodi kutoka kwa wadaiwa sugu wa serikali .

Kevela alisema baadhi ya kazi walizofanya baada ya kupata zabuni ya kukusanya madeni ya wadaiwa ni za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wizara mbalimbali, taasisi za fedha na wakala wa serikali pamoja na wadau wengine.

Alisema ushindi wa tuzo hiyo ni faida ya ufanisi wa kazi zao katika kukusanya kodi za serikali huku akiahidi kutobweteka katika jukumu hilo alilopewa na Serikali hadi kushinda tuzo hiyo na badala yake atazidi kuongeza juhudi ili kampuni hiyo izidi kufanya vizuri.

“Tunashukuru kazi na huduma zetu kutambuliwa kimataifa, tumekuwa mabalozi wazuri wa Tanzania, tumetumia fursa hiyo kuitangaza nchi na kuwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza “, alisema. Kevela

Alisema Tuzo hiyo ilitolewa Ufaransa na sherehe za kukabidhi washindi tuzo hizo zilifanywa Juni 25, mwaka huu Rome Italia ambako kampuni hiyo imeshinda ikitoka sekta binafsi, huku upande wa serikali ukishinda sekta ya Utalii kupitia Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).

Kampuni hiyo ya Yono imejizolea umaharufu hivi karibuni bada ya kupewa kazi ya kukusanya madeni ya wadaiwa 24 wa TRA, yenye thamani ya Sh bilioni 18.95 baada ya wadeni hao kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana.

Hata hivyo baada ya kampuni hiyo kuanza kazi, baadhi ya wadaiwa walifanikiwa kulipa madeni yao huku wengine wakilipa kiasi na wengine mali zao walikubali zikamatwe na kuuzwa ili kulipa madeni hayo, ambapo hadi sasa zaidi ya Sh bilioni saba zimeshakusanywa.

Maeneo mengine ambayo kampuni hiyo inafanya kazi ya kukusanya madeni dhidi ya wadaiwa mbalimbali ni pamoja na maeneo ya ardhi, mahakama, mabenki na taasisi zingine.

BUZWAGI YAKABIDHI SHULE MPYA NA NYUMBA ZA WALIMU KWA SERIKALI WILAYANI KAHAMA

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakati wa ziara ya kupokea miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyeweka mkono kwenye mfuko wa suruali) akiwa na wajumbe wengine wa kamati ya ulinzi na Usalama wa wilaya ya Kahama walipofanya ziara katika mgodi wa Buzwagi wa kukabidhiwa miradi ya maendeleo. 
Meneja Mkuu wa Mgodo wa Buzwagi Asa Mwaipopo akieleza jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
  Kifaa maalumu cha kupoza umeme ambacho kitatumika kupeleka umeme katika mji wa Kahama na kungunguza tatizo la kukosekana kwa umeme kikiwa kimefungwa katika kituo cha Umeme cha mgodi wa Buzwagi.
 Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (Mwenye kofia ya blue) akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) wakati wa makabidhiano ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Budushi, wengine katika picha ni mbunge wa kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kahama Mhe.Abel Shija. 
  Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu na Mbunge wa Kahama Mhe.Jumanne Kishimba wakizindua majengo ya shule mpya ya Budushi iliyojengwa kwa ufadhili wa mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na Mwenyekiti wa kijiji cha Budushi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo na nyumba moja ya walimu katika shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa Buzwagi na Watendaji wa Kata ya Mwendakulima
Moja ya majengo ya madarasa yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Budushi chini ya ufadhili wa Mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa kata ya Mwendakulima.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi uliyoko wilayani Kahama, katika mkoa wa Shinyanga, umekabidhi kwa uongozi wa katika Halmashauri ya mji wa Kahama majengo ya shule mpya ya msingi Budushi yenye madarasa sita, ofisi ya walimu na nyumba moja ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia mbili.
Akikabidhi madarasa hayo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema ujenzi huo umefadhiliwa na Mgodi wa Buzwagi kwa zaidi ya shilingi milioni mia nne na themani kupitia mfuko wa Acacia Maendeleo Fund, ambao umelenga kuwapunguzia adha wanafunzi wa eneo hilo la Budushi na maeneo yanayozunguka eneo hilo kuondokana na adha ya kutembea mwendo mrefu kwenda shule.
Aidha, Meneja mkuu huyo wa Mgodi wa Buzwagi alikabidhi pia nyumba mbili za kisasa za walimu zenye uwezo wa kuishi familia nne kwa shule ya msingi Mwime hatua ambayo amesema kuwa itasaidia katika kupunguza tatizo la nyumba kwa walimu kwa shule hiyo. Nyumba hizo ambazo zimejengwa kwa kutumia teknolojia ya Tofali za kufungamana zimegharimu shilingi milioni mia mbili arobaini na nane (248,126,000/=)
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea miradi hiyo ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.


WAZIRI WILLIAM LUKUVI ATEMBELEA NYUMBA ZILIZOHAMISHIWA UMILIKI TOKA SHIRIKA LA NYUMBA

1w
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akijadiliana jambo na Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa- Iringa, Repson Joshua wakati Waziri huyo alipofanya ziara mkoani humo na kupewa taarifa ya utendaji kazi wa Shirika baadaye kufanya ziara ya kutembelea nyumba zilizokuwa za NHC zamani na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa baadaye kurejeshwa Serikali Kuu na akakutana na wapangaji waliokuwa wamepanga kwenye nyumba hizo.
Waziri alikusudia kuona hali alisi ya nyumba zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, ili kupata taswira ya nyumba zote zilizoko Mikoa mingine na kutoa taarifa ya Mheshimiwa Rais juu ya mustakali wa nyumba hizi.
2s
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa- Iringa wakati Waziri huyo alipofanya ziara mkoani humo na kupewa taarifa ya utendaji kazi wa Shirika baadaye kufanya ziara ya kutembelea nyumba zilizokuwa za NHC zamani na kukabidhiwa kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa baadaye kurejeshwa Serikali Kuu na akakutana na wapangaji waliokuwa wamepanga kwenye nyumba hizo.
3s
Waziri Lukuvi, akiteta jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa William Donald Mafwele alipowasili ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa na baada ya hapo msafara uliojumuisha watendaji kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa wa Mkoa Iringa ulielekea eneo la barabara ya Kalenga kuliko na nyumba 49. Mheshimiwa Waziri alifanya ukaguzi wa eneo hilo na kumuuliza Mkurugenzi wa Halmashauri, William Donald Mafwele kuhusu hali ya umiliki ulivyo sasa. Baada ya hapo msafara wa Waziri ulielekea eneo la Barabara ya Pawaga kuliko na nyumba 25.
4s
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi akionyeshwa ramani ambapo nyumba zilizorudishwa TAMISEMI zilipo.
5s
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi, akimsikiliza maelezo toka kwa Mpima Ardhi wa Manispaa ya Iringa Mwenda.
6s
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi, akizungumza na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Boniphace Kimba.
7s
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi, akisikiliza kero za wapangaji waliopanga nyumba zilizokuwa Shirika.
8s
Wapangaji waliopanga kwenye nyumba zilizokuwa za NHC na kukabidhiwa kwa Manispaa ya Iringa wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Vangimembe Lukuvi (hayuko pichani) kwenye ukumbi wa Mwembetwoga mkoani Iringa.
9s
Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba Taifa mkoani Iringa, Repson Yosia akisoma taarifa mbele ya Mheshimiwa Waziri.
10s
Kaimu Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Iringa akimkabidhi taarifa Mheshimiwa Waziri.
11s
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, William Donald Mafwele akisoma taarifa mbele ya Mheshiwa Waziri.

ASASI YA FEDHA YAAMSHA FIKRA KWA VIJANA WA CHUO CHA KILIMANJARO ILI KUFIKIA UHURU WA KIPATO

Muanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Asasi ya FEDHA Jafari Selemani akizungumzia changamoto za vijana na watanzania kwaujumla juu  ya kutokufikia Uhuru wa kifedha (financial freedom) ikiwemo ukosefu wa elimu ya usimamizi fedha binafsi ambapo inapelekea umasikini wa watanzania wengi, pia alitumia nafasi hiyo kuzindua progranu ya FEDHA KLABU ambayo itakayowapa fursa vijana kupata elimu ya udhibiti fedha binafsi buree kila jumamosi chuoni hapo.


Ni mshauri wa vijana pia ni Meneja Masoko wa Taasisi ya  FEDHA Abdalah Kipinga akiongea na wanafunzi wa chuo ch Kilimanjaro ambapo alizungumzia juu ya maisha ya wanavyuo na changamoto zake na jinsi ya kuzikabili.

Mhamasishaji wa vijana Elly David akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro (hawapo pichani)  ambapo alizungumza kuhusu siri ya mafanikio kwa vijana na kuwaasa kusimamia ndoto zao lkatika kongamano lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita chuoni hapo

Wanafunzi wa chuo cha kilimanjaro wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo lililowezeshwa na Taasisi ya Fedha mwsihoni wa wiki iliyopita

Baadhi ya  washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji katika kongamano hilo lilifnayika mwisho wa wiki iliyopita chuoni hapo Sinza Mapambano ,Jijini Dar es salaam.

DAWASCO YAFUTA ADHA YA MIAKA 10 YA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI ENEO LA SALASALA JIJINI DAR

Meneja wa mkoa wa Dawasco -Tegeta Alpha Ambokile akizungumza na wakazi wa mtaa wa Upendo Salasala jijini Dar es Salaam ambao wameanza kupata huduma ya maji safi katika maeneo yao. 
  Bomba likitoa maji katika moja ya mitaa ya Salasala jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa Salasala wakimsikiliza Meneja wa Dawasco-Tegeta Alpha Ambokile (hayupo pichani) 
 Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kupatikana kwa huduma ya maji katika eneo la Salasala ambapo kwa sasa wakazi wa eneo hilo wanapata huduma ya maji.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog.

WANANCHI zaidi ya 265 wa mtaa wa Upendo, Mbezi Salasala wilayani Kinondoni wamelishukuru Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), kwa kuwafikishia huduma ya Majisafi waliyoipatia shida kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. 

Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja wa serikali za mitaa na DAWASCO, Mjumbe wa mtaa wa Upendo Bw. Robert Massawe amepongeza juhudi zilizofanywa na Dawasco za kuwapatia huduma ya Maji wananchi wa eneo lake na kwamba juhudi hizo zinaendana na kauli ya serikali ya awamu ya tano inayosema hapa kazi tu.


Akieleza historia fupi ya eneo hilo Bw. Massawe alisema tangu watu waanze kuhamia eneo hilo huduma ya Maji ilikuwa ni ya kununua kutoka mtaa mwingine wa mbali ambao ulikuwa umefikiwa na huduma hiyo ya Maji. 


“Ilifikia kipindi gharama ya kununua Maji ni kubwa kuliko gharama ya chakula, na wananchi wengi walikuwa wakitumia muda wao mwingi kuhangaika kutafuta Maji jambo ambalo lilikuwa likikwamisha kutekeleza majukumu mengine ya kujenga nchi” alisema Massawe.


Nae mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Bi. Sofia alisema; “Kweli DAWASCO imemtua mama ndoo ya Maji kichwani, sisi akina mama ndio tuliokuwa tukiteseka zaidi na suala la Maji, lakini akina mama wa mtaa huu tulijitoa ili kupambana na janga la Maji ambalo lilikuwa likitukabili, na hatimaye tumefanikiwa kupata huduma ya Maji” 


Kwa upande wa Dawasco, Meneja wa Mkoa wa Tegeta, Bw. Alpha Ambokile amewataka wakazi wa mtaa huo kujitokeza kwa wingi kufanya maombi ya kuungiwa huduma ya Maji kwa kuwa tayari huduma hiyo imefika katika makazi yao, baada ya kuhangaika kwa muda mrefu wakisaka huduma hiyo, na ameahidi kuwaunganishia huduma Maji mapema na kwa uharaka zaidi, mara tu baada ya kupokea maombi yao ya kuungiwa huduma.


“Ninawaomba mjitokeze kwa wingi ili kwa pamoja tuweze kuwaunganishia huduma ya Maji, nitawatengea siku yenu maalum ambayo timu yangu ya ufundi itakuja kuwafanyia maunganisho ya Maji, ambao bado hamjafanya maombi, fanyeni haraka ili tuweze kuwaunganishia wote kwa pamoja huduma ya Maji” alisema Ambokile


PICHANI: Sehemu ya wakazi wa mtaa wa Upendo, Mbezi salasala wakiwa na Mjumbe wa mtaa huo, Bw. Robert Massawe (aliyevaa shati ya bluu), wakisikiliza kwa makini katika kikao cha pamoja na uongozi wa Shirika la Maji safi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO) kutoka mkoa wa Tegeta, baada ya mtaa huo kufikiwa na huduma ya Majisafi na salama kwa mara ya kwanza tangu waanze kuhamia katika makazi hayo, jijini Dar es salaam.