Pages

KAPIPI TV

Tuesday, August 2, 2016

WAUMINI WA KKKT MTAA WA KULASI WILAYANI KOROGWE WAJENGEWA KANISA JIPYA.

Muonekano wa Jengo la Kanisa lililokuwa likitumiwa na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe .
  Muonekano wa Jengo jipya la Kanisa linalotumiwa na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe .
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe wakiandamana wakati wa sherehe ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa lililojengwa na wazawa wa kijiji hicho waishio maeneo mbalimbali nchini.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga (wa kwanza kushoto) akiongoza wachungaji wa kanisa hilo kupokea waumini wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akiongoza ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Baadhi ya Waumini wa kanisa hilo wakiimba nyimbo wakati wa  ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akikata utepe kufungua rasmi jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akifungua mlango wa kanisa ili waumini wapate kuingia ndani.
Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Kanisa la KKKT mtaa wa kulasi.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akisoma neno mara baada ya waumini kuingia ndani ya kanisa hilo.
Waumini wa kanisa la Mtaa wa Kulasi wakiwa wameshika kuta za kanisa hilo wakati wa sala ya kubariki jengo la kanisa.
Baadhi ya waumini wa kanisa la mtaa wa Kulasi wakiwa katika ibada hiyo .
Kwaya Walawi ya jijini Arusha ikiimba nyimbo za kusifu  kwa watu waliojitoa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
Mchungaji Kiongozi .........akitoa salamu kwa wauimini waliohudhuria ibada hiyo maalumu ya ufunguzi wa kanisa hilo.
Kwaya ya watoto wa kanisa la mtaa wa Kulasi wakiiiomba nyimbo wakati wa ibada hiyo.
  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akitoa mahubiri katika ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akimpa mkono Sayuni Shelutete kwa kushiriki katika utoaji wa msaada wa ujenzi wa kanisa hilo.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akimpa mkono Pascal Shelutete kwa kushiriki katika utoaji wa msaada wa ujenzi wa kanisa hilo.
Waumini wa kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe wakitoa zawadi kwa familia ya Pascal Shelutete kwa msaada waliotoa kwa ajili ya kufanikisha kazi ya ujenzi wa kanisa la mtaa wa Kulasi.
Kiongozi wa familia ya Mzee Shelutete,Bwana Nicolaus Kingazi  akizungumza  kwa niaba ya familia hiyo wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akihitimisha ibada ya ufunguzi wa kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akipeana mikono na wachungaji mara baada ya kumaliza ibada ya ufunguzi wa jengo la kanisa.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akisaidiana na Pascal Shelutete kuotesha mti wa kumbukumbu katika viunga vya kanisa hilo.
Bwana,Pascal Shelutete (Kushoto) na Bibi Sayuni Shelutete (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga mara baada ya kukamilika kwa ibada ya ufunguzi wa kanisa jipya la mtaa wa Kulasi.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

SHIRIKA LA HIFADHI ZA TAIFA(TANAPA) LAKABIDHI JENGO LA BWALO LA CHAKULA KATIKA SHULE YA SEKONDARI MWIKA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakitia saini hati ya makabidhiano ya jengo la Bwalo la chakula katika shule ya sekondari ya Mwika jana wilayani Moshi,Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Tanapa kwa kushirkiana na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na nguvu za wananchi ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil  186,494,890 zimetumika..
Baadhi ya Wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mwika wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo la Bwalo kwa ajili ya Chakula.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi hati ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq baada ya saini hati ya makabidhiano ya jengo la Bwalo la chakula katika shule ya sekondari ya Mwika jana wilayani Moshi,Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Tanapa kwa kushirkiana na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na nguvu za wananchi ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil  186,494,890 zimetumika..
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq akizindua jengo la Bwalo la chakula katika shule ya sekondari ya Mwika jana wilayani Moshi,Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirkiana na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na nguvu za wananchi ,ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil  186,494,890 zimetumika.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi
Baadhi ya Wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Mwika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq akizungumza mara baada ya kuzindua jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya sekondari ya Mwika lililojengwa kutokana na msaada wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) .
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya jengo la Bwalo la kulia chakula kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwika.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya sekondari ya Mwika lililojengwa kwa msaada wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa ushirikiano na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na wananchi .

Na Dixon Busagaga wa Michzu Blog ,Kanda ya Kaskazini.

 

ESRF YAWAKUTANISHA WADAU MBALIMBALI KUICHAMBUA BAJETI YA SERIKALI KATIKA SEKTA YA AFYA NA VIWANDA

TAASISI ya Utafiti ya Uchumi na Jamii (ESRF) imewakutanisha wasomi na wawakilishi wa taasisi za umma na kibinafsi kuchambua bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Sekta ya Afya na Viwanda ili kuona inavyoweza kutatua changamoto zinazokabili Sekta hizo kwenye mdahalo uliokutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi na kufanyika makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Akifungua mdahalo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Dkt.Tausi Kida alisema, Taasisi yake imeona ni vema kuwakutanisha wadau kujadili bajeti hiyo katika sekta ya Afya na Viwanda, kwa vile zinagusa uchumi wa wananchi.

Akiwasilisha mada juu ya bajeti ya Serikali 2016/2017na changamoto zinazoikabili sekta ya Afya, Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi, Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja alisema, ingawa bajeti iliyotengwa kwenye sekta ya Afya ni kubwa, lakini bado kuna changamoto kadhaa kwa vile Wizara hiyo imepanuka kutokana na kuhudumia maeneo mengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF), Dkt.Tausi Kida, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mdahalo uliolenga kujadili changamoto zinazoikabili bajeti ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Afya na Viwanda, kwenye makao makuu ya ESRF jijini Dar es Salaam. Mdahalo huo umewakutanisha wasomi, wawakilishi wa Taasisi za Umma na Binafsi. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).

Profesa Mujinja alitolea mfano wa ununuzi wa madawa ambapo, zaidi ya asilimia 90 ya madawa yanayotumika huagizwa kutoka nje na hivyo fedha nyingi za kigeni hutumika.

Katika majumuisho yake, Profesa Mujinja alisema, ni vema Serikali ielekeze nguvu zake kwenye uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha madawa na vifaa tiba hapa nchini ili kwenda sambamba na malengo ya taifa ya maendeleo endelevu.

Akizungumzia kuhusu changamoto za bajeti kwenye eneo la Viwanda, muwasilisha mada Profesa Prosper H. Ngowi kutoka Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, alisema, fedha zilizotengwa kwenye Sekta ya Viwanda ni Shilingi Bilioni 81, 871,992,000, ambapo asilimia 51 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na asilimia 49 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo.

Kwa mtazamo wake, Profesa Ngowi alisema, mgawanyo huo ni mzuri na sio kwa kiwango kikubwa kwani hakuna tofauti na bajeti ya mwaka 2015/2016, na kuonyesha wasiwasi wake muda ambao Serikali inatoa fedha hizo kuhudumia maeneo yaliyokusudiwa.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS), Cha Muhimbili, Profesa Phares Mujinja, akitoa mada juu ya changamoto zinazoikabili bajeti ya Serikali ya 2016/2017 kwenye Sekta ya Afya wakati wa mdahalo huo.

“Bajeti ya 2016/2017 ni Asilimia 70.3% ya ile ya 2015/2016 na kwamba wizara hivi sasa ni kubwa kutokana na kuongezeka kwa sekta ya Uwekezaji.” Alifafanua.

Wakichangia mada hizo, wengi wa washiriki wameonyesha wasiwasi wao kuhusu kufanikiwa kwa malengo ya serikali kwenye Sekta hizo kutokana na muonekano wa bajeti yenyewe na mahitaji halisi ya sasa ya utoaji huduma kwenye Sekta hizo ili kufikia malengo ya kukuza uchumi wa nchi kumekuwepo kwa mtazamo kuwa biashara nchini zinaanguka kutokana na mkazo wa kukusanya mapato.

Akifunga mdahalo huo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo wa ESRF, Doris Likwelile, aliwashukuru washiriki kwa michango yao mbalimbali na kwamba mawazo yao yatawezesha utayarishaji wa mtazamo wa wadau kwenye Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye Sekta hizo mbili za Afya na Viwanda.
Edith Mackenzie, akichangia kwenye mdahalo huo.
Mkuu wa Program ya Taarifa na Utafiti kutoka TGNP, Gloria Shechambo akishiriki kwenye mdahalo huo.
Mkurugenzi wa SIKIKA, Irinei Kiria, akichangia mawazo yake kwenye majadiliano hayo.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi, akiwasilisha mada ya changamoto zinazoikabili bajeti ya serikali ya mwaka 2016/2017 kwenye sekta ya Viwanda hapa nchini, wakati wa majadiliano yaliyowaleta pamoja wasomi na wawakilishi wa taasisi za Umma na Binafsi kwenye ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam. Majadiliano hayo yaliandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii, (ESRF).
Dkt. Kida akichangia baadhi ya hoja za washiriki na watoa mada. Kushoto ni Profesa Prosper Ngowi.
Baadhi ya washiriki wa majadiliano hayo.

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala na Ujenzi wa Maendeleo wa ESRF, Doris Likwelile, akitoa hotuba ya kufunga mdahalo huo.
Afisa Mpipango Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, (TPA), Alfred Matuntera, (kushoto0, akizungumza jambo mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida, (kulia), Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Afya Shirikishi Cha Muhimbili, (MUHAS), Profesa Phares Mujinja, (wa pili kulia), na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Prosper Ngowi.

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE AUNGANA NA WATENDAJI WAKE KUSAMBAZA MAPIPA YA KUWEKEA TAKA BARABARA YA KIVUKONI JIJINI DAR

tem01Mkuu wa wilaya ya Illala Mh. Sophia Mjema akiongozana na Edward Mpogolo Katibu Tawala wa wilaya hiyo wakati walipoongoza zoezi la kusambaza mapipa ya kuwekea takataka kwenye barabara ya Kivukoni jijini Dar es salaam kwa ajili ya udhibiti wa utupaji wa taka hovyo.
tem1
Mkuu wa wilaya ya Illala Mh. Sophia Mjema katikati akiongozana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Bw.Msongela Palela kushoto pamoja na Edward Mpogolo Katibu Tawala wa wilaya hiyo weka mapipa ya kuhifadhia takataka katika barabara ya Kivukoni jijini Dar es salaam.
tem2Mkuu wa wilaya ya Illala Mh. Sophia Mjema akiongozana akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala juu ya mpangilio wa uwekaji wa mapipa ya kuhifadhia takataka kwenye barabara ya Kivukoni jijini Dar es salaam jana.

SINAI MISSIONS INTERNATIONAL (SMI) YAFANYA MKUTANO WAKE MKUU WA MWAKA KWA MAFANIKIO MAKUBWA

????????????????????????????????????Mgeni rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania, Bishop Dr Kameta (katikati) akizungumza na wanachama wa Shirika la kidini linalotoa huduma kwa makanisa na mashirika yanayofanya kazi ya kueneza injili ulimwenguni lijulikanalo kama SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI) wakati wa mkutano mkuu wa mwaka uliofanyika jijini Dar es Salaam Lengo la mkutano huo ilikuwa ni kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI. kulia ni Rais wa shirika hilo Ing.Bishop Piter M.Sanga.na kushoto Katibu Mkuu anaemaliza muda wake Bishop Pite W.Chinyama kutoka Zambia.na Mweka Hazina anayemaliza muda wake Msh Raphael Muhagama kutoka Tanzania.
????????????????????????????????????Wajumbe wa Mkutano.
????????????????????????????????????Mkutano ukiendelea.
????????????????????????????????????????????????????????????????????????Wajumbe wa mkutano mkuu wa mwaka wakifuatilia mada mbalimbali.
????????????????????????????????????Viongozi wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano mkuu wa mwaka kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
????????????????????????????????????Wajumbe wa mkutano wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio.
????????????????????????????????????Wajumbe wa mkutano mkuu wakimtukuza Mungu kwa wimbo wa pambio wakati wa mkutano mkuu wa mwaka kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
????????????????????????????????????Mgeni Rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Bishop Dr Kameta (kushoto), pamoja na Mtafisiri ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirika la MSI, Bishop Gilibert Biyengo.wakihutubia Mkutano Mkuu wa Mwaka.
????????????????????????????????????Mgeni rasmi kutoka Baraza la Makanisa ya Kipentekosite, Bishop Dr Kameta (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa SINAI MISSIONS INTERNATIONAL(SMI) uliofanyika jijini Dar es Salaam kwaajili ya kupeana taarifa za utendaji wa SMI na kila huduma chini ya mwavuli wa SMI.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG

MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA MKOANI MWANZA AANZA ZIARA ZA KUKAGUA MIUNDOMBINU JIMBONI HUMO

Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza ambae pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula (katikati), jana amefanya ziara ya kukagua Ukarabati wa Miundombinu ya barabara, mitaro na madaraja katika Kata ya Kirumba Jimboni humo ikiwa ni mwanzo wa ziara zake katika Kata zote za Manispaa ya Ilemela ili kujionea namna ukarabati wa mbiundombinu ya barabara unavyoendelea.

Kulia ni Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua ambapo miongoni mwa barabara zinazokarabatiwa katika Kata ya Kirumba ni barabara ya Villa, Kabuhoro, CWT-Sabatho.
Na BMG
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa nne kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Mitaro katika barabara ya Villa inaendelea kukarabatiwa ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua na kusababisha adha kubwa kwa wananchi.
Hii ni barabara ya CWT-Sabatho, awali ilikuwa haitamaniki kwani ilikuwa ni mashimo tupu. Lakini sasa inapitika vyema na kilichosalia ni ukarabati wa mitaro ili mvua ikinyesha isiweze kusababisha uharibifu wa ukarabati huu.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (wa tatu kulia), akiwa katika ziara ya kukagua ukarabati wa mbiundo mbinu katika Kata ya Kirumba Jimboni humo.
Namna miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Ukaguzi wa miundombinu ya barabara na mitaro inavyoendelea kukarabatiwa katika Kata ya Kirumba, Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.
Pia kuna ujenzi wa daraja katika barabara ya Kabuhoro Ziwani ambapo kulikuwa na adha kubwa kwa wananchi ambapo ukarabati huu unaleta ahueni kwa wakazi wa eneo hio pamoja na watumiaji wengine wa barabara.

Aliagiza ukarabati wa mbiundombinu ya barabara kukamilika haraka kabla msimu wa mvua haujaanza na kwamba Manispaa ya Ilemela imetenga Shilingi Milioni 625 ikiwa ni fedha za mfuko wa dharura na shilingi Milioni 146 ambazo ni fedha za mfuko wa barabara, fedha zote ikiwa ni kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (mwenye miwani) akiteta kidogo na wakazi wa Kata ya Kirumba alipotembelea Kata hiyo ili kujionea ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata hiyo.
Katibu wa Mbunge, Heri James (mwenye kofia) ambapo alisema ofisi ya mbunge itahakikisha ahadi zilizotolewa na mbunge wakati wa kampeni zinatekelezwa ikiwemo suala la upatikanaji wa maji na ukarabati wa miundombinu.
Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, akitoa taarifa ya ukarabati wa miundombinu katika Kata ya Kirumba ambapo alibainisha kwamba zaidi ya Shilingi Milioni 195 zimetengwa kwa ajili ya Kata hiyo ili kukarabati barabara zake ambazo ziliharibika kutokana na mvua.
Diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, ambapo alibainisha kwamba barabara za Kata hiyo zilikuwa zimeharibika sana kutokana na mvua zilizonyesha mwishoni mwanza mwaka jana. 

Alishukuru ushirikiano baina yake na wananchi wa Kata yake, ofisi ya mbunge pamoja na halmashauri ya Manispaa ya Ilemela na kwamba juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano katika kuwafikishia wananchi maendeleo zimepokelewa vyema na wananchi huku akiwasihi kuitunza vyema miundombinu hiyo.
Mmoja wa wakazi wa Kirumba akieleza adha waliyokuwa wakiipata wakazi wa Kata hiyo kabla ukarabati haujafanyika ambapo aliongeza kwamba ni vyema ukarabati huo ukaendelea kufanyika hususani katika ujenzi wa mitaro ili kuondoa adha ambayo huwa inajitokeza wakati wa mvua ikwemo kuharibu miundombinu ya barabara kutokana na kukosekana kwa mitaro.
Mkazi wa Kirumba akitoa shukurani zake kwa ukarabati unaofanyika katika barabara za Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, imeanza ukarabati wa miundombinu ya barabara kwa kiwango cha changarawe pamoja na mikakati ya ujenzi wa baadhi ya barabara kwa kiwango cha lami.

Akikagua zoezi la ukarabati wa miundombinu ya barabara katika Kata ya kirumba, Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Angelina Mabula, ametaka ukarabati wa miundombinu hiyo ikiwemo mitaro, kukamilika mapema kabla msimu wa mvua haujaanza ili kuepukana na athari za mvua.

Amesema katika kipindi cha miaka mitano, hali ya miundo mbinu ya barabara katika jimbo hilo itakuwa katika hali nzuri na hivyo kupunguza kero ya ubovu wa miundombinu ambayo imekuwepo kwa muda mrefu katika Manispaa ya Ilemela.

Mhandisi wa Manispaa ya Ilemela, Mikidadi Adam, amesema Manispaa hiyo imetenga shilingi Milioni 625 zilizotokana na fedha za mfuko wa dharura na barabara kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara katika manispaa hiyo japo amebainisha kwamba bado fedha hizo hazitoshi hivyo ni vyema serikali ikaendelea kutenga fedha zaidi kwa ajili ya kutekeleza ukarabari huo.

Wakati ukarabati huo ukiendelea, diwani wa Kata ya Kirumba, Alex Ngusa, amewataka wananchi kutunza vyema mbiundombinu ya barabara inayoendelea kukarabatiwa ikiwa ni pamoja na kuacha tabia ya kutupa taka kwenye mitaro.

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Kirumba, wamepongeza juhudi za ukarabati wa miundombinu ya barabara zinazofanyika katika Manispaa ya Ilemela na kuongeza kwamba ni vyema juhudi hizo zikandelea ili kumaliza kero zilizokuwepo awali.

Mbunge wa Jimbo la Ilemela, yuko katika mwendelezo wa ziara katika Kata zote 19 za Manispaa ya Ilemela ili kujionea ukarabati wa Miundombinu ya barabara ambayo ni pamoja na ujenzi wa mitaro na madaraja ambao unaelezwa kuleta ahueni kwa wananchi wa Manispaa hiy ikizingatiwa kwamba awali hali ya miundombinu ya barabara awali haikuwa ya kuridhisha.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.