Pages

KAPIPI TV

Tuesday, August 2, 2016

WAKURUGENZI MKOANI SIMIYU WAAGIZWA KUTENGA BAJETI ZA MAAFISA KILIMO

  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo wa mkoa huo(hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (katikati) akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo wa mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kikiwa na lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu, (kushoto) Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Bw. Donatus A. Weginah na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga
Viongozi na Maafisa kilimo wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anthony J. Mtaka (hayupo pichani) katika kikao kilichofanyika mjini Bariadi kwa lengo la kujadili mwelekeo wa sekta ya kilimo kama kipaumbele cha pili Mkoani Simiyu kwa mwaka huu.


         Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Simiyu)

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani humo kutenga bajeti kwa ajili ya kuwawezesha Maafisa kilimo wa Vijiji,Kata na Wilaya kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipokuwa akizungumza na Viongozi na Maafisa Kilimo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi ambacho kilihudhuriwa na Wakuu wa wilaya,Wenyeviti wa Halmashauri,Wakurugenzi na Makatibu Tawala Wilaya kutoka  katika wilaya zote tano za mkoa huo.

Mtaka amesema Maafisa Kilimo wanapaswa kuwezeshwa kwa kupewa vyombo vya usafiri kama pikipiki na magari pamoja na mafuta, ili waweze kuwafikia wakulima katika maeneo yao kwa ajili ya kuwapa ushauri wa kitaalam kila wanapowahitaji katika kuendeleza kilimo bora na chenye tija.

“Mwaka huu kilimo kwa mkoa wetu ni  kipaumbele cha pili na Halmashauri za Mkoa huu zinategemea kilimo kwa takribani asilimia 90 ya mapato yake ya ndani, ipo haja  kuwawezesha maafisa kilimo kwa kuwa wana mchango kubwa katika mapato ya Halmashauri. Ningependa kuona mwaka 2016/2017 hadhi ya Maafisa Kilimo inapanda, Wakurugenzi muwathamini hawa wataalam ndiyo wanaowasaidia kupata hayo mapato katika pamba, choroko, dengu, mpunga na mazao mengine”, alisema Mtaka.

Aidha, kufuatia makubaliano kati ya Serikali ya  Tanzania na India yaliyofanywa hivi karibuni kati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu wa India juu ya biashara ya mazao ya jamii ya mikunde kama choroko, dengu na mbaazi takribani tani milioni sita, Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu unayo fursa kubwa ya  kuzalisha mazao haya kwa takribani asilimia 60 kama ilivyo katika zao la pamba, kwa kuwa kuna ardhi yenye rutuba na wananchi wanalima mazao hayo. 

Katika kufikia azma hiyo, Mtaka amewataka Maafisa kilimo kutumia muda huu kufanya tafiti katika vituo mbalimbali vya utafiti  juu ya mbegu bora, kabla ya msimu wa mazao ya mikunde haujaanza ili wakati utakapofika uzalishaji wa mazao hayo ufanyike kitaalam na kuongeza uzalishaji kuliko ilivyo sasa.

Wakati huo huo Mtaka amewaagiza viongozi na Maafisa Kilimo kutoka katika wilaya zote kuwa na mashamba ya mifano ambayo yatatumika kama mashamba darasa kwa wananchi ili wananchi wajifunze kutoka kwao kwa kuwaonesha kuwa maelezo wanayoyatoa yanatekelezeka. 

Kwa upande wake Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulikia Uchumi na Uzalishaji katika Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Bw. Joseph Nandrie ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Simiyu kulima mazao yanayostahimili ukame kama mihogo na mtama ili kukabiliana na baa la njaa.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akikiri kupokea maelekezo ya Mkuu wa Mkoa amewataka Maafisa Kilimo kuandaa mipango kazi kwa ajili ya utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na kuyawasilisha kwa viongozi wao wa wilaya ili yaanze kutekelezwa.

Jumla ya Maafisa kilimo 203 kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Busega, Itilima, Maswa , Meatu na Halmashauri ya Mji  Bariadi wameshiriki katika kikao hiki ambacho kililenga kutoa mwelekeo wa Sekta ya Kilimo kama kipaumbele cha Pili Mkoani Simiyu kwa mwaka 2016/2017.

SIA PIUS NDIYE WINDHOEK DRAUGHT MISS SINZA 2016

 Windhoek Draught Miss Sinza 2016, Sia Pius (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Catherine Listoni (kushoto) na mshindi wa tatu Hafsa Mahamood baada ya kutangazwa mshindi Hoteli ya Defrance lilikofanyika shindano hilo jana usiku kwa udhamini wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd kupitia kinywaji wa Windhoek.
 Mwakilishi wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd akisema chochote kwenye shindano hilo.
 Mtoa huduma wa kampuni hiyo akitoa huduma kwa wadau wa windhoek.
 Wadau wa Windhoek ndani ya Defrance Hotel katika shindano hilo.
 Hapa ni windhoek tu kwa kwenda mbele.
 Wadau wa windhoek wakiwa kwenye shindano hilo.


 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Jerome Rugemalira (kushoto), akigongesha chupa ya windhoek na mdau wa kinywaji hicho, iliyokatika muonekano mpya katika shindano hilo.
 Wacheza shoo wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia wakishambulia jukwaa katika shindano hilo.
 Wasanii wa kampuni ya mabibo wakionesha umahiri wa kucheza wakati wa shindano hilo.
 Washiriki wa shindano hilo wakijitambulisha kwa kucheza kabla ya kuanza kwa shindano hilo.
 Wanenguaji wa Bendi ya FM Academia wakiwa kazini.

 Washiriki wakiwa katika vazi la ubunifu.
 Majaji wa shindano hilo wakiwa kazini.
 Baadhi ya washiriki ambao hawakufanikiwa kuingia tano bora.
 Warembo walioingia tano bora. Kutoka kulia ni Catherine Listone, Sia Pius, Hafsa Mahamood, Saida Khalifa na Faith Msuya.
 "Jamani tuchangechange mapene tuongeze windhoek meza imekauka hapa"
 Hapa ni furaha tu kwa kusonga mbele.
 Majaji wakiwa tayari kuwatangaza washindi.
 Mdau wa Windhoek na mashindano ya Miss Tanzania, Rutha Lucas akitoa sh.100,000 kwa kila mshiriki wa shindano hilo ikiwa ni kifuta jasho.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto),  akimkabidhi mshindi wa kwanza wa shindano hilo kitita cha sh.500,000.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mabibo Beer Wine and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira (kushoto), akimkabishi mshindi huyo moja ya katoni ya windhoek kati ya tano zilizotolewa na kampuni hiyo kwa mshindi huyo ambapo pia mshindi wa pili na watatu walikabidhiwa.

Na Dotto Mwaibale

KAMATI ya maandalizi ya shindano la Miss Sinza 2016 imemtangaza Sia Pius kuwa mshindi wa Windhoek Draught Miss Sinza 2016 baada ya kuibuka mshindi katika shindano lililofanyika Hoteli ya Defrance iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam jana usiku.

Pius aliibuka mshindi baada ya kuwabwaga washiriki wenzake tisa waliokuwa wakiwania taji hilo ambapo nafasi ya pili ilichukuliwa na Catherine Listoni huku ya tatu ikichukuliwa na Hafsa Mahamood.

Shindano hilo lilidhaminiwa na Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spiritis kupitia bia ya Windhoek pamoja na wadhamini wengine.

Mshindi wa kwanza wa shindano hilo alizawadiwa sh.500,000 wakati wa pili akijipatia sh.300,000 na watatu akiondoka na kitita cha sh.200,000 huku washiriki wengine wakiondoka na kifuta jasho cha sh.100,000 kila mmoja.

Washindi hao watatu wataingia moja kwa moja katika shindano la kumsaka Miss Kinondoni 2016 litakalofanyika mwezi ujao.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)


Friday, July 29, 2016

MAALIM SEIF KUONGEA NA WATANZANIA BOSTON JULY 30

Zanzibar Diaspora Association inapenda kuwaalika kwenye mkutano wa hadhara utakao fanyika Siku ya Jumamosi July 30th -
MAHALI: 42 Charles St Boston
MA 02122.
MDA: Kuanzia 5:pm mpaka 7:pm
Mgeni rasmi ni Katibu mkuu wa CUF. 
Maalim Seif Shariff Hamad
Nyote mnakaribishwa