Pages

KAPIPI TV

Friday, July 29, 2016

MAHAKAMA KUU KANDA YA TANGA YATUPILIA MBALI SHAURI LA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA PANGANI



Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso katika akipongezwa na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kutangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kuwa mshindi halali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau


Mbunge Aweso Jumaa akiwa amebebwa juu juu na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kesi iliyofunguliwa dhidi ya mpinzania wake wa CUF Amina Mwidau ya kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Tanga

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga jana imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Pangani lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia tiketi ya  CUF Amina Mwindau dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Hamidu Aweso CCM  na kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo.
Akizungumza wakati akitoa huduma ya Shauri hilo,Jaji Patricia Fikirini alisema mlalamikaji Amina Mwindau CUF ameonekana kushindwa katika shauri hilo dhidi ya mlalamikiwa Jumaa Aweso katika upingaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika oct  25 mwaka jana.

Alisema miongoni mwa malalamiko yalioambatanishwa kutoka kwa
mlalamikaji katika zoezi zima la kupinga matokeo hayo ni pamoja na kuwa mlalamikiwa ambae ni Jumaa Aweso katika kampeni zake alikiuka taratibu za uchaguzi,ubaguzi wa mgombea wa jinsia ya kike na kutumia lugha ya siziokuwa za kiungwana jambo ambalo mlalamikaji alidai lilimgharimu kupata matokeo mazuri katika uchaguzi huo.

Alisema sambamba na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo pamoja na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mlalamikaji havikuwa na ushawishi wa kuweza kutengua matokeo ya uchaguzi huo.

Jaji Fikirini alisema amezingatia hoja zote kutoka pande mbili na
kujiridhisha Jumaa Aweso ambae ni mbunge hivi sasa kuwa ni mbunge aliyepita kihalali na hakukuwa na vigezo vya upingwaji wa matokeo aliyopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Alisema haki zote za kisheria zipo wazi kwa pande zote mbili
mlalamikiwa na mlalamikaji ikiwa pamoja na kukata rufaa kwa maamuzi yaliyochukuliwa na Mahakam hiyo ikiwa kama kuna upande hauta ridhika na hukumu iliyotolewa.

Kwa upande wake  Wakili wa kujitegemea na mahakama kuu Warehema Kibaha alisema Jaji Patisia Fikirini amefanya maamuzi sahihi ya kutenda haki kwa mteja wake katika shauri hilo lililo dumu kwa takriban miezi 7.

Wakili Kibaha alisema katika shauri hilo walijiandaa kwa ushahidi  na mashahidi wazuri ili kuweza kukabiliana na kesi hiyo jambo ambaloliliwawezesha kupata ushindi wa kihalali na kuweza kumpa nafasi mteja
wake kuendelea na majukumu yake ya Kibunge.

Nae Wakili Mashaka Ngole aliyemsimamia Mlalamikaji Amina Mwindau alisema hana pingamizi lolote na  atamsikiliza mteja wake ikiwa ataamua kukata rufaa wataangalia vigezo muhimu vitakavyo wasaidia katika awamu ya pili pindi watakapo kata rufaa hiyo

Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ambaye alikuwa anakabiliwa katika shauri hilo alisema kipindi chote alichokuwa anakabiliana na kesi hiyo kulimpotezea umakinifu wa kufanya majukumu yake ya kibunge na kuweza kuangalia shida za wananchi wa Pangani kwa umakini zaidi.

Aweso alisema kesi imekwisha na sasa kilichombele yake ni kupambana na kero za wananchi wa Wilaya hiyo ili kuweza kuwaletea maendelo kama alivyowaahidi kipindi cha kampeni.
 
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

RATIBA YA USAJILI MAISHA PLUS EAST AFRICA 2016

Baada ya Usaili kufanyika kwa kishindo katika mikoa ya Mtwara na Dar es salaam usaili wa Maisha Plus unaendelea katika mikoa mingine ndani ya Tanzania. 
30/07/2016 - MBEYA - Ukumbi wa City Pub 
31/07/2016 - IRINGA - Savanna Garden 
02/08/2016 - DODOMA - Matei Lounge 
04/08/2016 - MWANZA - Rock Garden 
06/08/2016 - ARUSHA - Via Via
 13/08/2016 - ZANZIBAR - Ngome Kongwe 


Vijana wote wenye umri wa miaka 18 - 26 wanakaribishwa kujitokeza kwa wingi. Elimu na ujuzi ni kiwango chochote. Zawadi kwa mshindi ni Tzshs. Milioni 30. Fomu zinapatikana BURE kabisa kupitia www.maishaplus.tv na katika maeneo tajwa hapo juu. 

 Maisha Plus East Africa 2016 | #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
   
 Bofya hapa chini kuona video 33 fupi za usaili wa Maisha Plus Dar es salaam.

Thursday, July 28, 2016

HOMA YA INI B NA C KUTOKOMEZWA IFIKAPO MWAKA 2030

 Baadhi ya vijana waliokuwa wakitumia dawa za kulevya wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa kutokomeza homa ya ini wakielekea kwenye  maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo mchana.
 Bango likihimiza kuungana kutokomeza homa ya ini.
 Maandamano yakiendelea kuelekea viwanja vya Mwembe Yanga. Katikati ni Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan.
 Vijana waliopo kwenye mtandao wa kupinga matumizi ya dawa za kulevya wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mratibu wa Mtandao wa Watu Wanaotumia Dawa za Kulevya (TANPUD), Happy Assan, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa TanPud Tanzania, Godfrey Ten, akizungumza katika maadhimisho hayo.



 Ofisa Maendeleo ya Jamii, Mratibu wa Asasi za Kiraia kutoka Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya Tanzania, Salome Mbonile, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mwakilishi wa Taasisi ya Pasada, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
 Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo.

 Maadhimisho yakiendelea.
 Vijana waathirika na dawa za kulevya wakicheza kwenye maadhimisho hayo.
 Meneja wa Afya  Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde akizungumza kuhusu ugonjwa huo.
Wageni waalikwa katika picha ya pamoja.

Dotto Mwaibale

UGONJWA wa homa ini umepangwa kutokomezwa ifika mwaka 2030 imefahamika ambapo watu wapatao  milioni 1.4 upoteza maisha ulimwenguni kutokana na maambuki ya ugonjwa huo ulimwenguni hasa kwa wale wanaotumia mihadarati kwa njia ya kujidunga.

Hayo yalibainishwa na Mratibu wa Afya- Dawa za kulevya wa Manispaa ya Temeke, Mwajuma Mwihumbo kwa niaba ya Meya wa Manispaa hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya homa ya ini yaliyofanyika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam jana.

Alisema kuna umuhimu mkubwa wa kuongeza ufahamu kuhusu na kuungana na juhudi za ulimwengu za kutokomeza homa ya ini.

Alisema mada ya kampeni ya kimataifa ya homa ya ini ya mwaka huu ni utokomezaji ambao ni mwaka muhimu kwa homa ya ini.

Alisema lengo la maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na asasi za kiraia, wafanyakazi wa huduma za afya, taasisi na vikundi vya utetezi na ushawishi ni kuongeza ufahamu wa homa ya ini B na C hasa kwa makundi hatarishi kama watumiaji wa mihadarati wanaojidunga.

Meneja wa Afya  Madaktari wa Dunia Dk. Faith Aikaeli kutoka Taasisi ya Medicins Du Monde alisema katika mkutano mkuu wa 69 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) ni serikali zote ziliazimia kwa pamoja kuidhinisha mkakati wa ulimwengu wa utokomezaji wa homa ya ini.

Alisema hadi Februari 2016 nchi 36 zilikuwa zina mipango ya kitaifa ya utokomezaji wa homa ya ini na nchi 33 zipo katika mikakati ya kuandaa mipango hiyo.

"Mkakati unalenga kutokomeza homa ya ini B na C ifikapo mwaka 2030 ambapo unahusisha malengo ya tiba ambayo iwapo yatafikiwa yatapunguza vifo vinavyosababishwa na homa ya ini kwa asilimia 65 na kuongeza huduma ya tiba kwa asilimia 80 hivyo kuokoa maisha ya watu milioni 7.1 ifikapo mwaka 2030"  alisema Dk.  Aikaeli

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)





NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI AFANYA KIKAO NA VIONGOZI WA HIFADHI YA TAIFA YA RUBONDO

Naibu Waziri wa Maliasilili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ,akiviishwa vazi maalum (Boya) ambalo hutumika kujiokoa wakati uafiri wa maji unatumika.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani akiingia kwenye Boti kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Misana Mwishawa akimueleza jambo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani wakati akitembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi hiyo.
Mamba ni moja ya vivutio katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo ambayo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani alivutiwa kuwatizama.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitizama vivutio mbalimbali wakati akizunguka na boti maalumu katika visiwa vilivyoko Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Missana Mwishawa akimuonesha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani eneo ambalo ni makazi na mazalia ya ndege katika moja ya visiwa vilivyoko katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi alikuwa ni mmoja wa viongozi walioongozana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhandisi Ramo Makani kazika ziara hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizunbgumza jambo mara baada ya kupata maelezo mbalimbali kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Misana Mwishawa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akitia saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika hoteli ya Asilia Lodge iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa akizungumza wakati wa kikao kifupi cha Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili ,Mhandisi Ramo Makani na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini,Joseph Kasheku (Msukuma) akizungumza wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Geita,Herman Kapufi akizungumza katika kikao hicho.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na viongozi wa serikali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Geita pamoja na viongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipokutana nao katika Hoteli ya Asilia Lodge.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akizungumza na mmoja wa wageni katika Hoteli ya Asilia Lodge iliyopo katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Ugeni wa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani ukipunga mikono kuaga wenyeji wao katika Hoteli ya Asilia Lodge ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

Wednesday, July 27, 2016

MBUNGE WA SEGEREA BONNAH KALUWA AREJESHA KIWANJA KWA WANANCHI WA KATA YA BUGURUNI

 Mbunge wa Jimbo la Segerea,  Bonnah Kaluwa (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo na wafanyakazi wa Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited iliyokodishwa kiwanja kilichopo nyuma ya Kituo cha Polisi Buguruni ambapo ametoa siku tatu waondoke kupisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Buguruni. Mapato ya kiwanja hicho kwa zaidi ya miaka 10 yalikuwa hayajulikani yalipokuwa yakienda.
 Ofisa Mtendaji wa Kata ya Buguruni, Remmy Mishehe (kulia), akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu kiwanja hicho.
 Maelezo zaidi yakitolewa.
 Mmoja wa mtu aliyedaiwa ni dereva wa kampuni hiyo, akidhibitiwa baada ya kudaiwa kutoa lugha ambayo siyo nzuri mbele ya mbunge wakati wa ziara ya mbunge huyo kukagua kiwanja hicho.
 Malori ya kampuni hiyo yakiwa yameegeshwa kwenye kiwanja hicho. 
Mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo akitoa maelezo kwa Mbunge Bonnah Kaluwa (kushoto). Katikati mwenye suti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Buguruni, Barua Mwakilanga.


Na Dotto Mwaibale

MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kaluwa amefanikiwa kukirejesha kiwanja kwa wananchi wa Kata ya Buguruni kilichokuwa kikitumika kuegesha magari kwa malipo bila kujulikana matumizi ya fedha hizo.

Kiwanja hicho ambacho kipo nyuma ya kituo cha Polisi Buguruni kilikuwa kimetengwa miaka mingi iliyopita kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Buguruni.

Akizungumza wakati akikagua kiwanja hicho Dar es Salaam leo asubuhi ambacho  kinatumiwa na Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited kuegesha magari yao alisema wametoa siku tatu wawe wameondoka ili waanze mara moja ujenzi wa shule hiyo ambapo jumla ya sh. milioni 40 za kuanzia ujenzi huo zimetengwa.

"Kata ya Buguruni haina shule  hata moja ya sekondari kupatikana kwa kiwanja hiki kitasaidia watoto kupata shule katika kata yao badala ya kwenda shule zingine za mbali" alisema Kaluwa.

Kaluwa aliongeza kuwa waliokuwa wakitumia kiwanja hicho waliingia mkataba na uongozi wa Kata ya Buguruni ambapo katika kipengere namba nne kilieleza kuwa ikifika wakati eneo hilo likihitajika basi mpangaji atalazimika kuondoka.

"Kwa kuwa mpangaji wa eneo hilo yupo na mkataba unajieleza wenyewe kupitia kipengere hicho tunaomba wahusika watupishe haraka iwezekanavyo tuanze ujenzi wa sekondari" alisema Kaluwa.

BENDI 10 MAARUFU ZA MUZIKI WA DANSI KUWASHA MOTO JUMAMOSI VIWANJA VYA LEADERS NI KATIKA TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA DANSI

 Mwanamuzi wa mziki wa dansi, Ali Choki akiwaongoza wenzake kutoa burudani mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda walipofika ofisini kwake leo, kuzungumzia Tamasha la muziki huo litakalofanyika Jumamosi  Viwanja vya Leaders ambalo litashirikisha bendi 10 maarufu za hapa nchini.
 Baadhi wa wadau wa muziki wa dansi na wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
 wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Mdau wa muziki wa dansi, Asha Baraka akizungumza katika mkutano huo kuhusu tamasha hilo la kukata na shoka ambalo alijawahi kufanyika hapa nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda akizungumza na wanamuziki hao kuhusu tamasha hilo la muziki wa dansi nchini.
 Mkutano ukiendelea.
RC Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wanamuziki wa dansi baada ya kuzungumza nao ofisi kwake.

(Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)