Pages

KAPIPI TV

Thursday, July 21, 2016

WANAHABARI WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika Boti wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe,hifadhi maarufu kwa kuwa na mnyama aina ya Sokwe mtu.
Watalii wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe .
Eneo mojawapo linalotumiwa na wavuvi katika mwambao mwa ziwa Tanganyika jirani na Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Baadhi ya wanahabari muda mfupi baada ya kufika hifadhi ya taifa ya Gombe.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) ,Pascal Shelutete akiwatamburisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini  walipotembelea hifadhi ya taifa ya Gombe.
Kaimu Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe,Goodluck Tarimo akizungumza na wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo.
Baadhi ya Wahifadhi waongoza wataalii katika Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Daktari wa Mifugo katika Hifdhi ya Taifa ya Gombe,Dkt Jane Raphael akizngumza mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuaza safari ya kutembelea hifadhi hiyo.
Mhifadhi Hussein 
Mhifadhi Isaya Mkude akitoa maelezo kwa wanahabari wakati wa kuanza safari ya kwenda kuwatizama Sokwe.
Safari ya kwenda kuwatizama Sokwe ikaanza.
Maeneo mengine Mhifadhi Isaya Mkude aalikua akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali na majibu ya maswali yaliyoulizwa na wanahabari.
Nyani ni miongoni mwa wanyama wanaoonekana kwa urahisi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Safari ya kuwatafuta Sokwe ili kua ni ya vipando pia.
Wakati mwingine wanahabari walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata pumzi mpya ya kuendelea na safari 
 Baadhi ya Sokwe mtu walioonekana kwa mbaali sana wakiwa katika miti.
Hatimaye safari ya kurudi katika makazi ikaanza kwa kupita katika fukwe ya ziwa Tanganyika inayopakana na hifadhi ya taifa ya Gombe. 

Na Dixon Busagaga wa Michzui Blog.

DK.KIGWANGALLA ASIMIKIWA MTEMI WA WANYAMWEZI

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amepewa heshima ya Uchifu wa Watanzania wa Kabila la Wanyamwezi na Wazee wa Kijiji cha Isalalo katika Kata ya Utwigu iliyopo katika Jimbo hilo la Nzega Vijijini Mkoani Tabora.
Dk. Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo kwa lengo la kushukuru Wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi za zilizomwezesha kuingia Bungeni, ambapo katika tukio hilo lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wanakijiji wa Kijiji hicho,
Wazee hao wa Mila walieleza kuwa, hatua hiyo ya kusimikwa Uchifu wa heshima wa kabila la Wanyamwezi ni ishara kubwa kuwa Kijana mashuhuri na kijana mpiganaji sawasawa hivyo kwa ushindi wake kuchaguliwa nahata kupewa Uwaziri (Naibu Waziri), ni ishara kubwa ya kufikia malengo yake aliyokusudia katika Taifa hili.
Wazee hao wa Mila waliweza kumkabidhi mishale, Mkuki, upinde na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kiutawala.
Akitoa shukrani zake katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Wananchi wake wategemee neema kubwa kwani kwa sasa yupo katika hatua ya utendaji kazi Zaidi na kuwataka wawe na Imani naye pamoja Serikali iliyopo madarakani kwani imejipanga kuleta maendeleo makubwa.
“Nawashukuru nyie kwa kuniwezesha kunipigia kura nyingi sana ambazo zimeniwezesha mimi kupata nafasi ya kuingia Buangeni. Nawaahidi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote. Nguvu nilizozianza tokea awali na kwa sasa zitakuwa kubwa Zaidi, muendelee kuniombea.
Nafahamu kuna kero nyingi sana, shida za barabara za kuingia na kutoka huku Vijijini, Suala la Umeme na mengine mengi haya yote yanafanyiwa kazi na taratibu zote zinaenda vizuri.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho cha Isalalo.
Ziara hiyo iliyoanza tokea Julai 13 mwaka huu, Mbunge huyo ambaye Jimbo lake hilo lenye jumla ya Kata 19, zikiwemo Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe.
Ambapo katika Vijiji vya Kata hizo amewafikia wananchi na kuwashukuru kwa hatua yao ya kumchagua ambapo pia ameweza kutekeleza ahadi aliyoitoa yeye mwenyewe ikiwemo vifaa vya michezo kwa timu za vijana, pamoja na kutimiza ahadi za michango mbalimbali ikiwemo ya kuchangia ujenzi wa shule, makanisa, misikiti, Zahanati na mambo mbalimbali huku pia akipokea maoni na uashahuri kutoka kwa wapiga kura wake hao.
DSC_2015 DSC_2023 DSC_2030Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Wanakijiji cha Isalalo
DSC_2032
Wazee wa Mila
DSC_2037
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni
DSC_2038
Wazee wa Mila wakiwa upande wa wageni maalum
DSC_2043
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akivishwa shuka katika hatua ya kusimikwa uchifu huo
DSC_2044 DSC_2047
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhiwa mkoba wa mishale
DSC_2050 DSC_2051 DSC_2054 DSC_2059
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipewa baraka na wazee hao
DSC_2083 DSC_2062 DSC_2066 DSC_2073 DSC_2073 DSC_2083 DSC_2084 DSC_2088
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akirejea kukaa baada ya kukabidhiwa Uchifu wa Wanyamwezi
DSC_2089
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akinyanyua juu mkuki ishara ya Kijana shujaa wa Wanyamwezi..
DSC_2095
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Diwani wa Kata Utwigu
DSC_2104 DSC_2123
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa shukrani zake kwa wananchi
DSC_2174
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Kijiji
DSC_2186
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea salamu kutoka kwa watoto
DSC_2201 DSC_2212 DSC_2217
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wazee wa mila pamoja na wanakijiji
DSC_2219
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaaga wazee wa mila
DSC_2224
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha pamoja na vijana wa kijiji hicho. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).

DC MUHEZA AWATAKA WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SAMAKI KUHAMIA ENEO LA SOKO LA MICHUNGWANI

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akizungumza na wafanyabiashara wa samaki katika soko la kuuzia samaki wabichi na wakavu ambalo limevunjwa na kutakiwa kuhamia kwenye soko la michungwani ambalo limejengwa kwa ubora kwa ajili ya kufanya shughuli zao

Mfanyabiashara wa soko la samaki la  kulia akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kitu wakati alipotembelea soko la kuuzia samaki wabichi na wakavu ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kuondoka eneo hilo kuhamia eneo la michungwani.

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa soko la samaki wabichi na wakavu kuhusu kuondoka eneo hilo na kuhamia soko la michungwani ambalo limejengwa kwa ubora mzuri kwa ajili ya kufanyia biashara zao

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akimsikiliza mmoja wa wafanyabiashara ya samaki katika soko la kuuzia samaki wilayani humo ambao waliamuriwa kuhamia kwenye soko la Michungwani ambalo limejengwa kwa ubora kwa ajili ya shughuli zao.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

FAMILIA YA MFANO KUOKOA WATOTO WANAOFANYIWA UKATILI

PRETTY binti mdogo mwenye umri wa kama mwaka mmoja na nusu unapomzungumzisha, kama watoto wengine wenye afya na uhakika wa malezi anatabasamu na kucheka.

Binti huyu mdogo ambaye analelewa na familia iliyomuasili kwa malezi (hajaasiliwa kisheria) ni miongoni mwa watoto kadhaa nchini ambao wanafaidika na mpango mpya wa kusaidia watoto waliokumbwa na ukatili na unyanyasaji.

Pretty (ambaye si jina lake la ukweli-nimempa jina hilo kulinda haki yake) maisha yake mpaka sasa ni kama kitendawili kibaya ambacho ni Mungu tu alitaka kukifumbua.

Nasema ni Mungu tu kwa kuwa Pretty aliokolewa kutoka katika shimo la choo alilotumbukizwa akiwa ndani ya mfuko wa rambo uliofungwa vyema.

Sajini taji (Staff Sergeant) Pundensiana Baitu wa Dawati la jinsia wilaya ya Kipolisi Mbalizi, anasema kwamba Pretty wakati alipoopolewa katika choo cha mtu binafsi alikuwa na hali mbaya sana kiafya na juhudi kubwa sana ilifanywa na hospitali ya Meta kumrejeshea afya yake.

Akisimulia tukio hilo la kuhudhunisha alisema kwamba usiku wa Machi Mosi, mwaka jana alipokea simu iliyomtafadhalisha msaada ili kuokoa maisha ya mtoto aliyetupwa katika choo kinachotumika, katika eneo la Mlimareli huko Mbalizi.
Sajini taji Pundensiana Baitu wa Dawati la jinsia wilaya ya Kipolisi Mbalizi akizungumza na mwandishi wahabari wa Modewjiblog (hayupo pichani) hivi karibuni.(Imeandaliwa na Zainul Mzige wa Modewjiblog)

Alisema wakati anajaribu kuwasiliana na askari kwenda kuona kama wanahitaji msaada wa Kikosi cha zimamoto, akapokea simu nyingine kwamba wananchi wamebomoa choo hicho na kumtoa mtoto huyo ambaye alikuwa amefungwa katika mfuko wa rambo na kwamba alishaanza kuliwa na wadudu wa chooni.

Aidha aliambiwa katika simu kwamba mtoto huyo anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki moja alikuwa bado anapumua hali iliyomfanya aelekeze polisi kuitengeneza PF 3 haraka na kumpeleka mtoto huyo katika hospitali ya Ifisu ambao nao kutokana na kukosa vifaa vya watoto wa aina yake katika hali ile, walimkimbiza hospitali ya Meta.

Anasema yeye alifika asubuhi kuona hali ya mtoto huyo akiambatana na Ofisa Ustawi wa Jamii na hakupendezwa na hali aliyomkuta nayo mtoto.

Anasema kwamba juhudi za upelelezi kujua mama wa mtoto huyo hazikufanikiwa kwani mtoto alitupwa katika choo binafsi karibu na klabu ya pombe. Hata hivyo anasema baada ya kushindwa waliwaambia wananchi wa eneo hilo kumtazama mtu ambaye wanamtilia shaka na kumfikisha kwao kwa mahojiano.

Mpaka wakati wa kuandika makala haya mtu huyo hajapatikana.

Anasema kutokana na mfumo mpya wa familia ya mfano baada ya wao kama polisi kukamilisha kazi ya usalama na kumkabidhi mtoto huyo kwa Ofisa Ustawi wa Jamii, ofisa huyo alimtafuta mtu ambaye yuko tayari kulea mtoto na kumkakabidhi kwao.

Sajini taji huyo anasema kuwa kuna ongezeko la vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya watoto na kwamba jamii inatakiwa kubadilika na kukubali wajibu wake katika kuhakikisha usalama wa mtoto.
Afisa Ustawi wa Jamii Hospitali ya Kanda ya Nyanda za juu Kusini, Gerald Mwaulesi akielezea tukio la mtoto Pretty mbele ya kamera ya Modewjiblog jijini Mbeya hivi karibuni.

Anasema kabla ya kuanzishwa kwa wilaya mpya wakati bado iko Mbeya amekuwa akishuhudia vurugu nyingi kuhusu ukatili kwa watoto na kwamba dawati lake inachofanya ni kutoa ushauri hasa kwa wadada ambao wanatoa mimba na wengine kutupa watoto wanapopatikana.

Alisema ingawa kuna taratibu ndefu za sheria, mfumo mpya uliokubaliwa na serikali wa kupata familia ya mfano ni mfumo bora wenye kuhakikisha malezi mema na kizazi bora kijacho.

Pretty ambaye kwa sasa anaishi na familia ya mfano yenye watoto sita na yeye akiwa wa saba katika kijiji cha Muvwa kilichopo kata ya Mshewe wilayani Mbalizi ana uhakika na malezi kutokana na mfumo huo mpya.

Na Si ajabu akikua hakuna mtu hata yeye mwenyewe atakayejua kwamba aliokolewa kutoka kwenye shimo la choo alikotupwa na mama katili wiki moja baada ya kuzaliwa kwake na kusaidiwa malezi yake na mfumo wa familia ya mfano.
Dk Sipora Harison Kisanga wa UNICEF kanda ya Iringa akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa Modewjiblog (hayupo pichani)

Dk Sipora Harison Kisanga ambaye anafanyakazi na UNICEF kanda ya Iringa anasema kwamba ulinzi na usalama wa mtoto ni eda ya wananchi wote kwa ujumla, lakini kutokana na dosari zilizopo ndio maana UNICEF na Tanzania zimetia saini makubaliano yanayowezesha maandalizi ya watu wa kuwapokea watoto waliotelekezwa na wale wenye mazingira magumu ili nao waweze kuwa sehemu ya familia zilizobora.

Anasema kuufanya mfumo huo uwe na utekelezaji uliobora waliendesha mafunzo na kutambua watu wanaoweza kukaa na mtoto, na baada ya kuwakagua wapo katika orodha wakisubiri mtoto yeyote atakayepatikana.

Anasema kutokana na maandalizi hayo ndio maana hata walipompata mtoto Pretty walijua kwamba watampelaka Muvwa kwa familia ambayo iko tayari kupokea mtoto wa aina yoyote na wa umri wowote.

Anasema ni lengo la UNICEF kuhakikisha kwamba haki za watoto zinatekelezwa ikiwamo ya ulinzi na usalama dhidi ya vitu na watu wabaya, huduma za afya, huduma za elimu, haki ya kucheza na haki ya kufundishwa yaliyo mema kutoka kwa wakubwa wao.
Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri ya Mbeya, Lilian Kilongumtwa akielezea tukio la mtoto Pretty aliyetupwa kwenye shimo la choo jijini Mbeya kwa mwandishi wa habari wa mtandao wa Modewjiblog.

Anasema Ofisa huyo wa UNICEF kwamba Mradi wa familia ya mfano ulianzia Temeke na sasa upo Mbeya, Mbarali, na Mbalizi kwa lengo lile lile kuwawezesha watoto hawa kuwa na familia na kuwa salama kuliko kuwapeleka katika vituo vya kulelea yatima.

Mama anayemtunza mtoto huyo pamoja na mumewe, Mama Christer Eliston Mwashusa anasema amefurahi sana kupata mtoto huyo kwani alikuwa tayari kumsaidia kutokana na hofu ya Mungu aliyonayo.

Anasema yeye angelifurahi kama mtoto angemuasili kisheria kwani hali ya sasa ya ulezi pekee anaiona kama haimpi nafasi ya kufanyakazi yake vyema ya kumtunza. Anataka awe mali yake moja kwa moja.

Anasema amepata changamoto nyingi tangu alipomkuta mtoto Pretty hospitali ya Meta, changamoto ambazo zilimuumiza kwanza kama mzazi kwa kutambua kwamba mtoto yule hana wazazi na pia kwa kutambua kwamba ametelekezwa kikatili.
Familia Bw. Juma Mbuza (48) na Bi. Christer Mwashusha (43) inayomlea mtoto Pretty wakifurahi jambo na binti yao baada ya mahojiano na mwandishi wa habari wa Modewjiblog (hayupo pichani).

Pia changamoto ambayo alikumbana nayo ni kule kutambua kwamba mtoto yule kwa sababu ya kuwekwa chooni alikuwa na dhiki kubwa ya afya na hivyo kumfanya kuwa dhaifu.

Anasema hata wakati alipoanza kumtunza changamoto za afya yake zilikuwa kubwa na hasa alipoambiwa kwamba ana ugonjwa ambao ameurithi kwa mama yake, ugonjwa ambao ni upungufu wa kinga na kuanza kumlisha dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI kuanzia alipokuwa na miezi miwili hadi minne.

Hata hivyo katika mahojiano na Ofisa Ustawi wa Jamii kutoka hospitali ya kanda ya rufaa Mbeya (Meta) aliyempokea mtoto huyo Gerald Godfrey Mwambesi alisema kwamba Pretty hakuwa na virusi tangu awali walipompima na kusema kwamba hata vipimo vya hospitali nyingine vilivyosema kwamba ana virusi havikuwa sahihi.

Anasema Pretty alipoteza nguvu ya kinga ya mwili kutokana na kukaa chooni kwa muda na hivyo siku zilivyozidi ndivyo alivyokuwa akiongeza kinga.

Anasema baada ya siku tatu ya kukabiliana na vidonda vyake vilivyotokana na kutafunwa na wadudu chooni na baada ya wiki tatu alionekana kuwa nafuu sana na ingawa mlezi alipata changamoto kiukweli mtoto huyo hakuwa na virusi zaidi ya kupoteza kinga za kawaida ambazo zilitakiwa kurudishwa taratibu.
Dada na kaka wa kufikia mtoto Pretty wakifurahi na mdogo wao mara baada ya kutoka shule.

Anasema mtaalamu huyo kwamba waliongea na wataalamu wa watoto kuhusiana na shida hiyo ya hospitali Mbalizi kumuona mtoto na virusi wakati wao walimpima mara mbili bila kuviona na kusema kwamba hali hiyo inatokana na maambukizi yaliyosababishwa na kutupwa ndani ya choo ambayo yalihitaji tiba ya muda mrefu.

Mlezi anasema kwamba baada ya miezi miwili ya kukaa na mtoto huyo kwa uzuri aliona afya yake inadorora kiasi cha kuhitaji msaada wa tiba na kuanza kwenda hospitali kupata msaada.

Anasema hospitali aliyoenda ilisema mtoto ana maambukizi kutoka kwa mama na kushauri tiba hivyo alipelekwa katika kiliniki ya Beira ambako walimpima na kumwanzishia dozi waliyokuja kuikatisha baada ya kumpima tena kutokana na ufuatiliaji wa hospitali ya Meta na kugundua kwamba hana tatizo la maambukizi ya UKIMWI.

Mlezi wa mtoto huyo alishukuru sana watendaji wa taasisi ya Kihumbe ambao walimsaidia fedha za nauli kwenda katika hospitali kutetea afya ya Pretty na kwamba baada ya matumizi ya dawa na dawa lishe mtoto huyo mwezi uliopita (Juni 16,2016) aliambiwa kwamba mtoto wake hana maambukizi tena.

KIHUMBE, ni taasisi inayofundisha wawezeshaji namna ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa familia zao ili waweze kujimudu wenyewe na kuondokana na matatizo hayo.

Baba mlezi katika familia hiyo yenye watu saba akiwamo Pretty, Juma Mbuza amesifu juhudi za mke wake katika kuhakikisha kwamba Pretty anapata mapenzi yote ya kimama na kuendelea kustawi akiwa katika familia hiyo.

Anasema familia yake inawiwa.kulea mtoto huyo kwa kuwa ndiyo ilikuwa nia yao tangu awali na kwamba awali walitaka kuwachukua watoto waliotelekezwa katika kijiji jirani kwenye tarafa yao. Kuendelea kusoma makala hii bofya hapa

MSAJILI WA HAZINA AMALIZA MANENO KUHUSU TWIGA BANCORP


Kumekuwepo na maneno mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu benki ya Twiga Bancorp, tangu Rais John Magufuli alipoiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuchukua hatua kwa benki zote ambazo zimekuwa hazifanya vizuri ikiwepo benki ya Twiga na hivyo wananchi wengi wakawa wakiamini kuwa benki hiyo itafutwa

Akielezea kuhusu hatua zinazochukuliwa kwa benki hiyo, Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru alisema kuwa ni kweli Rais Magufuli aliagiza jambo hilo lakini alikuwa na maana nyingine tofauti na watu wengi ambavyo wamekuwa wakizunguzia jambo hilo ambalo kwa namna kubwa anaamini linachangiwa na vyombo vya habari.
Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru akitoa ufafanuzi kuhusu jambo hilo mbele ya waandishi wa habari. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Cosmas Kimario. (Picha zote na Rabi Hume, Mo Blog)

Alisema kuwa rais aliagiza BoT kuzisimamia benki ambazo zimekuwa hazitoi faida ili ziweze kusimama zenyewe na kuacha kutumia pesa ya umma ambayo imekuwa haizalishi faida yoyote na hivyo kuonekana inafanya matumizi mabaya ya fedha za serikali.

"Rais alitaka hatua zichukuliwe ili kuzifanya benki hizo ikiwepo Twiga kusimamiwa ili ziweze kuwa na tija na mwenyewe aliweka wazi kuwa hayupo tayari pesa ya umma kutumiwa bila faida,

"Baada ya hilo tumeanza kutafuta njia mbadala kuona ni jinsi gani itaweza kufanya vizuri kama ikishindikana tutatafuta hata wawekezaji lakini biashara itaendelea kuwepo kama kawaida," alisema Mafuru.

Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa kupata maelezo kutoka kwa Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru kuhusu benki ya Twiga Bancorp.

Aidha alieleza kuwa kumekuwepo na taarifa kuwa wateja wa benki hiyo wapo katika hatari ya kupoteza pesa zao kutokana na benki hiyo kuwa katika hasara na hivyo kuwatoa hofu kuwa benki ipo na pesa zipo salama na wasiwe na wasiwasi kuhusu hilo.

Pia Mafuru aliongeza kuwa pamoja na kuwa katika mpango wa kutafuta mbinu mpya ya kutumia ili kuifanya benki hiyo kuwa na tija lakini pia taarifa ambayo imetolewa wiki iliyopita inaonyesha kuwa kwa mara ya kwanza benki hiyo imeingiza faida na hivyo kuwa na matumaini mapya kuwa kuna uwezekano wa benki hiyo kuanza kufanya vizuri katika biashara.

Na Rabi Hume, Mo Blog