Pages

KAPIPI TV

Friday, July 22, 2016

KUELEKEA MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM MJINI DODOMA, WAJUMBE KUTOKA MKOANI MWANZA WAELEZEA IMANI YAO

Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, akizungumzia maandalizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza, ambao tayari wameanza kuwasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 23,2016 ambapo pamoja na mambo mengine pia Mkutano huo ni maalumu kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Katika Mkutano huo, Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM wanatarajiwa kumpitisha kwa kura za ndiyo Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, akipokea Uongozi kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mkoani Mwanza, wamesema wana imani kubwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ambaye anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

Katibu Mwenezi wa CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, ameyasema hayo hii leo, wakati akizungumzia maandalizi ya wajumbe hao ambao baadhi yao tayari wamewasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Julai 23 mwaka huu.

“Sisi wajumbe tunaotoka Mkoa wa Mwanza tunaamini kwamba anatosha (JPM) na yuko makini na chama chetu kitaendelea kuimarika zaidi akikabidhiwa uongozi. Amesema Mangelepa na kuwasihi viongozi wengine wa CCM kuanzia ngazi ya Mashina, Matawi, Kata, Wilaya na Mkoa, kuendelea kukiimarisha chama, ikiwemo kusimamia vizuri Ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanyonge kama Rais Magufuli anavyosisitiza.

Ametanabaisha kwamba wananchi wakiwemo wanaccm, wanayo matumaini makubwa kwa Rais Magufuli katika utendaji wake wa kazi, na kwamba wapenda amani na maendeleo wanaochukia rushwa pamoja na ubadhirifu wanampenda sana.

Katika hatua nyingine Mangelepa amepuuzilia mbali madai yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaobeza utendaji kazi wa Rais Magufuli na kwamba hiyo inaashiria hofu waliyo nayo baada ya kukabidhiwa uongozi wa CCM kwa kuwa watakosa hoja za kuzungumza kisiasa.
Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.

MAN UTD DORTMUND KUFUNGUA PAZIA LA MICHUANO YA ICC ITAKAYOONEKANA KUPITIA STARTIMES




 Na Dotto Mwaibale

 IKIWA chini ya kocha wake mpya Mreno, Jose Mourinho, Manchester United wanatarajia kushuka dimbani jijini Shanghai, China kuwakabili Borrusia Dortmund siku ya Ijumaa Julai 22, 2016 mechi itakayopigwa saa tisa za alasiri kwa saa za hapa nyumbani kupitia ving’amuzi vya StarTimes.

Akizungumzia juu ya habari hiyo njema kwa wapenda soka nchini Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif amebainisha kuwa michuano hiyo itakuwa ni ya kusisimua kutokana na orodha ndefu ya timu kubwa zitakazoshiriki kama vile Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain, Juventus, Liverpool, Chelsea na Bayern Munich kwa uchache.

“Tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa watapata fursa ya kutazama timu zao katika mechi za awali kabla ya kuanza kwa ligi kuu mbalimbali duniani kupitia ving’amuzi vya StarTimes pekee. Mechi zote za michuano ya ICC itaonekana moja kwa moja kupitia chaneli ya World Football inayopatikana katika kifurushi cha Mambo kwa malipo ya shilingi 12000/- tu kwa mwezi. Michezo yote itakuwa ni yenye msisimko mkubwa kwani timu zinazoshiriki ni kubwa, nyingi zikiwa ni mabingwa katika ligi kuu zao, zina wachezaji nyota na kikubwa zaidi zingine hazikuwahi kukutana kabla.” Alisema Bi. Hanif

“Hii ni fursa ya pekee kwa watanzania kwani tunafahamu ya kuwa ni wapenzi wakubwa wa mchezo huu na siku zote StarTimes tunajitahidi kuwapatia kile wanachokipenda. Hii ni mara ya pili tunaonyesha moja kwa moja michuano hii kwani mwaka jana tulifanya hivyo ambapo timu ya Real Madrid waliibuka mabingwa. Hivyo basi mashabiki watakuwa na shauku kubwa ya kujua ni timu gani itakayoibuka mabingwa au kama utarudi kwa Real Madrid,” alisema na kumalizia Bi. Hanif kuwa, “Ni wajibu wetu kuhakikisha wanafikiwa na matangazo ya vipindi vizuri na kusisimua kama hivi kwa ubora wa hali ya juu na gharama nafuu ambazo kila mtu atazimudu.”

Mchezo huo ni sehemu ya ufunguzi wa michuano ya kombe la mabingwa wa kimataifa almaarufu kama International Champions Cup au ICC itakayoanza kutimua vumbi Julai 22 na kumalizika Agosti 13, 2016 katika viwanja mbalimbali nchini Marekani, Ulaya, Australia na China.

Katika michuano hii wapenzi wa soka duniani watapat fursa kujionea kwa mara kwanza mechi ya watani wa jadi kutoka jiji la Manchester au unavyojulikana kama ‘Machester Derby’ miongoni mwa mashabiki wengi. Mechi hiyo itapigwa siku ya Jumatatu ya Julai 25 jijini Beijing, China.

Mchezo huo utanogeshwa si tu na ushindani baina ya wachezaji au mashabiki bali safari hii ni makocha waliopewa vibarua vya kunoa vikosi hivyo, Jose Mourinho wa Manchester United na Pep Guardiola wa Manchester City.

Ukiachana na mechi hiyo, pia macho ya mashabiki wengi yatakuwa yakisubiria kwa hamu kutazama mechi kali zitakazozikutanisha timu za, Real Madrid na  PSG,  Chelsea na Liverpool, Real Madrid na Chelsea, Bayern Munich na Real Madrid pamoja na Liverpool na Barcelona.

Kwa ujumla timu zitazoshiriki  michuano hii ni pamoja na Real Madrid, Barcelona, Manchester United, Manchester City, Paris Saint-Germain (PSG), Juventus, Liverpool, Chelsea, Bayern Munich, Liverpool, Tottenham Hotspurs, AC Millan, Inter Millan, Leicester City FC, Celtic FC, Atletico Madrid, Melbourne Victoria na South China.

Thursday, July 21, 2016

“NAVY KENZO KUMSINDIKIZA MISS TANGA 2016”


                      

                NA, MWANDISHI WETU TANGA
MSANII wa Mziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Navy Kenzo anatarajiwa kutumbuiza kwenye shindano la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga Miss Tanga 2016 litakalofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.

Licha ya Navy Kenzo wasanii wengine ambao watasindikiza onyesho hilo kwa kutoa burudani ni kundi la mziki wa kizazi kipya mkoani Tanga,Wazenji Classic pamoja na Dances.


Akizungumza jana,Mratibu wa Onyesho hilo, alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri ambapo tayari warembo watakaoshiriki wameanza kuingia kambini .


Shindano hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha Radio cha TK FM 88.5 kilichopo mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wameelezea namna walivyo jipanga kuhakikisha onyesho hilo linakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya warembo waliopo .

   
“Nisema tu tumejiandaa vizuri kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa umakini mkubwa ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya urembo mkoani hapa kuweza kupata ladha halisi ya onyesho hilo kwani licha ya kuwaona warembo wakali wakini pia mzee wa kamatia chini atakuwepo kuwapagawisha “Alisema.


Hata hivyo alisema kuwa mazoezi ya warembo watanaoshiriki onyesho hilo yanaendelea kwenye ukumbi wa New Hotel uliopo mjini hapa kuanzia saa kumi jioni.

Aidha alisema kuwa kabla ya kufanyika shindano hilo warembo hao watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani hapa ikiwemo Mapango ya Amboni na Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

CHAMA CHA NCCR- MAGEUZI CHABAINI NCHI KUONGOZWA KWA MATAMKO YA RAIS BADALA YA KATIBA



Mkuu wa Idara ya Kampeni na Uchaguzi wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia (katikati), kuzungumza kuhusu maazimio yaliyofikiwa  na Kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa cha kawaida kilichoketi Julai 16 mwaka huu. Kushoto ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe.
 Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu maazimio mbalimbali yaliyopendekezwa katika kikao cha Halmshauri Kuu ya Taifa ya chama hicho cha kawaida  kilichoketi Julai 16 mwaka huu. Kushoto Katibu Mkuu wa chama hicho, Mosena Nyambabe.


 wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha NCCR Mageuzi kupitia Halmshauri yake Kuu ya Taifa kimesema kinasikitishwa na hali ya nchi hivi sasa ambayo inaongozwa kwa matamko ya Rais badala ya kufuata katiba jambo ambalo ni hatari kwa taifa.


Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi Taifa, James Mbatia wakati akizungumza na wanahabari makao makuu ya chama hicho, Ilala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mapendekezo yaliyofikiwa na kikao hicho.

"Hivi sasa nchi inaongozwa kwa matamko mbalimbali ya Rai badala ya kufuata katiba ya nchi" alisema Mbatia.

Mbatia alisema Rais Dk.John Magufuli amekuwa akiongoza nchi kwa kutoa matamko badala ya kuongozwa kwa kufuata katiba, sheria na kanuni za nchi.

"Mfano siku akiongea na majaji aliwaamuru watoe hukumu haraka dhidi ya waliokuwa na makontena ambayo yalikuwa hayajalipiwa kodi na kuahidi kama wakilipa atawapa sehemu ya fedha hizo wakati bunge ndiyo lenye mamlaka yakuidhinisha matumizi ya pesa za serikali,"alisema Mbatia.

Alisema kutokana na tamko hilo kwa majaji ilikuwa ni kuingilia mamlaka ya Mahakama na Bunge kitu ambacho ni kinyume cha kanuni, taratibu na katiba ya nchi.

Alisema hali hiyo imesababisha demokrasia kukiukwa huku uhuru wa kujieleza (Freedom of Exptression) ukiendelea kudidimia siku hadi siku. 

Alisema kumekuwa na matumizi ya nguvu za dola kupitia jeshi la polisi kwa kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa kwa kuwakamata na kuwaweka rumande viongozi wa kisiasa na kuwashtaki kwa  makosa mbali mbali.

"Viongozi wakisiasa wamekuwa wakikamatwa na Jeshi la Polisi kwa makosa mbali mbali lakini kinachofanyika ni ukiukwaji wa uhuru na hazi za vyama vya siasa katika kufanya kazi zao ambazo zipo kikatiba pamoja na sheria za vyama vya siasa,"alisema.

Kwa upande mwingine chama hicho kupitia maazimio ya kikao cha Halmashauri Kuu ya chama kimetangaza kumsimamisha uongozi wa Umakamu Mwenyekiti (Bara) na kumvua uanachama Leticia Ghate Mosore kwa makosa mbali mbali aliyoyafanya ndani ya chama.

Mbatia alisema wameamua kumsimamisha uongozi na kumvua uanachama kwa kukiuka kanuni na katiba ya chama hicho ikiwa ni pamoja na usaliti alioufanya kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

"Kwa jumla makosa aliyoyafanya ni pamoja kujihusisha na migogoro ndani ya chama, kutoa tuhuma dhidi ya kiongozi wa cham au mwanachama nje ya utaratibu, kukashifu kiongozi wa chama au mwanachama, kuhujumu chama katika uchaguzi na wakati mwingine wowote na kutoa na kupokea rushwa," alisema Mbatia.

Alisema milango iko wazi kwa Leticia kukata rufaa kama atakuwa hajaridhika na maamuzi hayo na rufaa yake itasikilizwa na kama ataonekana hana hatia juu ya makosa hayo atarudisha kundini.

Aidha kuhusu chama chake kushiriki katika muungano wa Umojka wa kaiba ya wananchi (Ukawa), alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na vyama hivyo kwa nguvu zote.

Alisema kupitia umoja huo chama chake kipo pamoja na wanachi katika kupambana na kupigania kuhakikisha katiba mpya inapatikana kama matakwa yao wananchi wenyewe.

Alisema ikiwa Jaji Lubuva ataleta katiba ile iliyopitishwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) watapiga kampeni za kuipinga kwa nguvu zote mpaka itakapopatikana katiba inayokidhi mahitaji ya wananchi.




SBL YAZINDUA BOMBA LA MIL.470/= KUDHIBITI MAJITAKA.



Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie  wakiongozana kuelekea kwenye  bomba la kudhibiti wa majitaka  ambalo linalenga  kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira  na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.





Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha akifafanua jambo kwa wageni waalikwa katika hafla   ya uzinduzi wa bomba la majitaka  ambalo lilizinduliwa na  Mhe. Luhaga Mpina Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira mapema leo katika kiwandani hapo mapema leo.









Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini jinsi mtambo wa kusafirisha majitaka unavyofanya kazi kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.





Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akifurahi jambo  na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie mara baada ya kukata utepe katika mtambo kusafirisha majitaka katika hafla iliyofanyika mapema leo kiwandani hapo,


Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiwasha mtambo wa kusafirisha majitaka  kiwandani hapo mara baada ya kuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika kiwanda hicho Temeke Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda cha bia cha serengeti wakifuatilia kwa makini

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha bia ya serengeti mara baada ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda hicho Jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam, Kampuni ya Bia ya Serengeti leo imezindua  bomba la kudhibiti wa majitaka  ambalo linalenga  kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira  na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.


Bomba hilo  limejengwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya Maji Safi na Taka  ya Dar es Salaam (Dawasco), Mamlaka ya Barabara (Tanroads) na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke  likihusisha takribani  kilometa mbili kuanzia katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichpo Temeke  hadi Kurasini ambako ndip ulipo mfumo wa majitaka wa Dawasco.


Akizungumza wakati wa uzinduzi, huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie, alisema kwamba  mradi huo wa aina yake na wa kwanza nchini unadhihirisha juhudi zisizo na ukomo za kampuni hiyo katika kuhifadhi mazingira.


“Ubora wa maji ni jambo lililo mstari wa mbele katika utengenezaji wa bia  lakini suala la usafi kutokana na kuzalishwa kwa majitaka ni sehemu kubwa inayotujengea hisia za kimazingira katika shughuli za kutengeneza bia. Kwa hiyo uzinduzi wa bomba hili ni moja ya hatua ya kusonga mbele  katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira safi kiafya,” alisema Weesie.


Mkurugenzi Mtendaji huyo alibainisha kwamba majitaka yanayotolewa na bomba hilo yatakuwa yanafanyiwa tiba kwanza ili kuondoa aina yoyote ya sumu kabla ya kuachiwa ili kuingia katika mfumo wa majitaka wa Dawasco.


 Alisema kuwa uzinduzi huyo uko katika mkondo  mmoja na sera ya Kampuni ya Serengeti ya kujikita katika ustawi wa jamii ambayo imeainishwa katika maeneo manne ya vipaumbele ambavyo vinajumuisha, Utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuboresha Unywaji wa Kistaarabu.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Masuala ya Muungano na Mazingira, Mh. Luhanga Mpina aliipongeza Serengeti kwa kuzindua bomba hilo  akibainisha kwamba  ujenzi  unaendana na ajenda ya serikali  ya uhifadhi wa mazingira.

Mpina alibainisha kwamba uchafuzi wa mazingira katika miji na maeneo ya pembezoni unaathiri afya za watu wengi na kupunguza tija inayotokana na mazingira na kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga  kazi nzuri ya Kampuni ya Bia ya Serengeti katika kuhifadhi mazingira.

WANAHABARI WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE.

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika Boti wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe,hifadhi maarufu kwa kuwa na mnyama aina ya Sokwe mtu.
Watalii wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe .
Eneo mojawapo linalotumiwa na wavuvi katika mwambao mwa ziwa Tanganyika jirani na Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Baadhi ya wanahabari muda mfupi baada ya kufika hifadhi ya taifa ya Gombe.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) ,Pascal Shelutete akiwatamburisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini  walipotembelea hifadhi ya taifa ya Gombe.
Kaimu Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe,Goodluck Tarimo akizungumza na wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo.
Baadhi ya Wahifadhi waongoza wataalii katika Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Daktari wa Mifugo katika Hifdhi ya Taifa ya Gombe,Dkt Jane Raphael akizngumza mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuaza safari ya kutembelea hifadhi hiyo.
Mhifadhi Hussein 
Mhifadhi Isaya Mkude akitoa maelezo kwa wanahabari wakati wa kuanza safari ya kwenda kuwatizama Sokwe.
Safari ya kwenda kuwatizama Sokwe ikaanza.
Maeneo mengine Mhifadhi Isaya Mkude aalikua akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali na majibu ya maswali yaliyoulizwa na wanahabari.
Nyani ni miongoni mwa wanyama wanaoonekana kwa urahisi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Safari ya kuwatafuta Sokwe ili kua ni ya vipando pia.
Wakati mwingine wanahabari walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata pumzi mpya ya kuendelea na safari 
 Baadhi ya Sokwe mtu walioonekana kwa mbaali sana wakiwa katika miti.
Hatimaye safari ya kurudi katika makazi ikaanza kwa kupita katika fukwe ya ziwa Tanganyika inayopakana na hifadhi ya taifa ya Gombe. 

Na Dixon Busagaga wa Michzui Blog.

DK.KIGWANGALLA ASIMIKIWA MTEMI WA WANYAMWEZI

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amepewa heshima ya Uchifu wa Watanzania wa Kabila la Wanyamwezi na Wazee wa Kijiji cha Isalalo katika Kata ya Utwigu iliyopo katika Jimbo hilo la Nzega Vijijini Mkoani Tabora.
Dk. Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo kwa lengo la kushukuru Wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi za zilizomwezesha kuingia Bungeni, ambapo katika tukio hilo lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wanakijiji wa Kijiji hicho,
Wazee hao wa Mila walieleza kuwa, hatua hiyo ya kusimikwa Uchifu wa heshima wa kabila la Wanyamwezi ni ishara kubwa kuwa Kijana mashuhuri na kijana mpiganaji sawasawa hivyo kwa ushindi wake kuchaguliwa nahata kupewa Uwaziri (Naibu Waziri), ni ishara kubwa ya kufikia malengo yake aliyokusudia katika Taifa hili.
Wazee hao wa Mila waliweza kumkabidhi mishale, Mkuki, upinde na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kiutawala.
Akitoa shukrani zake katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Wananchi wake wategemee neema kubwa kwani kwa sasa yupo katika hatua ya utendaji kazi Zaidi na kuwataka wawe na Imani naye pamoja Serikali iliyopo madarakani kwani imejipanga kuleta maendeleo makubwa.
“Nawashukuru nyie kwa kuniwezesha kunipigia kura nyingi sana ambazo zimeniwezesha mimi kupata nafasi ya kuingia Buangeni. Nawaahidi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote. Nguvu nilizozianza tokea awali na kwa sasa zitakuwa kubwa Zaidi, muendelee kuniombea.
Nafahamu kuna kero nyingi sana, shida za barabara za kuingia na kutoka huku Vijijini, Suala la Umeme na mengine mengi haya yote yanafanyiwa kazi na taratibu zote zinaenda vizuri.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho cha Isalalo.
Ziara hiyo iliyoanza tokea Julai 13 mwaka huu, Mbunge huyo ambaye Jimbo lake hilo lenye jumla ya Kata 19, zikiwemo Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe.
Ambapo katika Vijiji vya Kata hizo amewafikia wananchi na kuwashukuru kwa hatua yao ya kumchagua ambapo pia ameweza kutekeleza ahadi aliyoitoa yeye mwenyewe ikiwemo vifaa vya michezo kwa timu za vijana, pamoja na kutimiza ahadi za michango mbalimbali ikiwemo ya kuchangia ujenzi wa shule, makanisa, misikiti, Zahanati na mambo mbalimbali huku pia akipokea maoni na uashahuri kutoka kwa wapiga kura wake hao.
DSC_2015 DSC_2023 DSC_2030Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Wanakijiji cha Isalalo
DSC_2032
Wazee wa Mila
DSC_2037
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni
DSC_2038
Wazee wa Mila wakiwa upande wa wageni maalum
DSC_2043
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akivishwa shuka katika hatua ya kusimikwa uchifu huo
DSC_2044 DSC_2047
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhiwa mkoba wa mishale
DSC_2050 DSC_2051 DSC_2054 DSC_2059
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipewa baraka na wazee hao
DSC_2083 DSC_2062 DSC_2066 DSC_2073 DSC_2073 DSC_2083 DSC_2084 DSC_2088
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akirejea kukaa baada ya kukabidhiwa Uchifu wa Wanyamwezi
DSC_2089
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akinyanyua juu mkuki ishara ya Kijana shujaa wa Wanyamwezi..
DSC_2095
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Diwani wa Kata Utwigu
DSC_2104 DSC_2123
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa shukrani zake kwa wananchi
DSC_2174
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Kijiji
DSC_2186
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea salamu kutoka kwa watoto
DSC_2201 DSC_2212 DSC_2217
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wazee wa mila pamoja na wanakijiji
DSC_2219
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaaga wazee wa mila
DSC_2224
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha pamoja na vijana wa kijiji hicho. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).