Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 7, 2016

USAILI MAISHA PLUS MTWARA,FUNGA KAZI.

Ni asubuhi tulivu katika fukwe za bahari ya hindi kusini mwa Tanzania ambapo vijana wengi wamejitokeza kufanya usaili wa mashindano ya Maisha Plus East Africa 2016. Wapo wanaoonekana kujiamini na wengine wamejawa uoga. "Ni siku niliyoisubiri kwa hamu sana" anasema Faustine Komba miongoni mwa washiriki kutoka Mtwara.
678A0009
Safari ya msimu wa tano wa mashindano ya Maisha Plus imeanza rasmi kwa kuanza na usaili uliofanyika katika hotel ya NAF Beach iliyoko Mtwara. Washiriki kutoka mikoa ya jirani nao pia walijitokeza. "Maisha Plus kwangu ni ndoto ya muda mrefu sana, niliposikia mnakuja Mtwara nikasema piga ua lazima nishiriki" Anasema Ismail Likando aliyesafiri kutoka Lindi.
678A0022
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A9916
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A9925
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Maswali mengi yalilenga kupima uelewa wa vijana kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo mtazamo wao juu ya mwenendo wa kiuchumi. Mengine yalilenga kuwachanganya tu.
678A9961
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A9971
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Mshiriki Grace Pemba anaelezea changamoto mbalimbali alizokutana nazo kutokana na kuolewa akiwa na umri mdogo, anasema hadi sasa ana watoto wawili ambao wanaishi na baba yao. Alipoulizwa maswali zaidi Grace alijawa na simanzi na kujikuta akitoa machozi, "Nimelia kwa sababu mmenikumbusha nyuma nilikotokea" anasema Grace mfanyakazi wa Saloon kutoka mkoani Mtwara.
A video posted by Maisha Plus (@maishaplus2016) on Jun 4, 2016 at 6:47am PDT
678A9980
Mshiriki Grace Pemba akijifuta machozi.
Wakati usaili ukiendelea hali ya kujaa kwa maji baharini ilitokea na kulazimisha timu ya Maisha Plus kubadili utaratibu wa awali wa upigaji picha.
678A0075
Waandaaji wa mashindano ya Maisha Plus wakibadili utaratibu wa awali wa kupiga picha baada ya maji kujaa.
678A0046
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0056
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0281
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0279
Muhitimu wa shahada ya kilimo William Mbaga alibanwa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo faida za kilimo cha 'greenhouse' pamoja na namna ambavyo maziwa ya mtindi yanapatikana. William alijieleza kwa ujasiri.
678A0157
William Mbaga akiondoka baada ya kufanya usaili.
Washiriki wenye fani na ujuzi mbalimbali walijitokeza wakiwemo madereva bodaboda, mafundi, waigizaji, waimbaji, wasusi n.k
678A0223
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0083
Waigizaji pia walikuwemo katika usaili wa #MaishaPlusMtwara
678A0167
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0113
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0308
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0328
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

678A0336
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Mashindano ya Maisha Plus kwa mwaka huu yanatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda ambapo mshindi atajishindia ufadhili wa wazo la biashara lenye thamani ya Tzshs. Milioni 30.
"Mwaka huu washiriki wajipange sana. Maandalizi yaliyofanywa kufanikisha msimu huu hayajawahi kutokea katika historia ya Maisha Plus. Ni kama tunaanza moja" Alisema Masoud Kipanya, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa mashindano haya.
678A0145
"Tumewekeza katika teknolojia ya kisasa ili kupata picha za matukio yenye uhalisia zaidi. Watazamaji wategemee burudani safi isiyomithirika kupitia Azam Two." Alisema David Sevuri, miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus.
Taarifa mbalimbali kuhusu mashindano haya zinapatikana kupitia tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv

Saturday, June 4, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




NAIBU WAZIRI WA HABARI MGENI RASMI AZANIA BANK KIDS RUN 2016 YATAKAYOFANYIKA KESHO KUTWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR E SALAAM

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akimkaribisha Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu mbio hizo zitakazofanyika kesho kutwa. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday.
 Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), akizungumzia kuhusu mbio hizo.
 Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday (kulia), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo.
 Mwanafunzi Rachel Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Mwenzake Ali Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wa mbio hizo.
 Wanahabbari wakichukua taarifa hiyo.
Waratibu wa mbio hizo wakionesha fulana zitakazotumiwa na watoto watakao kimbia mbio hizo. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Peter Mwita, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.

Dotto Mwaibale

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  Mbio za Watoto za Azania Kids Run 2016, 
 zitakazofanyika Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016, zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi katika kinyang'anyiro hicho kitakachokuwa na mbio za kategori tano.

Gidabuday amebainisha kuwa, maandailizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.

"Mbio hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, zikihusisha watoto chini ya miaka 16, ambako Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi," alisema Gidabuday.

Amewasisitiza wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Gidabuday ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa kukimbia.

"Barabara zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa watakaohitaji kupatiwa huduma hizo," amesema Gidabuday katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam.

Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la kihistoria.

"Mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh. 150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000," amesema.

Katika mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000 na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.

Aidha, amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh. 75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh. 40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama kilivyotajwa hapo juu.

Pia kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini ya miaka mitatu, ambako washindi washindi wote watafunguliwa akaunti katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MWANDISHI WA " THE ECONOMIST" GAZETI LA KIINGEREZA.

 Kaimu  Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mchana huu wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mwandishi wa " The Ecomist" Gazeti la Kiingereza linatoka kwa wiki dhidi ya Serikali ya Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda. 
 Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda (kulia), akitoa ufafanuzi wa Uchumi tangu Rais Dk. John Magufuli aingie madaraka na miradi iliyosajiliwa na kituo hicho.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Taarifa akichukuliwa na wanahabari.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotpka kila wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.

Habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa "Government by gesture, A President who looks good but governs impulsively"

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi wa habari hiyo Kaimu  Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa.

"Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma" alisema Zamarad.

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na imelenga kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli aingie madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya watanzania na wageni.

Biganda alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa imesajiliwa na TIC.



"JIPU IDARA YA MALIASILI WILAYA YA SIKONGE"

Thursday, June 2, 2016

FASTJET YATANGAZA SHINDANO LINGINE KWA WATEJA WAKE


Dar es Salaam 30 Mei 2016 –  fastjet, shirika la ndege la bei nafuu Afrika  limezifanya ndoto za usafiri  kuwa za kweli  kwa abiria wake zaidi ya milioni mbili  waliopaa anga za Afrika tangu kuzinduliwa kwake Novemba 2012.


 Ukiwa kama mkakati wa kuhamasisha hata Watanzania wengi zaidi  kusafiri, fastjet  imetangaza kwamba abiria yeyote anayenunua tiketi  kuanzia Jumanne Mei 31 ataingia kwenye  bahati na nasibu  ya kwanza ya aina yake  ijumulikanayo Big 10 draw ambapo washindi 10 watasafiri bure   katika njia yoyote  ya fastjet katika mtandao wake barani Afrika.


Kwa watu kumi watakaoshinda bahati nasibu hiyo  shirika linawapa uwezo wa kwenda katika mapumziko  au kwenda katika safari ya manunuzi  pamoja na marafiki  na familia  jambo wamekuwa wakiliwazia  kila mara.


Ama kwa wajasiriamali wa Tanzania, safari hiyo inaweza kutumia kukuza mahitaji ya biashara kwa kuokoa  gharama za usafiri katika safari nyingine kumi wanazozihitaji  kusafiri.


 “Ni rahisi, lengo la fastjet ni kufanya uwezekano kwa wateja wengi kusafiri, iwe ni kwa shughuli za biashara, kutembelea marafiki  na familia, au kufurahia burudani ya kusafiri,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania John Corse.


 Njia ambazo zinahusiana  kwa ajili hiyo ni safari za kutoka Dare es Salaam kwenda Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Nairobi, Entebbe, Lusaka, Harare na Johannesburg hali kadhalika safari  kati ya Kilimanjaro na Harare.


 Tiketi zitakazonunuliwa Jumanne Mei 31, 20016 kwa njia za kimataifa na  za ndani  zitawawezesha abiria wake kuingia katika bahati nasibu ya Big 10. Washindi watatangazwa Juni 2016 na safari 10 za bure  ni lazima zifanyike  kabla ya Desemba 11, 2016.


 Ikitambuliwa kama shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, fastjet hivi sasa inafanya safari  ndani ya nchi 11 kwa wafanyabiashara, watali na familia ambazo zimeipokea tozo lake la nauli nafuu na linalofikia kwa usafiri wa anga.


 “Usafiri wa anga ni ufunguo unaoendelea kuhamasisha na kukuza uchumi wa Tanzania  kwa kuufanya uwe rahisi kwa familia, wafanya biashara  na watalii kumudu kusafiri,” alisema Corse  na kuongeza, “tumezindua punguzo hili la nauli  hivyo kwamba hata wasafiri wanaweza kuzoea usafiri wa anga wanaoumudu, iwe wanasafiri kwa ajili ya biashara au mapumziko.”


Kukata tiketi kiunaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia www.fastjet.com, kupitia wakala aliyethibitishwa au kwa kuwasiliana na na fastjet kupitia +255 784 108 900. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa fedha taslimu, kwa njia ya mtandao kwa kutumia kadi au  malipo kwa njia ya mitandao ya simu.

Tuesday, May 31, 2016

VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUJIUNGA NA MASHIRIKA YA KUJITOLEA ILI WAJIONGEZEE UJUZI NA MAARIFA.

Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.
Martin alisema, "Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu" 

"Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira" aliongezea Martin.

Aidha, Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya na Amerika.

Mmari aliongezea, "Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali, usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa kwenye programu"
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.
Kwa upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo  wameshukuru kwa nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.

Mmoja wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha,  alisema kuwa anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia kutatua matatizo hayo.
"Nimekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania" aliongezea Bi. Malamsha.

Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao
Naye kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha biashara.
"Nimeweza kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe" alimalizia Said.

Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo  la kuisaidia jamii ya Tanzania sehemu mbalimbali.

MISS TANZANIA USA PAGEANT AEESHA KAMARA TEMBELEA, KUONGEA NA KUTOA MSAADA KENTON HIGH SCHOOL

Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja

JK AWAFUNDA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali ya 2016 ya Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
 Vijana vyuo vikuu Dar es Salaam wakiserebuka katika mahafali yao.
 Vijana hao wakiendelea kuserebuka.
 Hapa ni furaha kwa kwenda mbele.
Ni kama wanasema'  Hapa ni ushindi tu 2020 kwani vijana tumejipanga.
Vijana wakiwa kwenye mahafali hayo.

Friday, May 27, 2016

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA

Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.


Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.