Pages

KAPIPI TV

Tuesday, June 7, 2016

MAHOJIANO NA CHIEF ISSA KAPANDE TOKA SWEDEN

Chef Issa ma ma-Chef  wa timu ya Stockholm, Sweden, waliposhiriki na kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha timu za kanda kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Mapishi  2014 yajulikanayo kama  Villeroy & Boch Culinary World Cup 2014  yaliyofanyika nchini Luxemborg.
Chef Issa Kapande ni mpishi maarufu na mmiliki wa mgahawa mkubwa unaotoa huduma za chakula cha Kitanzania nchini Sweden, unaojulikana kama Tanzania Restaurant
Alikuwa mkarimu sana kujiunga na Mubelwa Bandio kuzungumzia safari yake katika fani ya upishi na mpaka alipofikia.
Karibu ujiunge nasi kusikiliza



JUKWAA LANGU JUNE 6 2016:HAKI,WAJIBU NA NAFASI YA DIASPORA KWA TANZANIA.

Photo Credits: WikiProject African Diaspora
Katika kipindi cha JUKWAA LANGU wiki hii, tumejadili kuhusu DIASPORA.
Ni ipi nafasi, wajibu na haki yetu katika nchi yetu (Tanzania)?
Ni kweli kuwa tuna watu ama mahala muafaka kutuwakilisha nchini kwetu?
Na je! Tuna vyanzo halisi vya habari na taarifa kutoka Tanzania?
Tu,eumgama ma waTanzania wa Uingereza na Marekani kujadili hili

WATANZANIA WAANZA KUFURAHIA MICHUANO YA COPA AMERICA KUPITIA STARTIMES

 Meneja Mauzo wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Michuano ya Copa America katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Copa America imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo inachezeka nchini Marekani na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya Kusini na Kaskazini na kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl Football.



 Wateja wakinunua ving’amuzi vya StarTimes kwa bei ya shilingi 22,000/- vilivyounganishwa na ofa ya kifurushi cha Mambo chenye chaneli za Sports Focus na World Football ili kujionea michuano ya Copa America moja kwa moja. Copa America imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo inachezeka nchini Marekani na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya Kusini na Kaskazini na kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl Football. 

 Hapa wakipiga mpira.
 Wateja wa StarTimes wakiwa na zawadi zao walizojishindia baada ya kununua ving’amuzi ili kujionea michuano ya kombe la Copa America. Copa America imeanza Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu ambapo inachezeka nchini Marekani na kushirikisha mataifa 16 ya Marekani ya Kusini na Kaskazini na kuonekana kupitia chaneli za Sports Focus na Worl Football.
Na Dotto Mwaibale

MASHABIKI  wa soka nchini kote wameanza kufurahia mechi za michuano ya kombe la Copa America ambayo inaonekana moja kwa moja kupitia ving’amuzi vya StarTimes kwenye chaneli zake za michezo za Sports Focus na World Football kuanzia Juni 4 mpaka Juni 26 mwaka huu inayopigwa nchini Marekani.

Akizungumza katika uzinduzi wa kuanza rasmi kwa michuanoo hiyo katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii Meneja wa Mauzo wa StarTimes Tanzania, Bw. David Kisaka amebainisha kuwa Copa America imekwishaanza na tayari timu za Marekani na Colombi zimekwisha fungua pazia.

“Leo ninayo furaha kubwa kuwafahamisha wateja wetu na watanzania wapenda soka kwamba michuano ya Copa America inaonekana moja kwa moja kwenye ving’amuzi vyao vya StarTimes. Mechi zote za kombe hili 32 zitakazozikutanisha timu kutoka mataifa 16 kwenye viwanja 10 tofauti nchini Marekani zitaonekana kupitia chaneli zetu za michezo za Sports Focus na World Football. Anachotakiwa mteja ni kujiunga na malipo ya mwisho wa mwezi ya kuanzia shilingi 12,000/- na kuendelea na wasio na ving’amuzi vyetu watembelee viwanjani hapa au maduka, mawakala na ofisi zetu ili kununua kwa bei nafuu kabisa ya shilingi 22,000/- tu ikiwa na ofa ya kifurushi cha Mambo kwa mwezi mmoja.” Alisema Bw. Kisaka

Meneja huyo wa Mauzo alifafanua zaidi kuwa kutokana na tofauti ya muda baina yetu na nchi ya Marekani ambako michuano hiyo inafanyikia kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwake miaka 100 iliyopita mechi hizo zitakuwa zikirudiwa kupitia chaneli hizo hizo kuanzia saa saba mchana.

“Kuna tofauti kubwa kati ya muda na hivyo kusababisha mechi nyingi kuanza usiku au alfajiri, mechi za mapema kabisa kwa muda wa kwetu zinaanza saa sita ya usiku. Kwa kulitambua hilo mechi hizo zitakuwa zikirudiwa mchana ili kila mtu aweze kushuhudia ni kitu gani kinaendelea. Na mpaka sasa tayari wenyeji Marekani wamekwisha fungua pazia kwa mechi yao ya kwanza ambayo wamepoteza kwa kufungwa magoli 2 – 0 dhidi ya Colombia. Msisimko ni mkubwa wa michuano hii kwani wachezaji nyota wote wa dunia kutoka bara la Amerika ya Kusini watakuwa uwanjani kuhakikisha kombe linarudi nyumbani. Wachezaji kama Lionel Messi, Luis Suarez, Kun Aguero, Gonzalo Higuan, Angel Di Maria, Edinson Cavani, James Rodriguez, Countinho na wengineo wengi.”

Bw. Kisaka alimalizia kwa kusema kuwa, “Ninapenda kuchukua fursa hii kuwasihi watanzania kulipia ving’amuzi vyao na kujiunga nasi. Falsafa ya StarTimes Tanzania ni kutaka kila mtanzania afurahie matangazo ya dijitali akiwa nyumbani kwake kwa bei nafuu na ndio maana gharama zetu ni nafuu. Dhamira yetu ni kuwapatia wateja huduma bora zenye uhakika. Tunafahamu watanzania wanapenda michezo hususani soka na tunajitahidi kila siku kuwaletea michezo mizuri zaidi kama safari hii Copa America, awali tumeonyesha ligi za Bundesliga na Seriea A pamoja na kombe la vilabu bingwa duniani (ICC). Hivyo basi tunawaomba wateja wetu waichangamkie hii fursa kwa kufurahia kile wakipendacho na StarTimes.”

Michuano ya Copa America ilianza mnamo mwaka 1916 na mwaka huu inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake. Kwa mafanikio hayo waandaaji wameamua shamrashamra zake kufanyika nje ya ardhi ya bara la Amerika Kusini, yaani Marekani. Timu ya taifa ya Uruguay ndiyo inashikilia rekodi ya kutwaa ubingwa huo mara nyingi zaidi, mara 15 ikifuatiwa na Argentina mara 14 ambapo mara mwisho walichukua mwaka 1993, na kushika nafasi ya pili mara tatu mfululizo, safari hii tena wakiongozwa na mchezaji wao bora wa dunia mara tano, Lioneli Messi mastaa kibao, wanapewa nafasi kubwa zaidi ya kuibuka mabingwa.

Bingwa mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya taifa ya Chile ambayo inaongozwa na nyota kama Alexis Sanchez (Arsenal), Arturo Vidal (Bayern Munich) na kipa Claudio Bravo (Barcelona) ambapo walichukua ubingwa mwaka jana kwa mikwaju ya penati dhidi ya Argentina.

WAFANYAKAZI WA SERENGETI WAFANYA USAFI NA KUCHANGIA DAMU HOSPITALI YA TEMEKE

 Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) wakifanya usafi katika mazingira ya Hospital ya Temeke mwishoni wa wiki iliyopita katika maadhimisho ya shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke ambapo wafanyakazi hao walifanya usafi katika mazingira ya hospitali hiyo wakishirikiana na Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke na timu yake

Usafi ukiendelea katika mazingira ya Hospitali ya Temeke ambapo pia wafanyakazi wa SBL mapema wiki iliyopita ikiwa ni moja ya shughuli za kijamii pia walijitolea kuchangia damu na kupima afya zao  katika Hospitali hiyo

Wafanyakazi wa kiwanda cha Bia Serengeti wakiwa katika picha ya pamoja mapema wiki iliyopita mara baada ya kufanya usafi katika mazingira ya Hospitali ya Temeke 


Meneja wa Usalama na Afya kazin wa SBL Bwana David Mwakalobo akimkabidhi vifaa vya usafi Kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Temeke


Mmoja wa wafanyakazi wa kiwanda cha bia Serengeti (SBL) akichangia damu ambapo  zoezi hilo la kuchangia damu liliambatana na shamrashamra za kilele cha wiki ya usalama na afya kazini zilizoanzia kiwandani kwa matembezi ya hisani kuelekea katika hospitali ya Temeke


Dar es salaam;Wafanyakazi wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) leo wamechangia damu katika hospitali ya Temeke jijini Dar es salaam ikiwa ni moja ya mpango ya kampuni  kusaidia sekta ya afya nchini.

Uchangiaji wa damu ni moja ya shughuli za kusaidia jamii zinazoendana sambamba  na wiki ya afya na usalama kazini kwa kampuni hii,tukio hili linalofanywa kila mwaka likilenga viwanda vya bia na vinywaji vikali kuongeza ufahamu kwa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kuzingatia usalama sehemu za kazi.

Akiwashukuru wafanyakazi wa SBL kujitokeza kwa wingi kuchangia damu Meneja Uzalishaji wa kiwanda cha Dar es salaam Alice kilembe alisema zoezi hili linaenda sambamba na mipango ya kusaidia jamii na lengo ikiwa ni kusaidia   kuboresha afya zao.

“Tunapenda kuwashukuru wafanyakazi wote kujitokeza kuchangia damu .Tunaamini msaada huu wa damu utasaidia kuokoa maisha ya wale wanaohitaji na pia kusaidia kuboresha afya za watu wetu “alisema Kilembe

Mapema leo Kiwanda cha Serengeti cha Dar es salaam wameshiriki pia katika usafi wa mazingira kuzunguka katika maeneo ya Temeke jambo ambalo meneja uzalishaji wa kiwanda alisema ni “kuitikia wito wa serikali wa kuhakikisha usafi katika maeneo ya wazi”

Kwa mujibu wa Kilembe SBL haijakumbwa na matatizo katika maeneo ya kazi kwa zaidi ya miaka minne ikiwa ni matokeo ya mafunzo ya mara kwa mara kwa wafanyakazi na tahadhari zinazochukuliwa zinazofanya kampuni kukidhi viwango ya kimataifa vya usalama katika mazingira ya  kazi.

USAILI MAISHA PLUS MTWARA,FUNGA KAZI.

Ni asubuhi tulivu katika fukwe za bahari ya hindi kusini mwa Tanzania ambapo vijana wengi wamejitokeza kufanya usaili wa mashindano ya Maisha Plus East Africa 2016. Wapo wanaoonekana kujiamini na wengine wamejawa uoga. "Ni siku niliyoisubiri kwa hamu sana" anasema Faustine Komba miongoni mwa washiriki kutoka Mtwara.
678A0009
Safari ya msimu wa tano wa mashindano ya Maisha Plus imeanza rasmi kwa kuanza na usaili uliofanyika katika hotel ya NAF Beach iliyoko Mtwara. Washiriki kutoka mikoa ya jirani nao pia walijitokeza. "Maisha Plus kwangu ni ndoto ya muda mrefu sana, niliposikia mnakuja Mtwara nikasema piga ua lazima nishiriki" Anasema Ismail Likando aliyesafiri kutoka Lindi.
678A0022
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A9916
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A9925
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Maswali mengi yalilenga kupima uelewa wa vijana kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo mtazamo wao juu ya mwenendo wa kiuchumi. Mengine yalilenga kuwachanganya tu.
678A9961
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A9971
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Mshiriki Grace Pemba anaelezea changamoto mbalimbali alizokutana nazo kutokana na kuolewa akiwa na umri mdogo, anasema hadi sasa ana watoto wawili ambao wanaishi na baba yao. Alipoulizwa maswali zaidi Grace alijawa na simanzi na kujikuta akitoa machozi, "Nimelia kwa sababu mmenikumbusha nyuma nilikotokea" anasema Grace mfanyakazi wa Saloon kutoka mkoani Mtwara.
A video posted by Maisha Plus (@maishaplus2016) on Jun 4, 2016 at 6:47am PDT
678A9980
Mshiriki Grace Pemba akijifuta machozi.
Wakati usaili ukiendelea hali ya kujaa kwa maji baharini ilitokea na kulazimisha timu ya Maisha Plus kubadili utaratibu wa awali wa upigaji picha.
678A0075
Waandaaji wa mashindano ya Maisha Plus wakibadili utaratibu wa awali wa kupiga picha baada ya maji kujaa.
678A0046
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0056
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0281
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0279
Muhitimu wa shahada ya kilimo William Mbaga alibanwa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwemo faida za kilimo cha 'greenhouse' pamoja na namna ambavyo maziwa ya mtindi yanapatikana. William alijieleza kwa ujasiri.
678A0157
William Mbaga akiondoka baada ya kufanya usaili.
Washiriki wenye fani na ujuzi mbalimbali walijitokeza wakiwemo madereva bodaboda, mafundi, waigizaji, waimbaji, wasusi n.k
678A0223
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0083
Waigizaji pia walikuwemo katika usaili wa #MaishaPlusMtwara
678A0167
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0113
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0308
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
678A0328
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.

678A0336
Washiriki mbalimbali waliojitokeza katika usaili wa #MaishaPlusMtwara.
Mashindano ya Maisha Plus kwa mwaka huu yanatarajia kuchukua washiriki 30 kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya, Tanzania na Uganda ambapo mshindi atajishindia ufadhili wa wazo la biashara lenye thamani ya Tzshs. Milioni 30.
"Mwaka huu washiriki wajipange sana. Maandalizi yaliyofanywa kufanikisha msimu huu hayajawahi kutokea katika historia ya Maisha Plus. Ni kama tunaanza moja" Alisema Masoud Kipanya, miongoni mwa majaji na waanzilishi wa mashindano haya.
678A0145
"Tumewekeza katika teknolojia ya kisasa ili kupata picha za matukio yenye uhalisia zaidi. Watazamaji wategemee burudani safi isiyomithirika kupitia Azam Two." Alisema David Sevuri, miongoni mwa waanzilishi wa Maisha Plus.
Taarifa mbalimbali kuhusu mashindano haya zinapatikana kupitia tovuti rasmi ya www.maishaplus.tv

Saturday, June 4, 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI




NAIBU WAZIRI WA HABARI MGENI RASMI AZANIA BANK KIDS RUN 2016 YATAKAYOFANYIKA KESHO KUTWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR E SALAAM

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akimkaribisha Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), kuzungumza na wanahabari kuhusu mbio hizo zitakazofanyika kesho kutwa. Kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday.
 Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea (katikati), akizungumzia kuhusu mbio hizo.
 Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday (kulia), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya mbio hizo.
 Mwanafunzi Rachel Stephen wa Shule ya Sekondari ya Mburahati (kulia) na Mwenzake Ali Muhidin kutoka Shule ya Msingi Muungano wakizungumzia ushiriki wa mbio hizo.
 Wanahabbari wakichukua taarifa hiyo.
Waratibu wa mbio hizo wakionesha fulana zitakazotumiwa na watoto watakao kimbia mbio hizo. Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Ufundi ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Peter Mwita, Mratibu wa Mbio hizo, Wilhelm Gidabuday, Ofisa Masoko Mwandamizi wa Bank ya Azania, Othman Jibrea na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Tullo Chambo.

Dotto Mwaibale

NAIBU Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  Mbio za Watoto za Azania Kids Run 2016, 
 zitakazofanyika Jumapili Juni 5 jijini Dar es Salaam.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa Azania Kids Run 2016, zinazodhaminiwa na Benki ya Azania, Wilhelm Gidabuday, amesema kuwa Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi katika kinyang'anyiro hicho kitakachokuwa na mbio za kategori tano.

Gidabuday amebainisha kuwa, maandailizi yote ya Azania Kids Run 2016 yanaenda vema, ikiwamo idadi kubwa ya wazazi na walezi kujitokeza kusajili watoto wao, huku akiwataka wengi kutumia siku mbili zilizobaki kuhakikisha wanawapa vijana wao nafasi ya kushiriki.

"Mbio hizi zinazotarajia kushirikisha zaidi ya watoto 2,000, zinatarajia kufanyika Jumapili Juni 5, 2016 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, zikihusisha watoto chini ya miaka 16, ambako Naibu Waziri Wambura atakuwa mgeni rasmi," alisema Gidabuday.

Amewasisitiza wazazi, walezi na wadau kujitokeza kusajili watoto wao na kwamba fomu bado zinapatikana katika matawi yote ya Benki ya Azania, Ofisi za Baraza la Michezo la Taifa (BMT) zilizoko Samora Avenue na Ofisi za Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).

Gidabuday ametumia nafasi hiyo kuwahakikishia wazazi na walezi wa watoto watakaoshiriki Azania Kids Run 2016 kuwa, usalama wa watoto wao wakati wa shindano utakuwa kipaumbele chao na kuwatoa hofu ya usalama wakati wa kukimbia.

"Barabara zote zitakazotumiwa na watoto kukimbilia zitakuwa na uangalizi maalum ikiwa ni pamoja na gari za huduma ya kwanza na matibabu kwa watakaohitaji kupatiwa huduma hizo," amesema Gidabuday katika mkutano na wanahabari Dar es Salaam.

Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, amezitaja zawadi za washindi mbalimbali wa mbio hizo, huku akiweka msisitizo kwa kutawaka wazazi kuendelea kusajili watoto wao kuwa sehemu ya tukio hilo la kihistoria.

"Mshindi wa kwanza mbio za Kilomita 5 ni Sh. 200,000, mshindi wa pili Sh. 150,000 na mshindi wa tatu sh. 100,000, pamoja na medali, begi lenye vifaa vya shule na sare za michezo, wakati mshindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000," amesema.

Katika mbio za kilomita 2, Jibrea alitaja zawadi kuwa ni sh. 100,000 kwa mshindi, huku atakayeshika nafasi ya pili akitarajiwa kulamba sh. 75,000 na wa tatu kujitwalia sh. 50,000, kategori ambayo pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho cha sh. 15,000.

Aidha, amebanisha kuwa, kategori ya mbio za kilomita moja mshindi atatwaa sh. 75,000, huku wa pili akibeba sh. 50,000 na wa tatu akijishindia sh. 40,000, ambako pia washindi wa nne hadi wa 10 watapata kifuta jasho kama kilivyotajwa hapo juu.

Pia kutakuwa na mbio za mita 50 na 100, ambazo zitakimbiwa na watoto chini ya miaka mitatu, ambako washindi washindi wote watafunguliwa akaunti katika Benki ya Azania, itakayokuwa na kianzio cha sh.15,000, sanjari na begi la shule lenye vifaa vyote muhimu.

SERIKALI YATOA UFAFANUZI KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA NA MWANDISHI WA " THE ECONOMIST" GAZETI LA KIINGEREZA.

 Kaimu  Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam mchana huu wakati akitoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mwandishi wa " The Ecomist" Gazeti la Kiingereza linatoka kwa wiki dhidi ya Serikali ya Tanzania. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda. 
 Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TCI), Daud Biganda (kulia), akitoa ufafanuzi wa Uchumi tangu Rais Dk. John Magufuli aingie madaraka na miradi iliyosajiliwa na kituo hicho.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea.
 Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Taarifa akichukuliwa na wanahabari.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imekanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Kiingereza linalotpka kila wiki lililodai kuwa Rais Dk.John Magufuli anaongoza nchi kwa msukumo licha ya kuonekana mzuri na kuwa taarifa hiyo imelenga kuupotosha umma.

Habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo ilikuwa na kichwa kilicho andikwa "Government by gesture, A President who looks good but governs impulsively"

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa ufafanuzi wa habari hiyo Kaimu  Mkurugenzi wa Idara Habari Maelezo, Zamarad Kawawa alisema taarifa hiyo haikuwa na uzalendo na amewataka wanahabari kuwa makini na habari zenye mlengo wa kupotosha taifa.

"Nawaombeni wanahabari wenzangu kuweni makini na taarifa zenye mlengo wa kupotosha umma" alisema Zamarad.

Akitoa ufafanuzi kuhusu suala la uchumi Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Daud Biganda alisema taarifa hiyo siyo sahihi na imelenga kupotosha na inavuruga ukweli kwani Tangu Rais Dk.John Magufuli aingie madarakani kwa kipindi cha kati ya mwezi Desemba 2015 na 2016, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeweza kuandikisha miradi ya uwekezaji ipatayo 551 yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 9,211.88 kati ya miradi hiyo miradi 229 yenye asilimia 42 inamilikiwa na watanzania, miradi 215 yenye asilimia 39 inamilikiwa na wageni na miradi 107 yenye asilimia 19 inamilikiwa kwa njia ya ubia kati ya watanzania na wageni.

Biganda alisema kuwa miradi yote hiyo ya uwekezaji ilitarajiwa kuzalisha ajira zipatazo 55,970 na kuleta matokeo mengine kwa watanzania na kuwa imesajiliwa na TIC.



"JIPU IDARA YA MALIASILI WILAYA YA SIKONGE"

Thursday, June 2, 2016

FASTJET YATANGAZA SHINDANO LINGINE KWA WATEJA WAKE


Dar es Salaam 30 Mei 2016 –  fastjet, shirika la ndege la bei nafuu Afrika  limezifanya ndoto za usafiri  kuwa za kweli  kwa abiria wake zaidi ya milioni mbili  waliopaa anga za Afrika tangu kuzinduliwa kwake Novemba 2012.


 Ukiwa kama mkakati wa kuhamasisha hata Watanzania wengi zaidi  kusafiri, fastjet  imetangaza kwamba abiria yeyote anayenunua tiketi  kuanzia Jumanne Mei 31 ataingia kwenye  bahati na nasibu  ya kwanza ya aina yake  ijumulikanayo Big 10 draw ambapo washindi 10 watasafiri bure   katika njia yoyote  ya fastjet katika mtandao wake barani Afrika.


Kwa watu kumi watakaoshinda bahati nasibu hiyo  shirika linawapa uwezo wa kwenda katika mapumziko  au kwenda katika safari ya manunuzi  pamoja na marafiki  na familia  jambo wamekuwa wakiliwazia  kila mara.


Ama kwa wajasiriamali wa Tanzania, safari hiyo inaweza kutumia kukuza mahitaji ya biashara kwa kuokoa  gharama za usafiri katika safari nyingine kumi wanazozihitaji  kusafiri.


 “Ni rahisi, lengo la fastjet ni kufanya uwezekano kwa wateja wengi kusafiri, iwe ni kwa shughuli za biashara, kutembelea marafiki  na familia, au kufurahia burudani ya kusafiri,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania John Corse.


 Njia ambazo zinahusiana  kwa ajili hiyo ni safari za kutoka Dare es Salaam kwenda Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Nairobi, Entebbe, Lusaka, Harare na Johannesburg hali kadhalika safari  kati ya Kilimanjaro na Harare.


 Tiketi zitakazonunuliwa Jumanne Mei 31, 20016 kwa njia za kimataifa na  za ndani  zitawawezesha abiria wake kuingia katika bahati nasibu ya Big 10. Washindi watatangazwa Juni 2016 na safari 10 za bure  ni lazima zifanyike  kabla ya Desemba 11, 2016.


 Ikitambuliwa kama shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, fastjet hivi sasa inafanya safari  ndani ya nchi 11 kwa wafanyabiashara, watali na familia ambazo zimeipokea tozo lake la nauli nafuu na linalofikia kwa usafiri wa anga.


 “Usafiri wa anga ni ufunguo unaoendelea kuhamasisha na kukuza uchumi wa Tanzania  kwa kuufanya uwe rahisi kwa familia, wafanya biashara  na watalii kumudu kusafiri,” alisema Corse  na kuongeza, “tumezindua punguzo hili la nauli  hivyo kwamba hata wasafiri wanaweza kuzoea usafiri wa anga wanaoumudu, iwe wanasafiri kwa ajili ya biashara au mapumziko.”


Kukata tiketi kiunaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia www.fastjet.com, kupitia wakala aliyethibitishwa au kwa kuwasiliana na na fastjet kupitia +255 784 108 900. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa fedha taslimu, kwa njia ya mtandao kwa kutumia kadi au  malipo kwa njia ya mitandao ya simu.