Pages

KAPIPI TV

Tuesday, May 31, 2016

VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUJIUNGA NA MASHIRIKA YA KUJITOLEA ILI WAJIONGEZEE UJUZI NA MAARIFA.

Vijana nchini Tanzania wameshauriwa kuwa tayari kufanya kazi kwa kujitolea ili kujiongezea ujuzi, uwezo, maarifa na kuleta mabadiliko katika jamii zao,hayo yalielezwa na Meneja wa Maendeleo ya Vijana wa shirika la Raleigh Tanzania, Genos Martin wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari hii.

Martin alisema kuwa ni vyema kwa vijana kujiunga na mashirika ya kitaifa na ya kimataifa ya kujitolea kwani kwa kufanya hivyo kutawapa vijana fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa ambao utawasaidia katika sehemu mbalimbali.
Martin alisema, "Kufanya kazi kwa kujitolea ni kitu kigeni nchini kwetu tofauti na Mataifa ya nchi zilizoendelea, watu waliowahi jitolea wanapewa kipaumbele kwenye maombi ya kazi tofauti na nchini kwetu. Hii inafanya kujitolea kuwa jambo la muhimu sana kwenye mataifa ya wenzetu" 

"Vijana wengi wanalalamika kuwa nafasi nyingi za kazi zinawataka wawe na uzoefu wa miaka mitatu nakuendelea, hawajui ni vipi wanaweza kupata uzoefu lakini kama wakijiunga na haya mashirika ya kujitolea wanaweza pata huo uzoefu na kuwafanya wawe na nafasi nzuri pindi waombapo ajira" aliongezea Martin.

Aidha, Afisa Mawasiliano wa Raleigh Tanzania, Kennedy Mmari alieleza kuwa ni kawaida ya shirika hilo kutafuta vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini ambao huungana na vijana wenzao kutoka mataifa ya mbali mbali ya Ulaya na Amerika.

Mmari aliongezea, "Raleigh tuna programu kwa vijana zinazohusu ujasiriamali, usafi, maji na utunzaji wa mazingira, kijana yeyote anaweza kujjiunga nasi na kufanya program zetu. Hatutoi malipo yoyote wala hawatulipi chochote isipokuwa tunagharamia mahitaji yao yote ya msingi pindi wakiwa kwenye programu"
Wanafunzi wa shule ya Msingi Chibe iliyopo kata ya Old Shinyanga mkoani Shinyanga wakishuhudia ufunguzi wa kituo cha elimu ya awali kilichojengwa na na vijana wa kujitolea kwa msaada wa shirika la Raleigh Tanzania.
Kwa upande wa vijana waliofanya programu na shirika hilo  wameshukuru kwa nafasi waliyopewa kwani imewasaidia kupata ujuzi na ufahamu wa mambo tofauti ikiwemo jinsi ya kuandaa na kusiammia biashara.

Mmoja wa vijana ambao wamepata fursa hiyo, Sia Malamsha,  alisema kuwa anajiona wa tofauti baada ya kumaliza programu, hakuwahi fikiria kama kuna watu Tanznaia hawana huduma za maji safi na salama lakini kupitia programu za Raleigh nimeweza fika kwenye jamii hizo na kuwasaidia kutatua matatizo hayo.
"Nimekuwa sehemu ya mabadiliko makubwa katika nchi yangu, najivunia kuona nimefanya kitu kuikomboa jamii ya Watanzania" aliongezea Bi. Malamsha.

Vijana wa Shirika la kujitolea la Raleigh wakishiriki ujenzi wa choo katika moja ya miradi yao
Naye kijana Ashiru Said aliyefanya programu ya ujasiriamali amesema kua programu za Raleigh zimemsaidia kupata elimu ya kusimamia na kuendesha biashara.
"Nimeweza kupata elimu ya ujasiriamali, baada ya kurudi nyumbani jamii imefaidika na elimu niliyoipata kwani nimeweza waelimisha vijana wenzangu jinsi ya kuanzisha na kusimamia biashara zao wenyewe" alimalizia Said.

Raleigh Tanzania ni shirika lisilo la kiserikali lenye ofisi zake mkoani Morogoro na kufanya programu za kujitolea kwa lengo  la kuisaidia jamii ya Tanzania sehemu mbalimbali.

MISS TANZANIA USA PAGEANT AEESHA KAMARA TEMBELEA, KUONGEA NA KUTOA MSAADA KENTON HIGH SCHOOL

Miss Tanzania USA 2015-2016 Aeesha Kamara akiongea na wanafunzi wa Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam siku alipotembelea shuleni hapo katika moja ya majukumu yake ya kuhudumia jumuiya. Miss Kamara anadhamini wanafunzi wawili shuleni hapo
Miss Tanzania USA Pageant Aeesha Kamara akimkabidhi msaada mwalimu mipira siku alipotembela shule ya Kenton High School ya Tabata jijini Dar es Salaam.
Miss Tanzania USA Aesha Kamara akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wawili anaowadhamini kwa kuwasomesha shuleni hapo.
Picha ya pamoja

JK AWAFUNDA VIJANA WA CCM VYUO VIKUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete akihutubia katika mahafali ya 2016 ya Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu wa CCM yaliyofanyika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam.
 Vijana vyuo vikuu Dar es Salaam wakiserebuka katika mahafali yao.
 Vijana hao wakiendelea kuserebuka.
 Hapa ni furaha kwa kwenda mbele.
Ni kama wanasema'  Hapa ni ushindi tu 2020 kwani vijana tumejipanga.
Vijana wakiwa kwenye mahafali hayo.

Friday, May 27, 2016

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIRUSHA KUTOKA KWENYE MNARA WA SIMU JIJINI MWANZA

Kijana Mmoja (picha) Jijini Mwanza amenusurika kifo baada ya kujirusha kutoka katikati ya mnara wa simu.
Na BMG
Tukio hilo limetokea hii leo na kuvuta watu wengi waliofika kumshuhudia kijana huo ambae amepanda katika mnara huo tangu majira ya asubuhi na kukatalia mnarani hadi majira ya saa sita mchana.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao pia ni marafiki wa karibu na kijana huyo, wamesema huenda kijana huyo amefikia maamuzi hayo kutokana na ugumu wa maisha ambao amekuwa akiulalamikia huku wengine wakisema ni kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo gundi ambayo amekuwa akiyatumia.

Akizungumza kwa niaba ya Kamanda wa jeshi la uokoaji na zima moto mkoani Mwanza, mmoja wa maafisa wa uokoaji Mussa Kaboni, amsetoa rai kwa makampuni yenye minara ya simu kuimarisha ulinzi katika minara hiyo ili kuondoa hatari inayoweza kujitokeza kutoka kwa raia wasio wema.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walionekana kuchukizwa na kitendo cha kijana huyo na kusikika wakifoka kwa hasira na makelele ya hali ya juu "rukaa, ruka sasa, jirushe kama wewe ni mwanaume" hali ambayo ilikuwa ikimuongezea morari kijana huyo na hivyo kujirusha kweli kutoka katikati ya mnara huo.


Baada ya kijana huyo kujirusha kutoka katikati ya mnara hadi chini, alipoteza fahamu na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mwanza, Sekour Toure kwa ajili ya huduma ya kwanza.

MULTICHOICE TANZANIA YAADHIMISHA SIKU YA AFRIKA NA WADAU WAKE DAR

DSC_4273
Social Media Administrator wa MultiChoice (DStv) Tanzania, Shumbana Walwa akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam. (Picha na Modewjiblog)
Kampuni ya MultiChoice Tanzania wasambazaji wa bidhaa za DStv nchini usiku wa Mei 26 wameweza kujumuika kwa pamoja katika kusheherekea siku ya Afrika kwa kukutana na wadau wake Jijini Dar es Salaam na kufurahia paamoja fahari ya Afrika.
Wadau hao ni pamoja na wanahabari, Waendesha vipindi vya televisheni na radio, wasanii na baadhi ya wateja ambao walijumuika kwa pamoja usiku maalum ambao pia walipata kula na kunywa pamoja na kubadilishana mwazo.
Awali wakati wa ufunguzi wa hafla hiyo maalum, Meneja Uhusiano na Masoko wa MultiAChoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu alieleza kuwa, MultiChoice wanajisikia fahari katika ushiriki wao wa kuleta mabadiliko na maendeleo tangu kuanzishwa hapa Barani Afrika miaka 20 iliyopit huku ldngo kuu ni kuwa na maudhui ya kila siku ya kiafrika.
Aidha, Bi. Furaha Sumalu alibainisha kuwa, kwa kuthamini Afrika, hata chaneli wameweka zinazolenga Afrika zikiwemo: Africa Magic, Maisha Magic Bongo, Maisha Magic East ambapo ndani ya chaneli hizo zimekuwa na mtazamo tofauti kuhusu Afrika hivyo watanzania na waafrika kwa ujumla ni wakati wa kuchangamkia bidhaa bora za DSTV ilikufurahia uhondo huo wa Kiafrika na mambo mbalimbali yanayotokea ndani ya Afrika nan je ya Afrika.
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
DSC_4291
Meneja wa Fedha wa kampuni ya Multichoice Tanzania, Bw. Francis Senguji akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4286
Meneja Mauzo wa Kampuni ya MultiChoice Tanzania, Salum Salum akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4283Mchora vibonzo, Bwana Masoud Kipanya akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4707
Msanii wa muziki bongo fleva Queen Darleen ambaye ni ndugu na msanii wa muziki 'Diamond Platnumz' akiwa katika pozi na mmoja wa mashabiki wake wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4352
Mdau na Mwanahabari Sylvester akipata picha kwenye red Carpet akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4705
Msanii wa muziki bongo fleva Queen Darleen ambaye ni ndugu na msanii wa muziki 'Diamond Platnumz' akiwa katika pozi na Mwandishi Mwandamizi wa mtandao wa Modewjiblog, Bwana Andrew Chale wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4309
Mshiriki wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother III, Latoya Lyakurya, akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4336
Levina Bandihai wa Multichoice Tanzania akiwa katika pozi wakati wa hafla hiyo ya siku ya Afrika ambapo wadau mbalimbali walijumuika kwa pamoja kusheherekea siku hiyo iliyofanyika usiku wa Mei 27. Jijini Dar es Salaam
DSC_4300 DSC_4322
Msanii JB akiwa katika pozi kwenye red Carpet..
DSC_4273 DSC_4311 DSC_4274 DSC_4323
Meneja Uhusiano na Masoko wa MultiChoice Tanzania, Bi. Furaha Samalu akifanya mahojiano na wanahabari wakati wa tukio hilo
DSC_4356
Wadau na staff wa DSTV wakiwa katika pozi.
DSC_4369 DSC_4276 DSC_4316
kikundi cha ngoma cha NIMUJO Edutaiment wakifanya mambo yao katika usiku huo wa Afrika uliondaliwa na DSTV
DSC_4318 DSC_4359 DSC_4368
Msanii Uwoya (kulia) akiwa katika red carpet..
DSC_4377
Wadau wa DSTV, wakifuatilia tukio hilo
DSC_4424 DSC_4415
Burudani za ngoma zikiendelea
DSC_4382 DSC_4413 DSC_4403
Baadhi ya watendaji wakuu wa DSTV wakitambulishwa
DSC_4414 DSC_4415 DSC_4327 DSC_4355 IMGS2383 DSC_4464
Muda wa 'msosi' ulikuwa kama hivyo pichani.
DSC_4454 DSC_4470 DSC_4485 DSC_4479 DSC_4490 DSC_4482 DSC_4464
DSC_4515
Burudani zilipamba moto zaidi..DSC_4524 DSC_4535
Msanii Shilole 'Shishi bebi' akitangaza bahati nasibu ya mshindi w dikoda ya DSTV Exp
DSC_4551
Mshiriki wa Tanzania kwenye Shindano la Big Brother III, Latoya Lyakurya, akipokea zawadi ya dikoda ya DSTV
DSC_4564
Msanii Richie Richie akimtangaza mshindi wa DSTV
DSC_4568
Mwanablog ya Fullshangwe, John Bukuku akishangilia baada ya kutangaza kushinda zawadi ya dikoda ya DSTV
DSC_4576
Mwanablog ya Fullshangwe, John Bukuku akipokea dikoda yake
DSC_4585
Mke wa msanii Sheta, Leila Yusuph 'Mama Quila' akisoma jina la mshindi
DSC_4602 DSC_4612
Mmiliki wa mtandao wa Wananchi, Bw. William Malecela 'Lemutuz' akitangaza jina la mshindi
DSC_4621 DSC_4629
DSC_4638
Meneja Uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo akikabidhi zawadi
DSC_4650
Baadhi ya staff wa DSTVDSC_4664
Othuman Michuzi wa blog ya Mtaa kwa Mtaa akipokea zawadi yake wakati wa hafla hiyo ya usiku wa Afrika na DSTV.
DSC_4671 DSC_4675 DSC_4689
Wadau wakisakata rhumba.
IMGS2383
Wasanii wa kundi la NIMUJO Edutaiment wakicheza ngoma za makabila mbalimbali wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).