Pages

KAPIPI TV

Tuesday, May 17, 2016

MWANAMUZIKI NGURI WA DANSI NCHINI, ZAHIR ALLY ZORO AWAKOSHA WAKAZI WA JIJINI MWANZA

Mwanamuziki wa siku nyingi nchini kwenye muziki wa dansi na rumba, Zahir Ally Zoro (pichani) usiku wa kuamkia leo (jumamosi mei 14,2014) amewaburudisha wakazi wa Jiji la Mwanza baada ya kufanya show kali katika Ukumbi wa Kilimanjaro Hotel, Nyegezi.

Ilikuwa ni show yake ya kwanza kwa mwaka huu 2016 ambapo wapenzi wa muziki wa dansi na rumba walivutiwa na burudani iliyotolewa na Zoro hasa baada ya kuimba live wimbo uitwao "Beatrice" ambao ni wimbo uliofanya vizuri sana wakati anauachia akiwa na band yake ya Mass Media.

KIPINDI CHA JUKWAA LANGU MAY 16 2016. ZIARA YA WAZIRI MKUU UK. URAIA PACHA

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na waTanzania waliojumuika kumsikiliza jijini London

Kipindi cha JUKWAA LANGU hukujia kila Jumatatu kikiongozwa na Mubelwa Bandio toka Beltsville Maryland, USA, kuzungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu Tanzania ya sasa na ile tuitakayo.
Ni Tanzania kutoka jicho la DIASPORA
Na katika kipindi cha juma hili, tulizungumza na Chris Lukosi, ambaye alitupa muhtasari wa ziara ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa huko nchini Uingereza.
Muhtasari huo ulizua na mjadala mkali juu ya ahadi za serikali kuhusu vibali maalum kwa waTanzania waishio nje ya nchi.
Karibu

Friday, May 13, 2016

WAUGUZI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO JIJINI MWANZA WAOMBA KUTOBAGULIWA

Jana May 13,2016 Tanzania imeungana na Mataifa mbalimbali duniani kuadhimisha "SIKU YA WAUGUZI DUNIANI" ambapo Kitaifa Maadhimisho hayo yamefanyika Mkoani Geita.
Imeandaliwa na BMG

DIAMOND PLATNUMZ KUWASHA MOTO DALLAS TEXAS,MAREKANI MEMORIAL WEEKEND JUMAMOSI MEI 25

INFO CALL-301-366-9611 / 240-605-1870 /713-373-6525

MeTL YAKANUSHA KUFICHA SUKARI, YAELEZA HALI HALISI

industrial sugar


Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imekanusha taarifa ambayo ilitolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa kampuni hiyo imeficha sukari tani 2,990 katika Bandari Kavu (ICD) ya PMM iliyopo Vingunguti, Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutembelea ICD na kukuta tani 2,990 ambazo aliambiwa kuwa ni mali ya Mohammed Enterprises jambo ambalo halikuwa na usahihi bali ni mali ya Tanzania Commodities Trading inayomilikiwa na Murtaza Dewji.
Kwaa mujibu wa Murtaza Dewji ambaye ndiyo mmiliki wa sukari hiyo amesema kuwa sukari hiyo iliingia nchini kwa kufata utaratibu wote kama jinsi inavyotakiwa na anashangazwa kwanini hakufatwa ili kutoa maelezo kuhusu sukari hiyo.
“Tulifuata taratibu zote zikiwepo mamlaka husika za nchi kma bodi ya sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” amesema Murtaza.
Akifafanua zaidi amesema kuwa sukari hiyo ilikuwa njiani kuelekea nchini Uganda na vielelezo vyote vipo lakini kutokana na uhaba wa sukari nchini, serikali iliagiza mzigo huo kubaki nchini na kuingiza sokoni ili kumaliza tatizo hilo ambapo ulitakiwa kuanza kuingia sokoni kati ya Mei, 12 na Mei, 13.
Aidha ameelezea kuwa ni jambo la kawaida kuagiza sukari kutoka Dubai kwani hutumia siku 7 pekee kufika nchini tofauti na sukari kutoka Brazil ambayo hutumia siku 50 hadi 60 ikiwa njiani hadi kufika nchini.
“Wafanyabiashara wote wanaojua biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi sio wa kwanza kuagiza sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai,” amesema Murtaza.
Pia Murtaza amewatoa hofu Watanzania kuhusu uhaba wa sukari kwa kusema kuwa tayari sukari imeagizwa na ndani ya wiki mbili kutakuwa na sukari ya uhakika nchini hivyo kuwataka kuondoa hofu iliyokuwapo hapo awali.
Kibali halali cha TFDA hiki hapa chini

Wednesday, May 11, 2016

WARAMI WAMPONGEZA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KWA KUWATETEA WANYONGE,WASEMA ANAPIGWA VITA NDANI NA NJE YA BUNGE

12John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka WARAMI akizungumza na waandishi wa habari Kwenye Hoteli ya Tamarin Mwenge jijini Dar es salaam kuhusu Sakata la Sukari ambapo amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa jinsi anavyothubutu kuwatetea watanzania waliowanyonge katika masuala mbalimbali na hasa katika suala zima la uhaba wa sukari.
Kuna tani nyingi za sukari zimekamatwa katika msako maalum ambao Rais aliamrisha vyombo vya dola kufuatilia wafanyabiashara wasio waaminifu walioficha sukari, baada ya zoezi hilo kuanza sukari nyingi imeendelea kukamatwa maeneo mbalimbali nchini ikiwa imefichwa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu.
WARAMI inapongeza jitihada zote za dhati anazozifanya Rais Magufuli na Serikali yake za kuhakikisha watanzania wanaishi kwenye usawa, lakini pamoja na hayo wanapendekeza mambo kadhaa yafanyika na jeshi la polisi
Mratibu huyo wa Taasisi ya WARAMI amelitaka jeshi la polisi kutoa taarifa rasmi juu ya wafanyabiashara wanaotamba barabarani kuwa wameliweka jeshi hilo mfukoni kwamba hakuna wa kuwafanya lolote katika nchi hii.
Taasisi za kiserikali zifafanue juu ya tabia hii ya wafanyabiashara kutumia picha za viongozi kwa maslahi yao kama, ni haki ama si haki.
Kiongozi huyo wa WARAMI akaongeza kwamba hivi sasa Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli anayo vita kubwa kutokana na kazi anayoifanya ya kuwatetea watanzania waliowanyonge anayo vita ndani ya bunge na nje ya Bunge
Kutokana Na Hoja Ambazo Zimekuwa Zikitolewa Na Baadhi Ya Wabunge Zikikosoa Utendaji Wa Rais, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakifaidika na baadhi ya mambo hivyo wasingependa mabadiliko ya kumkomboa mwananchi wa kawaida yatokee, katika picha kushoto ni Makdeo Makeja mratibu msaidizi WARAMI
13 14Makdeo Makeja mratibu msaidizi WARAMI akifafanua jambo wakati viongozi hao wa taasisi ya WARAMI walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam , kulia ni John Marwa Mratibu wa Chama cha Watetezi wa Rasilimali Wasio na Mipaka WARAMI

MAMA YAKE TEDDY MAPUNDA MAREHEMU BENADETTE IZENGO AZIKWA MAKABURI YA KINONDONI

001
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanania Dk. Gharib Bilal wa tatu kutoka kushoto na Mama Salma Kikwete wa kwanza kushoto wakishiriki mazishi ya Merehemu Benadette Izengo mama wa Mkurugenzi wa kampuni ya Montage Limited Teddy Mapunda aliyekaa katikati yao pamoja na wanafamilia wengine wakati wa mazishi yaliyofanyika kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanis kuu la Mtakatifu Joseph.
01
Mke wa Rais Mstaafu Dk Jakaya Kikwete Mama Salma Kikwete akiweka mchanga kaburini wakati aliposhiriki mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo yaliyofanyika jana kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
02Balozi Asha Rose Migiro akiweka mchanga kaburini wakati wa maishi ya marehemu mama Benadette Izengo.
1Fathre Matumaini akiongoza ibada ya mazishi ya Marehemu Mama Benadette Izengo iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Josepha jana.
2Wanafamilia wakiwa katika ibada ya mazishi iliyofanyika kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana jijini Dar es salaam na kufuatiwa na mazishi yaliyofanyika kwenye makaburi ya Kinondoni.
3Teddy Mapunda na Ndugu yake wakiwa pembeni mwa jeneza la mama yao mpendwa marehemu Benadette Izengo.
4Mkwe wa Marehemu mama Benadette Izengo akishiriki ibada ya mazishi pamoja na ndugu na jamaa wa familia kwenye kanisa la Mtakatifu Joseph jana.
5Wajukuu wa marehemu wakishiriki ibada hiyo jana.
6Wana familia wakiwa na majonzi kwa kuondokewa na mpendwa mama yao Marehemu Mama Benadette Izengo.
7Mwenyekiti wa Chama cha UDP Mzee Jon Momose Cheyi akishiriki sakramenti ya bwana kutoka kwa Father Kaombwe wakati wa ibada hiyo ya mazishi
8Teddy Mapunda na Mumewe Nestor Mapunda wakiwa na majozni huku wakiangalia jeneza la mama yao mpendwa marehemu mama Benadette Izengo.
9Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salaam.
10Kutoka kushoto ni Jeseph Kusaga Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Enertainment, Nandi Mwiyombela, Justin Pamba, Godfrey Kusaga na John Mbele nao walishiriki katika mazishi hayo ya mama Bebadette Izengo.

Monday, May 9, 2016

WATANZANIA KUSHUHUDIA COPA AMERICA LIVE KUPITIA STARTIMES

 Meneja Uhusiano wa Kampuni ya StarTimes Tanzania, Mohamed Kimweri (kushoto), akizungumza katika na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu kampuni hiyo kupata haki za kuonesha michuano ya Copa Amerika moja kwa moja ambayoitafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu. Kulia ni Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri.
 Meneja Maudhui wa kampuni hiyo, Paulina Kimweri, akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya StarTimes Tanzania imefanikiwa kupata haki za kuonyesha michuano ya Copa America moja kwa moja ambayo itafanyika nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi wakati wa uzinduzi huo Makamu wa Rais wa kampuni hiyo nchini,  Zuhura Hanif alisema kuwa kupatikana kwa haki za kuonyesha michuano hiyo mikubwa na mikongwe ulimwenguni ikiwa inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ni jitihada za kuhakikisha kuwa wateja wao wanafurahia vipindi bora vya michezo na burudani.

“Leo StarTimes inayo habari njema kuwataarifu kuwa tumepata haki maalum za kuonyesha michuano ya Copa America moja kwa moja kutoka nchini Marekani kuanzia Juni 3 mpaka Juni 26 mwaka huu. Ninaposema haki maalumu manake ni kwamba watanzania hawataweza kushuhudia michuano hii sehemu yoyote isipokuwa kupitia king’amuzi cha StarTimes pekee. 

Alisema wateja wao na wapenzi wa soka nchini wataweza kushuhudia michezo yote 32 ambapo itazikutanisha timu 16 za bara la Amerika ya Kusini na mwenyeji Marekani zitazoumana katika viwanja 10 tofauti nchini Marekani ikiwa ni kwa mara ya kwanza kufanyikia huko.” Alisema Hanif.

Hanif aliwataka watanzania na wapenda soka kwa ujumla kujiandaa kushuhudia mechi kali za miamba ya soka kutoka bara la Amerika ya Kusini ambazo itayakutanisha majina makubwa katika ulimwengu wa mpira wa miguu kama vile; Lionel Messi, Kun Aguero (Argentina), Alexis Sanchez, Arturo Vidal (Chile), Neymar, Marcelo (Brazil), Luis Suarez, Edinson Cavani (Uruguay) na wengineo.

“Ninafahamu kuwa watanzania ni miongini mwa mashabiki wakubwa wa mchezo wa soka hivyo watafurahia zaidi kuwatazama wachezaji wanaowapenda wakiwakilisha mataifa yao katika michuano hii. Tayari tumekishashuhudia ligi mbalimbali ulimwenguni zikielekea ukingoni kama vile ligi za Bundesliga na Serie A za Ujerumani na Italia ambazo tayari timu za Bayern Munich na Juventus zimaeshatangazwa mabingwa. Na nafurahi kuwa ligi hizo zote mbili zilionekana moja kwa moja kwenye chaneli za michezo za ving’amuzi vyetu kwa malipo ya gharama nafuu kabisa ya mwisho wa mwezi kuanzia sh. 5,000 aliongezea

“Ningependa kuchukua fursa hii kuwataka watanzania na wateja wetu kwa ujumla kuwa michezo na burudani kwetu StarTimes ndio nyumbani. Kwa kuliona hilo baada ya kufaidi mechi za ligi kuu za Ujerumani na Italia sasa tumewaletea Copa America kuhakikisha kuwa mnafurahia vema luninga zenu. 

Mbali na michuano hii tunaahidi kuendelea kuwaletea michuano mingine kama awali tulivyofanya kwa Kombe la Dunia la Wanawake, Kombe la Vilabu Bingwa Duniani, Kombe la Dunia la Vijana chini ya Miaka 20 na miningineyo. Nawasihi wateja wetu kukaa mkao wa kula na wasiojiunga nasi wafanye hivyo ili kufaidi uhondo huu utakaowajia hivi punde kwenye luninga zao.” Alisema Hanif.

Michuano ya Copa Amerika inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi Juni kuanzia tarehe 3 mpaka 26 mwaka 2016 ni michuano mikongwe zaidi duniani ikiwa inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake ambapo nchi ya Uruguay inashikilia rekodi ya kuchukua mara nyingi zaidi, mara 15 ikifuatiwa na Argentina mara 14. Michuano ya mwaka huu itakuwa ni ya kusisimua zaidi hasa kwa bingwa mtetezi nchi ya Chile kutetea ubingwa wake, ambapo aliuchukua mwaka 2015 baada ya kuishinda timu ya taifa ya Argentina kwa mikwaju ya penati.

NAIBU WAZIRI ANGELINA MABULA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA NHC

001Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua rasmi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye makao makuu ya shirika hilo Upanga jijini Dar es salaam ambapo alilipongeza shirika hilo kwa kazi nzuri ambayo wafanyakazi wake wanaifanya kwani ndiyo shirika pekee la Serikali linaloendeshwa kwa ufanisi mkubwa na kuiletea heshima serikali, Waziri Mabula amewaambia wafanyakazi wa shirika hilo pamoja na Menejimenti yake kuendelea na kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya ili kuleta maendeleo zaidi nchini katika sekta ya nyumba.PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM
01Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi katika mkutano uliofanyika mwishoni mwa wiki katikia makao makuu ya shirika hilo Apanga kulia ni Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na kushoto ni Adolf Kasegenya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TAMICO NHC.
1Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu kulia na Adolf Kasegenya Katibu wa Baraza la Wafanyakazi TAMICO NHC kushoto wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
3Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula na Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo.
4Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt Angeline Mabula akipitia nyaraka huku Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akizungumza na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya kumkaribisha ili kufungua rasmi mkutano huo.
5 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akizunguma na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya Waziri Angelina Mabula kuufungua rasmi.
6 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu akisisitiza jambo wakai akizunguma na wafanyakazi wa shirika hilo kabla ya Naibu Waziri Angelina Mabula kuufungua rasmi.
7Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Nyumba wakifuatilia mkutano huo.
8Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiimba wimbo wa wafanyakazi kabla ya kufunguliwa kwa mkutano huo.
9Wafanyakazi wa shirika la Nyumba wakiwa katika mkutano huo.
11 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
12 Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.
13
Mkurugenzi wa Shirika hilo Bw. Nehemia Mchechu na Naibu Waziri Angelina Mabula wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa shirika hilo baada ya kuufungua rasmi mkutano huo.

MTANGAZAJI WA CNN RICHARD QUEST AFURAHISHWA NA VIVUTIO VUA UTALII TANZANIA KATIKA MAONESHO YA INDABA

Kwa mara nyingine tena Tanzania inashiriki katika onesho la kimataifa la Utalii la INDABA yanayofanyika huko Afrika Kusini maonesho hayo yalianza jana tarehe 7 Mei na yanatarajiwa kumalizika tarehe 9 Mei, 2016. jijini Durdan, Bodi ya Utalii (TTB) ndio waratibu wa onesho kwa upande wa Tanzania. Katika onesho hili TTB inashirki pamoja na taasisi za TANAPA na Mamlaka na Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makampuni mbalimbali binafsi Zaidi ya 30 ya sekta ya Utalii .
Katika siku yake ya kwanza Banda la Tanzania limetembelewa na wadau wengi wakiwemo watalii, waandishi wa habari za utalii, mawakala wa Utalii nk. Miongoni mwa watu mashuhuri waliotembelea Banda la Tanzania ni Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest ambaye alifurahishwa na vivutio vua utalii nchini Tanzania mara baada ya kupata maelezo kutoka kwa Maofisa wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB.
A05Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimuonyesha jambo Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini..
A3Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian akimpa maelezo kuhusu vivutio vya utalii nchini Tanzania Mwandishi maarufu na mtangazaji wa Kimataifa kutoka Shirika la habari la CNN la Marekani Bwana Richard Quest wakati alipotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni Bi Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB.
A4 A5Baadhi ya wagenimbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya Utalii ya Indaba yanayofanyika katika jiji la Durban nchini Afrika Kusini.
A1Mkurugenzi wa Masoko kutoka Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bwa Philip Sebastian na Bi. Devotha Mdachi Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB. wakiwa na mmoja wa wageni aliyetembelea katika banda la Tanzania katika maonesho ya kimataifa ya Utalii Indaba jijini Durban nchini Afrika Kusini Katikati ni
A2Baadhi ya wageni wakipata taarifa mbalimbali kutoka katika banda la Tanzania.
A7Wageni mbalimbali wakiwa katika banda la Tanzania.

Sunday, May 8, 2016

WANAMUZIKI WA NYIMBO ZA INJILI WAJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Joyce Hagu (wa pili kushoto), akimkabidhi Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel, kadi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),  katika hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo kwa waimbaji wa nyimbo za injili uliofanyika Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima na Rais wa chama hicho, Ado Novemba.
 Hapa mwimbaji nguli wa nyimbo za injili Mzee Kitenzogu Makassy akikabidhiwa kadi yake baada ya kujiunga na NHIF.
 Burudani kutoka Kwaya ya Victorous Station ya Mwananyamala ikiendelea.
 Wanakwaya wakibadilishana mawazo katika uzinduzi huo.
 Burudani zikiendelea.
 Waimbaji wa kwaya ya Kanisa la Nabii Flora la Salasala wakitoa burudani.
 Wanakwaya ya Ukombozi ya Kanisa la Anglikana Tegeta wakionesha umahiri wa kumtukuza mungu kwa kuimba.
 Muonekano wa meza kuu katika uzinduzi huo.
 Ushuhuda ukitolewa kuhusu mungu anavyowatendea watu wake miujuzi.
 Mlezi wa chama hicho, Askofu Dk. Rejoyce Ndalima (kushoto), akiwa ameketi na mgeni rasmi mama Joyce Hagu.
 Maofisa wa NHIF kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiwa tayari kuwandikisha wanachama wapa katika uzinduzi huo. Kutoka kulia ni Derick Ndyetabula, Margaret Malangalila na Dk.Fortunatus Salala.
 Mchungaji David Nyanda ambaye ni muimbaji (wa pili kulia), akionesha manjonjo wakati akitoa burudani kwa kuimba katika uzinduzi huo.
 Katibu wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), Stellah Joel akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Waimbaji na maofisa wa NHIF kutoka Kinondoni wakifuatilia uzinduzi huo.
 Rais wa Chamuita, Ado Novemba akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Furaha na shangwe zikiendelea katika uzinduzi huo watu wote mikono juuu.
 Meneja wa NHIF Wilaya ya Kinondoni, Constantine Makala akitoa darasa kuhusu faida za kujiunga na NHIF na jinsi ya kujiunga.
 Dk.Fortunatus Salala wa NHIF akizungumza kwenye uzinduzi huo.
 Mmoja wa waimbaji wa nyimbo za injili akielezea jinsi alivyonufaika na mfuko huo baada ya kujiunga miezi miwili iliyopita pamoja na mke wake.
 Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa, kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Joyce Hagu (kushoto), akionesha kadi za wanachama hao baada ya kuzizindua. Kulia ni Maadam Ruti Mwamfupe.


Na Dotto Mwaibale

WANACHAMA wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (Chamuita), wamejiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ili waweze kupata matibabi ya uhakika pindi watakapo umwa.

Katika hatua nyingine Mlezi wa chama hicho Askofu Rejoyce Ndalima amewataka waimbaji wa nyimbo za injili kujianzishia miradi mbalimbali itakayowaingizia kipato badala ya kutegemea uimbaji pekee na amewasihi wanamuziki hao kuachana na utamaduni wa kudurufu (kukopi) kazi za wenzao badala yake wawe wabunifu katika kutunga nyimbo zao.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya Afya kwa wanachama wa chama hicho Dar es Salaam jana kupitia Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Ndalima alisema kuokoka sio kuwa mjinga hivyo ni vyema kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo.

“Kuokoka sio kuwa mjinga kwani kuna fursa za biashara ambapo mnatakiwa kuonesha uwezo wenu wa kuzifanyia kazi ili muweze kujikwamua kiuchumi badala ya kung'ang'ania kazi moja tu ya uimbaji,” alisema Ndalima.

Askofu Ndalima aliwataka waimbaji hao wajiunge na bima ya afya kwani hakuna mtu atakayechangiwa tena pindi atakapoumwa na kama ni msaada mtu husika atasaidia katika masuala mengine.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa Joyce Hagu kutoka, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza kwa niaba ya Naibu Waziri wa wizara hiyo, alisema Serikali ipo katika mchakato wa kuanzisha mfuko wa wasanii kutokana na kutambua mchango wao katika jamii.

Hagu aliipongeza NHIF kwa kufikisha huduma hiyo kwa waimbaji hao kwani itawasaidia katika maisha yao hasa pale watakapohitaji kutibiwa katika Hospitali mbalimbali.

Meneja NHIF  Wilaya ya Kinondoni,  Constantine Makala alisema kuwa huduma hiyo watalipia 76800 kwa mwaka mzima.


Alisema watu wote waliojiunga na huduma hiyo wanaweza kupa matibabu katika Hospitali zilizoainishwa pamoja na kupata dawa katika maduka 200 yaliyosajiliwa na NHIF.