Pages

KAPIPI TV

Friday, November 27, 2015

UNIDO YAPIGA JEKI VIWANDA VIDOGO VYA MAFUTA YA ALIZETI DODOMA

IMG_2196
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga akitoa maelezo jinsi kiwanda hicho kinavyofanya kazi zake kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) aliyeambatana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (kulia) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa mjini Dodoma. (Picha na Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
Kutoratibiwa kwa mbegu za alizeti na ukosefu wa mitaji umeelezwa kuwa changamoto kubwa kwa wasindikaji wadogo wa mafuta ya mbegu ya alizeti katika kuendesha viwanda vyao kwa gharama nafuu.
Hayo yameelezwa na Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO) Vedastus Timothy wakati akizungumza na waandishi wa habari walioambatana na Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Alvaro Rodriguez.
Mratibu huyo alikuwa Dodoma kwa shughuli mbalimbali za ukaguzi wa miradi pamoja na kuhudhuria shughuli za bunge la Tanzania lililomalizika jana.
Timothy alisema kwamba pamoja kuwepo kwa taarifa za kuwepo kwa mbegu za kutosha nchini Tanzania,hali halisi inayoelezwa na wasindikaji inaashiria kwamba sekta hairatibiwi vyema kwani wasindikaji hukaa muda mrefu bila kuwa na mbegu za kusindika.
Aidha alisema kwamba mbegu za alizeti zinazovunwa kuanzia Aprili hadi Julai na huwa na bei nafuu kipindi hicho lakini kama wasindikaji wakikosa mitaji na kununua mbegu chache, msimu unapoisha hawawezi tena kuendelea kufungua viwanda vyao.
Alisema kwamba wasindikaji hao wanakumbana na kiwango kikubwa cha riba kuanzia asilimia 20 kwenda juu , riba ambayo inakwamisha maendeleo ya viwanda hivyo.
IMG_2202
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia), Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa pili kushoto), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (katikati) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (wa pili kulia) wakipata picha ya ukumbusho katika matanki ya kuhifadhia mafuta ya alizeti kiwandani hapo.
Hata hivyo alipoulizwa wanafanya nini katika kusaidia wasindikaji hao kukabiliana na hali hiyo alisema kwamba kupitia kongano hilo na Shirikisho la wasindikaji wadogo wa alizeti kanda ya mashariki na kati (CEZOSOPA). wana mipango ya kuwezesha wasindikaji hao kuwa na nguvu katika soko na kuwa na uwezo wa kupata mitaji bila gharama kubwa.
Aidha kupitia kongano hilo chama hicho kitawezeshwa uboreshwaji wa viwanda vya wanachama wake ili viweze kushindana na kukidhi viwango vya Shirika la Viwango nchini Tanzania (TBS).
Wakala huyo alisema hayo katika mahojiano yaliyofanyika kufuatia ziara ya mradi wa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez kwenye kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya Dodoma, kinachonufaika na mradi wa ubia wa uboreshaji viwanda kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Wizara ya Viwanda na Biashara (TIUMP).
Kwa mujibu wa taarifa ya UNIDO, taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa inachangia kuimarika kwa sekta ya viwanda vidogo na vya kati vya usindikaji mafuta na kuviweka katika ushindani.
Aidha kupitia UNIDO ni viwanda hivyo vinawekwa katika hali ya kukua kuwa viwanda vikubwa.
IMG_2212
Mfanyakazi wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya Alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Alpha Manyanga akiwa kwenye mashine ya kuchujia mafuta kiwanda hapo.
Katika ushirika wa aina hiyo ni matarajio ya mradi huo kufanikisha juhudi za kupunguza umaskini kama moja ya malengo ya maendeleo endelevu yanayotarajiwa na dunia.
Aidha katika upunguzaji huo wa umaskini mradi utachangia ongezeko la fursa za ajira na ukuaji wa uchumi.
Mkoa wa Dodoma wenye viwanda vya kusindika mbegu za alizeti vinavyofanyakazi katika mkaazi wakitumia zana dhaifu na vifungashia visivyokuwa na ishara yoyote ile na kuuza bidhaa zao kando mwa barabara wanahitaji mfumo thabiti wa ukuzaji wa shughuli zao na kueleweka.
Kutokana na mazingira hayo wajasirimali hawa hujikuta wakiingia hasara kubwa kwa kupoteza tija na pia soko lenye uhakika.
Kutokana na madhara hayo na pia kukosa hati ya ubora kwa kukosa mazingira yanayoruhusu hati hiyo kutolewa, TIUMP imelenga kusaidia wasindikaji hawa na teknolojia sahihi inayohitajika ili watoke pale walipo na kuwa na viwanda vidogo au vya kati.
Ingawa kwa sasa UNIDO inasaidia viwanda vinane vya mbegu za alizeti ili kuweza kuboresha bidhaa zao na utendaji kuna muonekano wa maendeleo makubwa siku za usoni hasa kwa wanachama wa CEZOSOPA ambao wameuinganishwa pamoja kwa ajili ya misaada mbalimbali ya kuwawezesha kuwa washindani katika soko.
IMG_2216
Mtaalamu wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid (aliyeipa mgongo kamera) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (kushoto) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (kulia) walipokua wakikagua mtambo wa kusafisha mafuta (Semi re-finery) uliofadhiliwa na UNIDO kiwandani hapo.
UNIDO wanatumia maarifa waliyojifunza Ethiopia kuimarisha wanachama wa CEZOSOPA ambao tayari wamekubali kuunda kampuni ya pamoja na kuwekeza katika kitu wanachokifanya kwa pamoja kwa lengo la kuongeza uwezo na ushindani katika soko.
Halmashauri ya Chamwino tayari imekubali kuipa ardhi CEZOSOPA kwa ajili ya uwekezaji huo mkubwa.
Aidha UNIDO imewezesha kupatikana kwa teknolojia rahisi kwa ajili ya usafishaji wa mafuta ya alizeti na teknolojia hiyo inafanyiwa kazi na VETA.
UNIDO wamesema teknolojia hiyo hiyo inasaidia kuweka mafuta katika viwango vinavyotakiwa kitaifa na kimataifa na kwamba teknolojia hiyo tayari inafanyakazi nchini katika viwanda viwili na vingine saba vimeonesha nia ya kupata teknolojia hiyo.
Imeelezwa kuwa fedha za mradi huo zinapatikana kutoka UNIDO na wadau wengine kama SIDA na UNDAP.
IMG_2233
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto akipozi kwa picha.
IMG_2237
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akifurahi jambo alipokuwa akipewa maelezo na Mtaalamu wa Chakula kutoka CEZOSOPA, Sophia Majid (kulia) ya mtambo mahususi wa kusafisha mafuta (Semi re-finery) uliofahdhiliwa na UNIDO.
IMG_2252
 
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (wa pili kushoto) akimuongoza Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe wake kukagua mradi huo unaofadhiliwa na UNIDO.
IMG_2324
Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO), Vedastus Timothy akizungumza na waandishi wa habari nje ya kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya Dodoma.
IMG_2257
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia) akiendelea kutoa maelezo ya namna wanavyojaza mafuta yao kwenye vigungashio wakati walipotembelea na ugeni kutoka Umoja wa Mataifa ulioongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.
IMG_2275
Pichani ni madumu yaliyojazwa mafuta ya alizeti kiwandani hapo yakisubiri kuwekwa nembo maalum na tayari kuingia sokoni kwa mlaji.
IMG_2282
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akijaza mafuta wakati wa ziara kwenye kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha cha Glory Farm & Agricultural Products kilichopo katika kijiji cha Nzuguni, manispaa ya Dodoma, kinachonufaika na mradi wa ubia wa uboreshaji viwanda kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Viwanda (UNIDO) na Wizara ya Viwanda na Biashara. Kulia ni mfanyakazi wa kiwanda hicho, Mike Brighton.
IMG_2313
Kutoka Dodoma, Tunapeleka malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini kote .....ni maneno ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa nne kulia), Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (kulia),Wakala wa uendelezaji Kongano la Mafuta ya Alizeti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo la Viwanda (UNIDO), Vedastus Timothy (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Awa Dabo (wa tatu kulia), Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum (wa pili kuhsoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la FAO nchini, Patric Otto (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho.
IMG_2319
Meneja Mkuu wa kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti cha Glory Farm & Agricultural Products, Justin Nyamoga (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wake wakipozi na bango la kuhamasisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
IMG_2381
Afisa Kilimo wa wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, Aizack Chaula (mwenye suti nyeusi) akitoa maelezo kwenye shamba la zabibu la heka 300 lililopo kwenye maandalizi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na ujumbe wake kwenye ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani humo.
IMG_2397
Muonekano wa Shamba hilo la heka 300 ikiwa kwenye maandalizi kwa ajili ya kilimo cha Zabibu.
IMG_2428
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa kikundi cha wakulima wa Zabibu, Sekian Mavunde ili kujua changamoto zinazowakabili katika kikundi chao. Kushoto ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu
IMG_2462
Sehemu ya eneo la shamba la heka 296 zilizopandwa Zabibu.
IMG_2515
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitembelea na kupewa maelezo na Afisa Kilomo wa wilaya ya Chamwino, Aizack Chaula (kulia) kwenye shamba la Zabibu la Chabuma Amlo’s Ltd. lenye ukubwa wa Heka 296 lililopo katika kijiji cha Chinangali II, wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambapo wakulima wa eneo hilo wanaopatiwa msaada chakula kwa vibarua pamoja na kuchimbiwa mitaro bure shambani hapo na Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP). Wengine katika picha ni Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum ( wa pili kushoto) pamoja na Mwakilishi Mkazi wa FAO nchini, Patric Otto (kushoto) waliombatana na Bw. Rodriguez katika ziara hiyo.
IMG_2521
IMG_2522
IMG_2566

Pichani juu na chini ni miche na vitalu vya Zabibu kabla ya kupelekwa shambani.
IMG_2550
IMG_2582

Bwawa la umwagiliaji wa kilimo cha Zabibu katika shamba hilo.
IMG_2632
Pichani juu na chini ni wakulima za kilimo cha Zabibu wakizungumzia changamoto zinazowakabili katika kilimo hicho kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) alipofanya ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini Dodoma.
IMG_2658
IMG_2664
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na wakulima.

DC MAKONDA AZUNGUMZIA KIFO CHA KATIBU WA CHAMA CHA WAFANYAKAZI MADEREVA TANZANIA (TADWU)


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi nje ya chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya kuhusu kifo cha utata cha aliyekuwa Katibu wa chama hicho Tanzania, Rashid Saleh kilichotokea hivi karibuni pamoja na ratiba ya mazishi yake yatakayofanyika jijini Mwanza.
 Marehemu, Rashid Saleh
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye ni mlezi wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADU), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), na wadau wengine kuhusu taratibu za mazishi za katibu huyo.
 Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Stanley Kilave (kulia), akizungumza na Mwenyekiti mstaafu wa chama hicho, Clement Masanja (kushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Pubrishers LTD, Eric Shigongo (katikati), wakati wa taratibu za mazishi zikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Salaam leo.

 Msemaji wa familia ya marehemu, Jonas Marinyizu (katikati), akitoa shukurani kwa DC Makonda na wadau wengine kwa kuwezesha msiba huo pamoja na utaratibu wa mazishi utakavyo kuwa.



Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdem akizungumza katika mkutano na wanahabari

 Ndugu na jamaa wa marehu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha uchunguzi wa mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa mazishi.
Ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakiwa katika chumba za kuhifadhi maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kufanyika taratibu cha uchunguzi wa mwili huo kabla ya kusafirishwa kwenda jijini Mwanza kwa mazishi.


Na Dotto Mwaibale

MWILI wa Katibu Mkuu na Msemaji wa Chama Cha Wafanyakazi Madereva Tanzania (TADWU), Rashid Saleh umesafirishwa jana kwenda kijijini kwao Kayenze wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kwa maziko.

Saleh alifariki jana Novemba 20 Majira ya saa 8 mchana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wakati akipata matibabu ya maradhi ya figo ili kuokoa maisha yake baada ya kile kinachodaiwa kushindwa kufanya kazi ipasavyo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni mlezi wa chama hicho, Paul Makonda alisema kuwa wamepata pigo kutokana na umuhimu na umahiri ambao alikuwa nao marehemu hasa katika kutetea haki za madereva wenzake sanjari na kuibua mambo mbalimbali ambayo yatabaki kuwa historia na kumbukumbu kwao.

"Saleh alifariki jana (Novemba 20) baada ya kusikia anaumwa ambapo hali yake haikuwa nzuri na madaktari walishauri nimlete Muhimbili kwa matibabu zaidi ambapo nilimfikisha lakini baada ya muda mfupi wakati madaktari wanahangaika kumtibu na kuokoa maisha yake alifariki,"alisema.

Alisema marehemu amekiacha chama sehemu ya mafanikio makubwa zaidi ya mabadiliko na mikataba ya haki za madereva nchi nzima huku akibainisha mazingira ya kifo na kutaka uchunguzi zaidi ili kujiridhisha na kifo chake uliofanywa chini ya uangalizi wa polisi.


"Hatukuona kama kuna haja ya kumuhifadhi mwili wa ndugu yetu hadi hapo tutakapojua nini chanzo cha kifo chake kwani majibu ndiyo yatatupa picha ya ugonjwa kwani tumehangaika tangu alipokuwa hospitali ya Kairuki ambapo tulipofika hapa ikabainika kuwa figo zake zote mbili hazifanyi kazi,"alisema.

Aliongeza kuwa marehemu alipelekwa hospitalini hapo kwa kitengo maalum huku akibainisha endapo figo zinashindwa kufanya kazi mzunguko mzima wa damu mwilini nao husimama ambapo madaktari walishirikiana lakini hawakuweza kuokoa maisha yake.


Mwenyekiti wa Chama hicho, Shaban Mdem alisema kuwa msiba huo umewasikitisha sana kutokana na mazingira ya kifo chake huku akiitaka mamlaka husika kulisimamia suala hilo la kupatika kwa majibu sahihi juu ya kifo chake.

"Tunataka uchunguzi ufanyike na majibu yatoke yakiwa sahihi na yanayoridhisha juu ya kifo chake kwani amekufa na madai ambayo yapo ndani yao, hivyo serikali itambue kifo cha Saleh ni katika harakati za kudai haki ambayo tuliyawasilisha mbele ya aliyekuwa waziri mkuu Mizengo Pinda,"alisema. 

Alisema Saleh ni kiongozi wa taifa zima hivyo alimtaka rais Magufuli kuingilia kati suala hilo kwani kutokana na hali hiyo watamaliza wafanyakazi wote kwa kuwauwa katika mazingira kama hayo sambamba na kutenga siku rasmi kwa ajili ya maombezo ya msemaji huyo.

Mazingira ya Kifo

Akizungumzia mazingira ya kifo Msemaji wa Familia ya Marehemu Jonas Ernest alisema kuwa Novemba 9 mwaka huu marehemu alipokea simu kutoka kwa rafiki yake ma kumtaka waende kwenye kikao, ambapo baada ya hapo mwenzake alidai kuwa na njaa.

Alidai baada ya hapo walikwenda kuagiza chakula ambapo mwenzake hakula na kumuacha marehemu akiwa anakula huku mwenzake akiwa amemuaga kwenda msalani."Baada ya kurudi msalani alimkuta marehemu akilalamika tumbo linamuuma na hivyo kuondoka eneo hilo pasi na huyo rafiki kula chochote,"alisema.

Alidai kuwa baada ya kuhisi maumivu makali ya tumbo alianza kuharisha na kutapika na alikimbizwa hospitali lakini uchunguzi ulibaini hakuwa na tatizo na kurudishwa nyumbani ambapo siku inayofuata alirudi hospitali na kuambiwa kuwa ana malaria 4.

"Alianza kutumia dawa za malaria na baadaye kujiskia vibaya na kumrudisha tena hospitali ya Kairuki laikini madaktari walidai kuwa anatatizo ndani ya mwili ambalo ni figo kushindwa kufanya kazi vizuri,"alidai na kuongeza kuwa hadi marehemu anafariki alikaririwa akidai kuwa"Nyama inanitenganisha na mwanangu lakini"na kumtaja mmoja wa wafanyakazi wenzake huku akidai kumuona mtoto wake.  

Harakati za kudai haki ya madereva

Saleh alizaliwa mwaka 1966 Mwanza, ambapo hadi anafariki alikuwa katika harakati za kudai na kutetea haki za madereva ambapo Oktoba 2, mwaka huu alikaririwa akisema wamechoshwa na uozo unaoendelea kufanywa na Mamlaka ya Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumatra) na Wizara ya Kazi na Ajira kuhusu kufumbia macho kero zinazoitatiza sekta ya usafirishaji hasa kwa madereva wa mabasi ya abiria na magari ya mizigo.

MSD YAPELEKA MOI VIFAA VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 251 ZILIZOKUWA ZITUMIKE KUJIPONGEZA WABUNGE

 Magari ya Bohari ya Dawa (MSD), yakishusha vifaa tiba Taasisi ya Moi kufuatia agizo la Rais Dk.John Magufuli kulitaka Bunge kutumia sh.milioni 15 kwa ajili ya kujipongeza na fedha zilizobaki kuzipeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kukabiliana na uhaba wa vifaa tiba na magodoro. 


Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais Dk. John Magufuli.

Vifaa hivyo vilianza kupelekwa juzi katika Taasisi hiyo ili kukabiliana na uhaba alioubaini Rais  Magufuli baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika mapema mwezi huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akizungumzia kuhusu vifaa hivyo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa usambazaji alisema  hivyo vyenye gharama ya sh.milioni .251 ni pamoja na vitanda 300, magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.

Alisema MSD ilianza kupeleka Vifaa hivyo MOI mwishoni mwa wiki na kuwa itaendelea kutoa vifaa hadi wiki hii inayoanza leo.

Fedha hizo zilizotumika kununulia vifaa hivyo zilitokana na agizo la Rais Dk.John Magufuli alilolitoa wakati akilihutubia bunge mjini Dodoma mwishoni mwa wiki ambapo alilitaka bunge kutumia sh.milioni 15 tu kwa ajili ya kujipongeza na kiasi hicho kilichobaki kitumike kununulia vifaa hivyo.

Sunday, November 22, 2015

KONGAMANO LA MABADILIKO YA TABIANCHI LAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO,JIJINI DAR

 Mc katika kongaman0 la Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu
 Eva Mageni  ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, akifungua kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alizungumzia kwa kifupi kuhusu mkutano wa COP21 ambao utafanyika Paris Ufaransa hivi karibuni.
 Edward Tunyone kutoka Forum CC akieleza maana zaidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alielekeza mazungumzo yake katika majanga asilia, mito kupotea kutokana na shughuli za wanadamu kama kulima jirani na maeneo hayo, mwisho alisisitiza swala la mabadiliko ya Tabianchi ni jukumu la kila mtu na taasisi zinazohusika na mamswala hayo tu.
 Bi Mwindiwe makame aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kutoka Zanzibar, akiendelea kueleza maana ya Mabadiliko ya Tabianchi alisisitiza kutunza mazingira.
 Denis Allan kutoka Norwegian Church Aid Actalliance akielezea umuhimu wa kutunza miti.
 Kikundi cha Ngonjela wakiendelea Kuburudisha
 Kushoto ni Mtaalam wa Mitandao ya kijamii toka Forum CC akitoa maelekezo ya shindano la Instagram
 Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza
 Aliyewahi kuwa Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 St.Matha akielezea jambo kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi
 Bw. Gambaedya P.M kutoka Tume ya Ardhi akitoa somo juu ya kilimo hifadhi
 Bi.Tatu Kayumbu kutoka Wizara ya Kilimo akieleza ushirikiano wa kilimo na utunzaji wa Mazingira
 Kundi la Youth can wakiendelea kutumbuiza
 Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akitoa mwongozo wa kikao
 Mkutano wa Forum CC ukiendelea
 Baadhi ya washiriki wakijadili Michoro ambayo walipewa kazi ya kuipitia na kuijadili.
 Baadhi ya washiriki wakielezea michoro waliyopewa kuielezea
Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akijumuika na wananchi wengine katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
 Baadhi ya waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kwa nyakati tofauti wakionesha bidhaa zao
Kushoto ni mmoja wa washiriki waliohudhulia kongamano la mabadiliko ya Tabianchi akipokea zawadi ya tsh 100,000 aliyoshinda Steven Albert.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi

*******
ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance  zafanya kongamano  la Kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula nchini.

Akizungumza  Afisa Miradi Msaidizi wa Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema kuwakilisha sauti za wakulima  kwa serikali katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Alisema  asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo wakati wanapolima.

Sawaya alisema  wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo mbalimbali vya maji  ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

"Kwa kushirikiana  na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian Church Aid  tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza bajeti,"alisema Sawaya
Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha katika uzalishaji wa chakula.

"Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji pamoja na wavuvi  katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na kuwapa mikopo,"alisema

Aidha Kongamano  hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.

"Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya  Mkuu wa  21 wa Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,"alisema Sewaya

Friday, November 20, 2015

KUMBUKUMBU MRS BARKE M. UBAYA

index
MRS BARKE M. UBAYA LEO UMETIMIZA MIAKA MIWILI TANGU UTUTOKE DUNIANI SISI TULIO HAI BADO TUNAKUKUMBUKA KWA UPOLE UCHESHI NA UKARIMU WAKO UNAKUMBUKWA NA MUMEO BW.MWINYI UBAYA WANAO SALAMA NA RAHMA MAMA YAKO FAMILIA YA MAGOHA NA UBAYA JIRANI NA MARAFIKI INSHA'ALLAH M MUNGU AKUSAMEHE MAKOSA YAKO AMIN INNA LILLAH WA INNA LILLAH RAJIUN

JAMESON YAANDAA PRE-PARTY GEORGE AND DRAGON DAR KUELEKEA JAMESON LIVE PARTY ITAKAYOFANYIKA NAIROBI


  • Mshindi mmoja kujishindia tiketi ya watu wawili kwenda Kenya kwenye party ya Jameson itakayotumbuizwa na B.O.B

Jameson inaandaa pre-party itakayofanyika tarehe 21 ya mwezi huu katika bar ya George and Dragon jijini Dar es Salaam.
Watumiaji wa Jameson watakaonunua chupa ya kinywaji hicho watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda tiketi ya kwenda Kenya kushuhudia party ya Jameson itakayofanyika hapo tarehe 12, December.
Jameson Live 2015 Party, inamleta msanii wa hiphop kutoka Marekani, Bobby Ray Simons, maarufu kama B.O.B, ambayo itafanyika Ngong Racecourse hapo tarehe 12 December.
Rapa huyo mzaliwa wa Atlanta amezungumzia kuhusu show yake hiyo ya Nairobi katika ukurasa wake wa Facebook, akiwataka mashabiki wake wajiandae kwa show kali.
B.O.B ambaye alitambulika katika ulimwengu wa muziki kupitia kupitia mixtape yake ya Cloud 9, amefanikiwa kufanya show sehemu mbalimbali duniani huku wimbo wake wa ‘Airplanes’ na ‘Nothing on You’ aliyomshirikisha Bruno Mars zikiongoza chati mbalimbali za mziki duniani.
Nyimbo zake za hivi karibuni kama ‘So Good’ na ‘Headband’ nazo zimefanikiwa kumfanya B.O.B kuwa mmoja ya wanamuziki wakubwa duniani.

Huku akiwa ameshinda tuzo mbalimbali za BET, MTV pamoja na Teen Choice na huku akifanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo za Grammy zaidi ya mara sita, B.O.B ameshawahi kufanya show na wanamuziki mahiri kama Janelle Monae, Eminem, Linkin Park, Kanye West, Drake, Usher, Paramore na wengine wengi.

Jameson wamejipanga kukuza viwango vya burudani kwa nchi za Afrika Mashariki na awamu hii wamejipanga kwa kuwapa burudani ya pekee mashabiki watakaohudhuria burudani hiyo huku wakizidi kuwekeza zaidi katika kuwaleta wasanii wa kimataifa.
                                                                                            
Mwaka 2014 Jameson ilifanikiwa kuandaa matamasha mawili makubwa nchini Kenya ambayo yote tiketi zake zilimalizika kabla huku la kwanza burudani ikitolewa na wasanii wa ndani, na la pili burudani ilitolewa na msanii 2 Chainz huku balozi mashuhuri wa Afrika Akon akihudhuria pia.

Akizungumzia kuhusu show hiyo, Balozi wa Jameson, Antony Owich amesema party ya mwaka huu itazidi kuwa kubwa na bora kuliko miaka iliyopita.

‘Jameson imejikita katika kuwapa kumbukumbu za kipekee mashabiki wake na kwa mwaka huu inawaahidi kuwapa burudani ya pekee kabisa na watu wasikose kuhudhuria’ alisema Owich.







UN WAZINDUA MRADI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI,CHAMWINO DODOMA

ALVARO KUPANDA MTI-2

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
ALVARO MWAGILIA MAJI-3
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimwagilia maji kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
ALVARO NA BURUDANI-2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo (kulia) wakieleka kukagua mradi wa ufugaji wa shirika la Tanzania Environmental Friendly Association (TEFA) huku wakiburudishwa na ngoma ya wenyeji wa kabila wa Kigogo, katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
ALVARO NA MAJI-2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma, Zena Mwalko baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.
ALVARO NA WANANGOMA
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa kwenye picha ya pamoja na wanakikundi cha ngoma cha Kijiji cha Machali A, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.
ALVARO ZUNGUMZA
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Machali A, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo. Kutoka kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum.
AWA KUBEBA NDOO
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo akiwa amebeba ndoo ya maji baada ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na wanakijiji wakishuhudia tukio hilo.
AWA KUPANDA MTI-3
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
DK HASHINA KUPANDA MTI-2
Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum akimwagilia maji mti kama ishara ya kutunza mazingira baada ya uzinduzi wa wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
YOHANA KUPANDA MTI-3
Mratibu wa Mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District) kutoka Shirika la Tanzania Environmental Friendly Association (TEFA), Yohana Kadiva akimwagilia maji mti kama ishara ya kutunza mazingira baada ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la Mpango wa Maendeleo (UNDP).
NGOMA
Wanakikundi cha ngoma ya asili katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakiburudisha wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
UZINDUZI MRADI
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo.