Pages

KAPIPI TV

Friday, November 27, 2015

MSD YAPELEKA MOI VIFAA VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 251 ZILIZOKUWA ZITUMIKE KUJIPONGEZA WABUNGE

 Magari ya Bohari ya Dawa (MSD), yakishusha vifaa tiba Taasisi ya Moi kufuatia agizo la Rais Dk.John Magufuli kulitaka Bunge kutumia sh.milioni 15 kwa ajili ya kujipongeza na fedha zilizobaki kuzipeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kukabiliana na uhaba wa vifaa tiba na magodoro. 


Na Dotto Mwaibale

BOHARI ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo alilotoa Rais Dk. John Magufuli.

Vifaa hivyo vilianza kupelekwa juzi katika Taasisi hiyo ili kukabiliana na uhaba alioubaini Rais  Magufuli baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika mapema mwezi huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akizungumzia kuhusu vifaa hivyo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa usambazaji alisema  hivyo vyenye gharama ya sh.milioni .251 ni pamoja na vitanda 300, magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.

Alisema MSD ilianza kupeleka Vifaa hivyo MOI mwishoni mwa wiki na kuwa itaendelea kutoa vifaa hadi wiki hii inayoanza leo.

Fedha hizo zilizotumika kununulia vifaa hivyo zilitokana na agizo la Rais Dk.John Magufuli alilolitoa wakati akilihutubia bunge mjini Dodoma mwishoni mwa wiki ambapo alilitaka bunge kutumia sh.milioni 15 tu kwa ajili ya kujipongeza na kiasi hicho kilichobaki kitumike kununulia vifaa hivyo.

Sunday, November 22, 2015

KONGAMANO LA MABADILIKO YA TABIANCHI LAFANYIKA KATIKA KIJIJI CHA MAKUMBUSHO,JIJINI DAR

 Mc katika kongaman0 la Mabadiliko ya Tabianchi kutoka Oxfam Tanzania Suhaila Thawer akiendelea kutoa utaratibu
 Eva Mageni  ambaye ni Rais wa wakulima wanawake vijijini na alikuwa mshiriki wa shindano la Mama shujaa wa Chakula 2015, akifungua kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alizungumzia kwa kifupi kuhusu mkutano wa COP21 ambao utafanyika Paris Ufaransa hivi karibuni.
 Edward Tunyone kutoka Forum CC akieleza maana zaidi ya Mabadiliko ya Tabianchi ambapo alielekeza mazungumzo yake katika majanga asilia, mito kupotea kutokana na shughuli za wanadamu kama kulima jirani na maeneo hayo, mwisho alisisitiza swala la mabadiliko ya Tabianchi ni jukumu la kila mtu na taasisi zinazohusika na mamswala hayo tu.
 Bi Mwindiwe makame aliyekuwa mshiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kutoka Zanzibar, akiendelea kueleza maana ya Mabadiliko ya Tabianchi alisisitiza kutunza mazingira.
 Denis Allan kutoka Norwegian Church Aid Actalliance akielezea umuhimu wa kutunza miti.
 Kikundi cha Ngonjela wakiendelea Kuburudisha
 Kushoto ni Mtaalam wa Mitandao ya kijamii toka Forum CC akitoa maelekezo ya shindano la Instagram
 Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza
 Aliyewahi kuwa Mshindi wa Mama Shujaa wa Chakula 2012 St.Matha akielezea jambo kuhusiana na mabadiliko ya Tabianchi
 Bw. Gambaedya P.M kutoka Tume ya Ardhi akitoa somo juu ya kilimo hifadhi
 Bi.Tatu Kayumbu kutoka Wizara ya Kilimo akieleza ushirikiano wa kilimo na utunzaji wa Mazingira
 Kundi la Youth can wakiendelea kutumbuiza
 Meneja wa Kampeni Haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akitoa mwongozo wa kikao
 Mkutano wa Forum CC ukiendelea
 Baadhi ya washiriki wakijadili Michoro ambayo walipewa kazi ya kuipitia na kuijadili.
 Baadhi ya washiriki wakielezea michoro waliyopewa kuielezea
Kushoto ni Mkurugenzi mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akijumuika na wananchi wengine katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi
 Baadhi ya waliokuwa washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula kwa nyakati tofauti wakionesha bidhaa zao
Kushoto ni mmoja wa washiriki waliohudhulia kongamano la mabadiliko ya Tabianchi akipokea zawadi ya tsh 100,000 aliyoshinda Steven Albert.
Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Mabadiliko ya Tabianchi

*******
ASASI za Kiraia nchini zikiwemo Oxfam Tanzania, Forum CC na Norwegian Church Aid Actalliance  zafanya kongamano  la Kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa Chakula nchini.

Akizungumza  Afisa Miradi Msaidizi wa Shirika la Forum CC,Jonathan Sawaya alisema asasi hizo zimeona ni vema kuwakilisha sauti za wakulima  kwa serikali katika kuhakikisha hatua stahiki zinachukuliwa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Alisema  asilimia kubwa ya wakulima wengi hasa wanawake ambao karibia asilimia 70 wamekuwa wakiathirika na Mabadiliko hayo wakati wanapolima.

Sawaya alisema  wananchi wanapaswa kuhifadhi mazingira na kutunza vyanzo mbalimbali vya maji  ili kupunguza athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.

"Kwa kushirikiana  na shirika la Oxfam pamoja na Norwegian Church Aid  tumeamua kufanya kongamano hili ili kupaza sauti za wakulima na wafugaji katika suala zima la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na serikali kutilia mkazo katika kusimamia suala hili kwa kuongeza bajeti,"alisema Sawaya
Aidha alisema asilimia kubwa ya wanawake wameonyesha juhudi mbalimbali za kukabiliana na athari hizo kutokana na wao kujihusisha katika uzalishaji wa chakula.

"Tuwaunge mkono wazalishaji wa chakula wadogo,wafugaji pamoja na wavuvi  katika suala hili kwa kuwaunganisha na masoko na kuwapa mikopo,"alisema

Aidha Kongamano  hili limehusisha wadau mbalimbali wakiwemo watendaji wa serikalini,wakulima pamoja na wafugaji katika kuhakikisha mabadiliko ya tabia nchi yanatokomezwa.

"Kongamano hili ni sehemu ya maandalizi ya  Mkuu wa  21 wa Mkutano wa kimataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi unaotarajia kufanyika Novemba 30 nchini Ufaransa,"alisema Sewaya

Friday, November 20, 2015

KUMBUKUMBU MRS BARKE M. UBAYA

index
MRS BARKE M. UBAYA LEO UMETIMIZA MIAKA MIWILI TANGU UTUTOKE DUNIANI SISI TULIO HAI BADO TUNAKUKUMBUKA KWA UPOLE UCHESHI NA UKARIMU WAKO UNAKUMBUKWA NA MUMEO BW.MWINYI UBAYA WANAO SALAMA NA RAHMA MAMA YAKO FAMILIA YA MAGOHA NA UBAYA JIRANI NA MARAFIKI INSHA'ALLAH M MUNGU AKUSAMEHE MAKOSA YAKO AMIN INNA LILLAH WA INNA LILLAH RAJIUN

JAMESON YAANDAA PRE-PARTY GEORGE AND DRAGON DAR KUELEKEA JAMESON LIVE PARTY ITAKAYOFANYIKA NAIROBI


  • Mshindi mmoja kujishindia tiketi ya watu wawili kwenda Kenya kwenye party ya Jameson itakayotumbuizwa na B.O.B

Jameson inaandaa pre-party itakayofanyika tarehe 21 ya mwezi huu katika bar ya George and Dragon jijini Dar es Salaam.
Watumiaji wa Jameson watakaonunua chupa ya kinywaji hicho watafanikiwa kuingia moja kwa moja kwenye droo ya kushinda tiketi ya kwenda Kenya kushuhudia party ya Jameson itakayofanyika hapo tarehe 12, December.
Jameson Live 2015 Party, inamleta msanii wa hiphop kutoka Marekani, Bobby Ray Simons, maarufu kama B.O.B, ambayo itafanyika Ngong Racecourse hapo tarehe 12 December.
Rapa huyo mzaliwa wa Atlanta amezungumzia kuhusu show yake hiyo ya Nairobi katika ukurasa wake wa Facebook, akiwataka mashabiki wake wajiandae kwa show kali.
B.O.B ambaye alitambulika katika ulimwengu wa muziki kupitia kupitia mixtape yake ya Cloud 9, amefanikiwa kufanya show sehemu mbalimbali duniani huku wimbo wake wa ‘Airplanes’ na ‘Nothing on You’ aliyomshirikisha Bruno Mars zikiongoza chati mbalimbali za mziki duniani.
Nyimbo zake za hivi karibuni kama ‘So Good’ na ‘Headband’ nazo zimefanikiwa kumfanya B.O.B kuwa mmoja ya wanamuziki wakubwa duniani.

Huku akiwa ameshinda tuzo mbalimbali za BET, MTV pamoja na Teen Choice na huku akifanikiwa kuchaguliwa kuwania tuzo za Grammy zaidi ya mara sita, B.O.B ameshawahi kufanya show na wanamuziki mahiri kama Janelle Monae, Eminem, Linkin Park, Kanye West, Drake, Usher, Paramore na wengine wengi.

Jameson wamejipanga kukuza viwango vya burudani kwa nchi za Afrika Mashariki na awamu hii wamejipanga kwa kuwapa burudani ya pekee mashabiki watakaohudhuria burudani hiyo huku wakizidi kuwekeza zaidi katika kuwaleta wasanii wa kimataifa.
                                                                                            
Mwaka 2014 Jameson ilifanikiwa kuandaa matamasha mawili makubwa nchini Kenya ambayo yote tiketi zake zilimalizika kabla huku la kwanza burudani ikitolewa na wasanii wa ndani, na la pili burudani ilitolewa na msanii 2 Chainz huku balozi mashuhuri wa Afrika Akon akihudhuria pia.

Akizungumzia kuhusu show hiyo, Balozi wa Jameson, Antony Owich amesema party ya mwaka huu itazidi kuwa kubwa na bora kuliko miaka iliyopita.

‘Jameson imejikita katika kuwapa kumbukumbu za kipekee mashabiki wake na kwa mwaka huu inawaahidi kuwapa burudani ya pekee kabisa na watu wasikose kuhudhuria’ alisema Owich.







UN WAZINDUA MRADI WA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI,CHAMWINO DODOMA

ALVARO KUPANDA MTI-2

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
ALVARO MWAGILIA MAJI-3
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimwagilia maji kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
ALVARO NA BURUDANI-2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo (kulia) wakieleka kukagua mradi wa ufugaji wa shirika la Tanzania Environmental Friendly Association (TEFA) huku wakiburudishwa na ngoma ya wenyeji wa kabila wa Kigogo, katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma katika utekelezaji wa moja kati ya malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
ALVARO NA MAJI-2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma, Zena Mwalko baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.
ALVARO NA WANANGOMA
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa kwenye picha ya pamoja na wanakikundi cha ngoma cha Kijiji cha Machali A, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo.
ALVARO ZUNGUMZA
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Machali A, wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo. Kutoka kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo na Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum.
AWA KUBEBA NDOO
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo akiwa amebeba ndoo ya maji baada ya uzinduzi wa mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez pamoja na wanakijiji wakishuhudia tukio hilo.
AWA KUPANDA MTI-3
Mkurugenzi Mkazi wa UNDP, Awa Dabo akipanda mti kama ishara ya uhifadhi mazingira baada ya kuzindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
DK HASHINA KUPANDA MTI-2
Mwakilishi Msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dk. Hashina Begum akimwagilia maji mti kama ishara ya kutunza mazingira baada ya uzinduzi wa wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), katika Kijiji cha Machali A, wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
YOHANA KUPANDA MTI-3
Mratibu wa Mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District) kutoka Shirika la Tanzania Environmental Friendly Association (TEFA), Yohana Kadiva akimwagilia maji mti kama ishara ya kutunza mazingira baada ya uzinduzi wa mradi huo unaofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kupitia Shirika lake la Mpango wa Maendeleo (UNDP).
NGOMA
Wanakikundi cha ngoma ya asili katika kijiji cha Machali A wilayani Chamwino mkoa wa Dodoma wakiburudisha wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo.
UZINDUZI MRADI
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akizindua mradi wa kupunguza na kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi kwa kutumia nishati jadidifu ya jua (Mitigating Climate change in vulnerable communities of Dodoma region, Machali village, Chamwino District), kijijini humo.

BALOZI WA UINGEREZA NCHINI AONGOZA UZINDUZI WA FILAMU YA KUPINGA UKEKETAJI YA SIMULIZI HALISI YA GHATI NA RHOBI

 Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE, wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Filamu ya Simulizi halisi ya Ghati na Rhobi ulifanyika nyumbani kwa balozi huyo, Oysterbay Dar es Salaam jana.
 Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose (kulia), akizungumza kabla ya uzinduzi wa filamu hiyo.
 Mwakilishi kutoka taasisi ya DFID, Jane Miller OBE (kushoto), akizungumza katika uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake Tanzania, Mary Rusimbi (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Wadau mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
 Sehemu ya filamu hiyo inavyoonekana.
 Sehemu ya filamu hiyo inavyoonekana.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward), Naana Otoo-Oyortey MBE (katikati), akichangia jambo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti (kulia), akielezea kuhusu filamu hiyo na changamoto mbalimbali za ukeketaji nchini.


Na Dotto Mwaibale

LICHA ya MKOA wa Dar es Salaam kuwa na watu wenye uelewa mkubwa lakini unaongoza kwa asilimia 38 ya ukeketaji imeelezwa.

Hayo yalibanishwa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto Wizara ya Wanawake na Watoto, Margaret Mussai Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Simulizi halisi ya Ghati na Rhobi uliofanyika nyumbani kwa Balozi wa Uingereza hapa nchini.

"Hali ya ukeketaji hapa nchini bado ni changamoto kubwa kutokana na jamii kutokuwa na uelewa mkubwa ikiwa ni pamoja na mila za baadhi ya makabila" alisema Mussai.

Alisema suala la ukeketaji limekuwa na changamoto kubwa kwa sababu ya wahusika wanaofanya ukeketaji wanatengeneza fedha na kwa msichana anayefanyiwa kitendo hicho anaonekana kuwa na thamani kuliko yule ambaye hajakeketwa.

Alisema kwa mkoa wa Dar es Salaam kuna maeneo ambayo yanaongoza kwa ukeketaji na wasichana hupenda kufanyiwa hivyo ili waonekane wenye heshima.

Alisema mkoa wa Dar es Salaam una asilimia 38 ya ukeketaji, Mara asilimia 58, Shinyanga asilimia 55 huku ikifuatia mikoa mingine.

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Dianna Melrose filamu hiyo inawahusu wasichana wawili ambao wanapinga ukeketaji katika jamii yao.

Alisema wasichana hao waqnaonesha ujasiri wa kukataa kitendo hicho chenye maumivu makali na kwa msaada wanafanikiwa kubadisha jinsi jamii yao inavyomchukulia msichana katika kipindi chake cha mpito kutoka usichana hadi kwenda kufikia utu uzima.

"Filamu hii inaonesha kwamba si jamii zote ndani ya Tanzania zinazojihusisha na ukeketaji na kwamba maeneo mengi wameamua kuachana na ukeketaji na kuamini kwamba ukeketaji unawezwa kutokomezwa" alisema Melrose.

Alisema mtoto wa kike ana haki ya kusomeshwa na kuendelezwa badala ya kuachwa nyumbani na kufanyiwa vitendo hivyo vinavyodumaza jamii kimaendeleo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), Koshuma Mtengeti alisema changamoto kubwa ni sheria ya makosa ya ukeketaji kuto kuwa na meno kwani ni mtu mmoja tu aliyehukumiwa kati ya watu 43 waliobainika na makosa hayo.  


Filamu hiyo imeandaliwa na ubalozi huo kwa kushirikiana na Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) na Mfuko wa Wanawake wa Afya, Utafiti na Maendeleo (Forward).




Wednesday, November 18, 2015

KAMPUNI YA SIMU YA TIGO YATOA SH. MILIONI 200 KUDHAMINI KILIMANJARO MARATHON 2016

 Meneja Mawasiliano wa  Kampuni ya Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), katika hafla ya kuzindua msimu mpya wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016. Tigo wametoa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya mbio hizo.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge (wa tatu kulia), pamoja na wadhamini wa Kilimanjaro Marathon 2016, wakifyatua fataki za karatasi ikiwa ni ishara ya kuzindua maandalizi ya mbio hizo Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa mashindano hayo, John Bayo
 Mkurugenzi wa mashindano hayo, John Bayo (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
 Wadau wa michezo na waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo.
  Mkurugenzi Msaidizi wa Michezo Wizara ya Habari Vijana, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge (katikati), akizungumza na wadau wa michezo wakati akizindua maandalizi hayo ya Kilimanjaro Marathon 2016.
Wanahabari wakichukua taarifa za uzinduzi huo.